Tangu lini Mikopo ikawa mbadala wa kulipa Kodi?

Kategitiwa mlaji wa mwisho
Mlaji wa mwisho ni sawa na ngombe asiyepewa majani na chakula na maji ya kutosha, Kisha wanalazimisha kumkamua,

Sasa inatoka Damu Badala ya maziwa!!

2025, tupeni kupumzika kidogo,

Tumechoka!!
 
Salaam, shalom!!

Nimesikiliza hotuba ya kiongozi wetu mkuu akisema kuwa, waliamua kuongeza Kasi ya kuchukua mikopo Kwa kuwa walijua wananchi wengi ni wakwepa Kodi hawalipi Kodi ipasavyo.

Kwamba mikopo iliyopatikana, ilikwenda kuziba pengo la matumizi ya upungufu wa makusanyo ya Kodi.

Kwamba baada ya kuona kuwa Kuna udhalilishaji mkubwa na masharti magumu katika kuipata mikopo hiyo, sasa ameamua kukusanya Kodi!!

TUJIULIZE MASWALI YAFUATAYO:

1. Ikiwa una wananchi wasiopenda kulipa Kodi, ukikopa, atalipa nani?

2. Je, mikopo ni mbadala wa kulipa Kodi?

3. Kwanini Serikali haipunguzi matumizi ya anasa Ili kidogo kinachokusanywa kitoshe matumizi?

4. Kama Nchi, Kweli tunao viongozi sahihi wenye upeo wa kutuvusha tulipokwama?

5. Kwanini Kodi haikusanywi, na kwanini watu wanakwepa kulipa Kodi ikiwa Kodi wanayowekewa ni sahihi?

6. Mikopo Huwa inakopwa Ili kuongeza kwenye mtaji Ili faida ipatikane Kisha tupate uwezo wa kulipa mkopo au Huwa inachukuliwa kufidia matumizi ya anasa ya Serikali yaliyopungua kutokana na UKWEPAJI Kodi na makusanyo hafifu?

Ongezea maswali mengine na karibu Kwa mjadala🙏
Shule ulienda kusomea ujinga? Mkopo ni suspended tax
 
Yaani namaanisha Kuna substance added kwenye normal feed purposely kupata matokeo wanayoyataka wahusika!!!

Kuna kauli anatoa unahisi hivyo!!

Labda ndio desert mission yenyewe hiyo!
Unamaanisha Yeye haoni hizo hujuma ikiwa zipo na Kupambana nazo kuhakikisha familia inaenda vizuri?

Nini maana ya kuwa kiongozi mkuu wa watu wengi au familia?
 
Shule ulienda kusomea ujinga? Mkopo ni suspended tax
Tumia kiswahili,

Si lazima Kila mtu ajue ulisoma shule za kata Kwa kiingereza Cha mseto!!

Fafanua Kwa kiswahili 🙏
 
Ccm haiwez kuondoka kwa kura. Na kwa akili za watanzania ccm itashinda bila hata kuiba kura maana wanaangalia diamond na shilole wanamuunga mkono nani baso nao wanaenda huko.
Wengine wanachanganya na kiingerrza cha cartel
Si Kweli,

Majimbo mengi CCM wamewahi kushindwa na yakaongozwa na upinzani Kwa Katiba hii hii.

Wananchi tuchukue tu hatua.
 
Salaam, shalom!!

Nimesikiliza hotuba ya kiongozi wetu mkuu akisema kuwa, waliamua kuongeza Kasi ya kuchukua mikopo Kwa kuwa walijua wananchi wengi ni wakwepa Kodi hawalipi Kodi ipasavyo.

Kwamba mikopo iliyopatikana, ilikwenda kuziba pengo la matumizi ya upungufu wa makusanyo ya Kodi.

Kwamba baada ya kuona kuwa Kuna udhalilishaji mkubwa na masharti magumu katika kuipata mikopo hiyo, sasa ameamua kukusanya Kodi!!

TUJIULIZE MASWALI YAFUATAYO:

1. Ikiwa una wananchi wasiopenda kulipa Kodi, ukikopa, atalipa nani?

2. Je, mikopo ni mbadala wa kulipa Kodi?

3. Kwanini Serikali haipunguzi matumizi ya anasa Ili kidogo kinachokusanywa kitoshe matumizi?

4. Kama Nchi, Kweli tunao viongozi sahihi wenye upeo wa kutuvusha tulipokwama?

5. Kwanini Kodi haikusanywi, na kwanini watu wanakwepa kulipa Kodi ikiwa Kodi wanayowekewa ni sahihi?

6. Mikopo Huwa inakopwa Ili kuongeza kwenye mtaji Ili faida ipatikane Kisha tupate uwezo wa kulipa mkopo au Huwa inachukuliwa kufidia matumizi ya anasa ya Serikali yaliyopungua kutokana na UKWEPAJI Kodi na makusanyo hafifu?

7. Nikisema kuwa tunelekea hatua ya kutokopesheka Kwa kushindwa kulipa mikopo nitakuwa nimekosea?

Ongezea maswali mengine na karibu Kwa mjadala🙏
Mambo ya hovyo sana!
 
Back
Top Bottom