Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 384
- 970
Bodi ya Ligi imetoa marekebisho na maboresho ya kanuni toleo la 2023 ambapo hivi sasa ikiwa mchezo atapata dili zake binafsi na benki nyingine basi hawaruhusiwi kutangaza kwa sababu ya mkataba wa NBC Tanzania na Ligi huku atakayekiuka akikabiliwa na kufungiwa kwa kipindi cha kati ya mwezi mmoja na mitatu.
Kwa mujibu wa kanuni namba 16: 1:12 katika maboresho: “Hairuhusiwi kwa mchezaji kuingia mkataba binafsi wa udhamini na mshindani wa kibiashara wa Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu, atakayekiuka atafungiwa kwa kipindi cha kati ya mwezi mmoja na mitatu."
Tukae tukijua, haya mambo ya kimakataba yanataka umakini sana. Kuna wadau huko wanajiuliza; Hivi ni Ligi gani duniani Mdhamini Mkuu wa Ligi anaweza kutosheleza mahitaji ya Vilabu shiriki, au mapato binafsi ya wachezaji? Je, Ligi yetu bado ni amateur?
Je, tumeshindwa ku market Ligi yetu, mpaka kuwa na utegemezi wa Wachezaji na personal issues za Vilabu?
Tunaimba Sponsors na Vilabu vitafute Sponsors, ni Sponsor gani atadhamini Klabu kwa mazingira haya kama akiwa Mshindani na Mdhamini wa Ligi anaminywa kiasi hicho?
Hivi tangu lini TFF au Bodi ya Ligi ikamiliki Image Rights za Wachezaji, ambazo hata Klabu tu ambayo inammiliki mchezaji haina hiyo power, Wanasheria wa Bodi ya Ligi na TFF mnafikiria nini lakini?
Tuna watu sahihi kweli wanaofikiria Mpira wetu na kukwamua Vilabu na wachezaji Kiuchumi? Yes, Viongozi wa Vilabu wana lawama kwa kupitisha hizi kanuni.
Hivi kweli Klabu ipate mdhamini ambaye anaweza kucover angalau 75% ya gharama zake za uendeshaji ashindwe kufanya naye kazi kisa ana ushindani kibiashara na Mdhamini wa Ligi Kuu, ambae hampi uhakika hata kufikisha 10% ya gharama zake.
Tuache kufikiria KIJIMA, duniani kote zawadi ya ushindi baada ya kutwaa kikombe ni za kawaida sana ndio maana majuu huko hamna haya mambo.