Tangu nimepiga chini kazi, sasa rasmi nafurahia maisha na nimeanza kuishi kwa amani na uhuru

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Jamani kazi ni utumwa, maisha yako utayafurahia lini?

Nimekuwa mtumwa kwa miaka miwili kwa ujira kiduchu; kila kukicha kukimbizana kusaka mkate kwa imani kuwa itakuja siku nipate nafuu ya maisha, kumbe ni ubatili tu ni kama ilivyo kwa kifaranga kuamini atanyonya kesho.

Ilikuwa kila siku kulialia JF kuulizia ‘mshahara lini’ na ushauri kuhusu mbinu za kufanya kujiongezea kipato, watu wanashusha nondo unajiona kabisa fala ni wewe pekee yako tu, nikawa naumia na kujilaumu sana.

Binafsi, ni mvivu ila napenda kutumia akili kidogo sana nipate matokeo, kwa umri wangu unavyosonga nikaona kabisa bila kubadili gia angani nitakuwa najichosha tu. Basi katika kuseti mitego nikanasa dili mmoja kwa beberu hapa mjini.

Beberu huyo nikafanikiwa kumwaminisha kuwa mimi ni mtu fulani mjuaji na muhimu sana kwa dili yake, basi ikawa ameniruhusu kumpiga na kwa vile nina hasira na mabeberu basi nimempiga kweli kweli. Sasa nimejipa miaka mitano ya kukaa tu na kutumbua mavuno haya kisha nitajua tena cha kufanya panapo majaaliwa.

Kwa muda huu sitofanya shughuli yoyote ya maendeleo bali kuishi na kufurahia na familia yangu, sio kwa bata sana ila kwa maisha ya kawaida kufanya mahitaji ya msingi, huku watoto wakiendelea kusoma na kuongezeka kwa idadi kwa vile muda wa uumbaji sasa ni uhakika.

Hekaheka za kuamka mapema kukimbizana na kurudi usiku uko hoi sasa basi, kama ni utajiri nawaachia mkimbizane mimi nachagua kupumzika, na nimebadili ID’s ili niwe huru zaidi hivyo nitakuwa nawachora tu wanaodhani mi ni mgeni hapa.

Nawatakieni kazi njema, mkalijenge taifa. Hapo Kazi Tu!
 
Watanzania fanyeni kazi, hiyo ni kauli pendwa kwa awamu hii ya kishindo.... unafanya kazi unakamuliwa nguvu zako zote ukifika 60 huna kitu ndo unaachiliwa (you’re dumped) ukaanze maisha.

Pensheni yote inaishia kwenye matibabu tu.
 
Hizi story za network marketing hizi.
Hongera kwa kutusua mkuu [emoji38][emoji38]

Sijatusua mkuu, nimepunguza tu matarajio.... hebu fikiria wewe kama wewe unatumia asilimia ngapi ya kile unachopata..?
 
cmoney,

Hiyo ni hofu ya kisichojulikana, ila nikumbushe tu kuwa hayo mabalaa humpata awaye yeyote.... usile mbegu.
 
wewe jamaa wewe... kwa hiyo hapo upo unakunjana na mama yoyo wako?

Hapana mkuu ila nipo nyumbani kwa uhuru, ikitokea hata mchepuko ni muda wowote wewe upo kazini kuchepuka ni wikendi tu, ambapo pia unaweza kujikuta unahitaji kupumzika.
 
Ncha Kali,
Ukiwa mpigaji mwishowe utapigwa tuu nakuona kule kwenye mahakama ya uhujumu uchumi.
 
Kazi ndo msingi wa maendeleo

Umeaminishwa hivyo ili uwe mtumwa, ila pengine inategemea na aina ya kazi.... kwa mujibu wa ripoti ya shirika gani sikumbuki kama 84% ya Watanzania wanafanya kazi bila mkataba.

Huu si utumwa tu huu, japo tunaita kazi kwa vile hatuna namna.
 
Ukiwa mpigaji mwishowe utapigwa tuu nakuona kule kwenye mahakama ya uhujumu uchumi.

Sifanyi kitu yoyote ya uwekezaji, naishi tu kawaida na familia yangu kwa kipindi hiki.... lengo ni kupumzika kisha huko mbele tutajua cha kufanya.
 
Sifanyi kitu yoyote ya uwekezaji, naishi tu kawaida na familia yangu kwa kipindi hiki.... lengo ni kupumzika kisha huko mbele tutajua cha kufanya.
Kupumzika unakula hewa? au ndiyo wale akina"£$%^? utanisamehe kama itakuwa nimekukosea.
 
Kupumzika unakula hewa? au ndiyo wale akina"£$%^? utanisamehe kama itakuwa nimekukosea.

Umechangia bila kusoma uzi, kama umesoma hujaelewa wewe Abunwasi.... hilo tu ndo la kukusamehe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…