Tangu mzee Makamba ahutubie pale Dodoma, walinzi wa legacy wanaweweseka sana

Tangu mzee Makamba ahutubie pale Dodoma, walinzi wa legacy wanaweweseka sana

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Habari kwamba Rais Magufuli ni dikteta ilianza kusemwa na Tundu Lissu ingali bado Magufuli akiwa hai.

Magufuli akaviteka vyombo vyote vya habari, vyombo vya dola, bunge na mahakama. Nchi ikawa kimya hakuna wa kumkosoa wala kumsema vibaya. Aliyethubutu alikiona cha mtema kuni.

Akaeneza propaganda kuwa yeye ni kiongozi wa wanyonge. Media zikauhubiri wema huu kwa nguvu na umma ukaaminishwa hivyo.

Alipofariki, futuhi kila aina zikaandaliwa ili kuendelea kuuaminisha umma kuwa alikuwa mtu wa watu.

Muda wote huo wafuasi wake waliamini wamefanikiwa kupandikiza hiyo imani potofu kuwa Magufuli alikuwa mtu wa watu.

Hotuba ya juzi ya mzee Makamba imewavuruga akili na sasa wanawaza watatoka vipi kwenye kadhia hii inayofuta kabisa legacy ya Magufuli. Wanaweweseka hawajui wafanye nini.
 
Hivi unadhani Average Joe Kitaa ataamini nini ?

Story za Makamba aliyesema ni wakati wao wa kulamba Asali au kuona wapo gizani / umeme haueleweki hence kukumbuka maneno jkuwa watu wanafanya hujuma ili kukuza biashara zao ?

Sifa za JPM hazitokani na Mazuri aliyofanya bali madudu yanayofanyika sasa..., kama vile ambavyo Uchafu wa Mrisho ulimfanya Benja aonekane msafi....
 
Habari kwamba rais Magufuli ni dikteta ilianza kusemwa na Tundu Lissu ingali bado Magufuli akiwa hai.

Magufuli akaviteka vyombo vyote vya habari, vyombo vya dola, bunge na mahakama. Nchi ikawa kimya hakuna wa kumkosoa wala kumsema vibaya. Aliyethubutu alikiona cha mtema kuni.

Akaeneza propaganda kuwa yeye ni kiongozi wa wanyonge. Media zikauhubiri wema huu kwa nguvu na umma ukaaminishwa hivyo.

Alipofariki, futuhi kila aina zikaandaliwa ili kuendelea kuuaminisha umma kuwa alikuwa mtu wa watu.

Muda wote huo wafuasi wake waliamini wamefanikiwa kupandikiza hiyo imani potofu kuwa Magufuli alikuwa mtu wa watu.

Hotuba ya juzi ya mzee Makamba imewavuruga akili na sasa wanawaza watatoka vipi kwenye kadhia hii inayofuta kabisa legacy ya Magufuli. Wanaweweseka hawajui wafanye nini.
Mkuu with all due rspect, ni laima ujue kuwa Makamba alikuwa haongelei chama wala nini.

Alikuwa anaongelea tumbo lake.

Kwamaba Makamba and Co. wamesha mu overcome Mwendazaki is the bragging issue here, which was ill timed and ill meant.

Matamshi ya Makmba yana mwongezea nini mlalahoi?

Kinachokera ni kwamba watu kama Mkamba wanalichafua chama mbele ya wanachama.

Tunamkumbuka mzee Rashid Kawawa na msimamo wake wa MSHIKAMANO, ambao haujalishi mtu anatok wapi.
 
Hivi unadhani Average Joe Kitaa ataamini nini ?

Story za Makamba aliyesema ni wakati wao wa kulamba Asali au kuona wapo gizani / umeme haueleweki hence kukumbuka maneno jkuwa watu wanafanya hujuma ili kukuza biashara zao ?

Sifa za JPM hazitokani na Mazuri aliyofanya bali madudu yanayofanyika sasa..., kama vile ambavyo Uchafu wa Mrisho ulimfanya Benja aonekane msafi....
mabaya gani yanafanyika sasa ambayo hayajawahi kufanyika huko nyuma? huyo JPM mnayemuabudu aliishia kutunga sheria za kumkinga asishitakiwe? mbona kama alikuwa anapambana na rushwa hakuibadilisha ile sheria ya PCCB?
 
Hii ndio naita myopic thinking..., kwahio sababu yalifanyika nyuma ndio yaendelee kufanyika ?

Hii ni kama mtu kupigana na kivuli chako...
ESq1fmqXsAAQ7Cd.jpg
 
kunawakati nafikiria harafu nashindwa kupata majibu sahihi kwakuwa sioni tena
  • wavuvi wa samaki bali kuna wala samaki
  • watengeneza mikate ila kunawanaopewa mikate hata ikiwabidi kudhalilika
  • wanaochinja hawapo wako wanyongaji
  • vision kuna mission (tunaishi leo kesho itajiangaikia)
  • hakuna anayesema tena bora lawama kuliko fedhea
Naona waathirka wakubwa ni vijana ambao vizazi vyao vitatawaliwa na Wanyarwanda,Wakenya,Waganda,Wasomali na Wakongo pamoja na kuwa na nchi kubwa na idadi kubwa ya watu. kwa kuwa viongozi wameamua vijana wetu upeo wao uishie kwenye maisha ya kutafuta leo tu ili watawalike kirahisi na wale wenye akili kidogo wawe chawa huku wakiwategemeza watoto wao watawale milele wakiwa na lengo la kulinda udhaifu wao.

imefika wakati hatuoni sababu hata ya kutetea tamaduni zetu na tunakubaliana kwa nguvu ya chama waliokufa ni watu wabaya wakiwemo baba zao na mama zao! kweli nasi tunashangilia kwa mihemko isiyotuletea tija? kweli?

wengi tumeendelea kuishi jana na hatuko tayari tena kusema yaliyopita si ndwele tugange yajayo kwa kujenga taifa imara na lenye tija.

kibaya zaidi tumeaminishwa kuwa familia fulani ndizo zinazofaa kushika madaraka na kututawala hivyo wake zao na watoto wao sawa mhn!

mnisamehe kama nimeona vibaya lakini nchi hii ni yetu sote tunahitaji kuishi na kuitunza na kuitetea kwa nguvu zote. sidhani kama ni busara tukubali kuiuza kwa kubadilisha mlo wa leo na dhahabu.

viongozi tulionao wamekuwa watawala na wababe wamesahau wimbo wao ccm yajenga nchi sijui kama wanaweza kuuimba kwa ujasiri kama mwanzo.

hata kama hatuna uwezo wa kuwatoa madarakani kwa kuwa ndio mmeshika hatamu ya kututandikia kwa kuwa kura si kitu cha maana kwetu mnajua njaa zetu mtatupa kula ya siku moja nasi tutawapa kura ambayo mtakula kwa mkataba wa miaka mitano.

lakini kumbukeni hawa watu million 61 kundi kubwa lina maumivu ya ndani litakapolipuka hawatajali tena bunduki kwa kuwa kwa mateso wayapatayo wataamua liwalo na liwe.

muda utaamua na si kwa siku nyingi sana linakuja tena haraka!

MWENYEZI MUNGU UTUHURUMIE
 
Back
Top Bottom