Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 15,335
- 29,114
Jamani kazi ni utumwa, maisha yako utayafurahia lini?
Nimekuwa mtumwa kwa miaka miwili kwa ujira kiduchu; kila kukicha kukimbizana kusaka mkate kwa imani kuwa itakuja siku nipate nafuu ya maisha, kumbe ni ubatili tu ni kama ilivyo kwa kifaranga kuamini atanyonya kesho.
Ilikuwa kila siku kulialia JF kuulizia ‘mshahara lini’ na ushauri kuhusu mbinu za kufanya kujiongezea kipato, watu wanashusha nondo unajiona kabisa fala ni wewe pekee yako tu, nikawa naumia na kujilaumu sana.
Binafsi, ni mvivu ila napenda kutumia akili kidogo sana nipate matokeo, kwa umri wangu unavyosonga nikaona kabisa bila kubadili gia angani nitakuwa najichosha tu. Basi katika kuseti mitego nikanasa dili mmoja kwa beberu hapa mjini.
Beberu huyo nikafanikiwa kumwaminisha kuwa mimi ni mtu fulani mjuaji na muhimu sana kwa dili yake, basi ikawa ameniruhusu kumpiga na kwa vile nina hasira na mabeberu basi nimempiga kweli kweli. Sasa nimejipa miaka mitano ya kukaa tu na kutumbua mavuno haya kisha nitajua tena cha kufanya panapo majaaliwa.
Kwa muda huu sitofanya shughuli yoyote ya maendeleo bali kuishi na kufurahia na familia yangu, sio kwa bata sana ila kwa maisha ya kawaida kufanya mahitaji ya msingi, huku watoto wakiendelea kusoma na kuongezeka kwa idadi kwa vile muda wa uumbaji sasa ni uhakika.
Hekaheka za kuamka mapema kukimbizana na kurudi usiku uko hoi sasa basi, kama ni utajiri nawaachia mkimbizane mimi nachagua kupumzika, na nimebadili ID’s ili niwe huru zaidi hivyo nitakuwa nawachora tu wanaodhani mi ni mgeni hapa.
Nawatakieni kazi njema, mkalijenge taifa. Hapo Kazi Tu!