Tangu Fastjet waondoke umepanda ndege mara ngapi ?

Tangu Fastjet waondoke umepanda ndege mara ngapi ?

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Nimejikuta nazikumbuka sana monents za Fast Jet miaka ya 2010's

Ni kipindi nachoweza kusema nilitoa ushamba wa ndege, ndege ilikuwa kama basi la mkoani.

Ilikuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa watu wenye uchumi wa kawaida.

Ndege zilikuwa zinajaa inabidi ukate ticket mapema,

Nilichokuwa nawapendea nje ya bei rafiki ni kujali ratiba, ukifika uwanjani una uhakika wakuondoka muda uliopangwa.

Tangu Fastjet waondoke nimepanda ndege mara 2 tu, Ni mara moja tu nimekata tiketi kwa pesa yangu ilikuwa ni emergency, safari nyingine ilikuwa ya kikazi sikulipia tiket,

Nimeshazoea mabasi, ninasafiri inaponilazimu tu, SGR ikisambazwa mikoani itakuwa vema zaidi
 
Nimejikuta nazikumbuka sana monents za Fast Jet miaka ya 2010's

Ni kipindi nachoweza kusema nilitoa ushamba wa ndege, ndege ilikuwa kama basi la mkoani.

Ilikuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa watu wenye uchumi wa kawaida.

Ndege zilikuwa zinajaa inabidi ukate ticket mapema,

Nilichokuwa nawapendea nje ya bei rafiki ni kujali ratiba, ukifika uwanjani una uhakika wakuondoka muda uliopangwa.

Tangu Fastjet waondoke nimepanda ndege mara 2 tu, moja ni emergency nyingine ni kikazi [emoji23][emoji23]
Magufuli aliua fastjet ila Mungu anamuona nilaka zaidi ya miaka 3 bila kupanda basi za mikoani, ila sasa hao wa Air Tanzania ni bogus safari zao ni kubahatisha tu.
 
Ungeandika tangu wafurumushwe, hawakuondoka kwa hiari yao walifanyiwa mizengwe ili atc wadunde wenyewe. Ule ushindani wa gharama hili shirika lisingepata wateja
 
Niliwatoa kule nikawaleta hadi hapa - J.M. Kikwete.
 
FastJet ingekuwepo nadhani ATC wangekua na adabu; hawajali muda, hawajali ratiba zao wenyewe; lakini hata bei zao sio za ukweli; unaweza kufanya booking leo then wakakuruhusu ufanye malipo may be siku fulani, siku unafanya malipo unashangaa hupati access ya kulipa, ukiwapigia simu wanakwambia Kuna mabadiriko ya bei. Staff wa ATC kwa mtazamo wangu, walitakiwa ku operate biashara ya ndege miaka ya 1980's huko, sio sasa. Hawajui kama watu wana connect ndege kwenda nje ya nchi, na wala hutawasikia wakiomba msamaha. FastJet wakirudi, ATC inakufa
 
Umenikumbusha enzi za bata mkuu. Niko chuo Mbeya kila weekend nipo dar j3 nageuza Mbeya Lecture unaatend kama kawaida. Kuna Accountant wa chuo alikuwa mshkaj wangu kila weekend anasepa dar alikuwa na familia huko j3 anageuza mbeya. Namkubali sana yule mkuu ameniunganisha na watu wakubwa. Alikuwa ananitania ole wako ufeli unakula bata mno. Sio sasa hiv ATCL wanazingua na bomberdier zao upepo ukiwa mwingi vinasukumwa huku na Kule kama ngalawa na hapo imekutoka pesa ndefu tu. Fast jet ilikuwa airbus dakika almost 40 ushaingia songwe airpot
 
Back
Top Bottom