Tangu tarehe 21/05/2020 nilikuwa nje ya vyombo vya habari hadi leo 05/06/2020. Mnijuze nini kilijiri

Tangu tarehe 21/05/2020 nilikuwa nje ya vyombo vya habari hadi leo 05/06/2020. Mnijuze nini kilijiri

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Halo wadau wa JF nimekuwa katika mazingira magumu sana kupata habari kuanzia tarehe 21/5 hadi Leo 05/06/2020.

Maisha haya ni mahangaiko na sikuwa na simu wala redio mahali nilikokuwepo. Wadau na familia yangu naombeni msaada wenu nini kilijiri humu nchini na duniani kisiasa, kiuchumi, michezo kijamii katika kipindi hicho chote nikiwa mafichoni au nje ya mifumo ya habari.

Nakumbuka wakati naondoka Makonda alitangaza jumapili inayofuata ni sherehe za kukata na shoka Dar.

Minijuze mengine tafadhali.

Asanteni.
 
Tata George Floyd aliuawa huko kwa Trump na kusababisha maandamano makubwa
 
Wamerekani wamewaonya raia wao wasije kutalii kwa sasa kwakua hakuna anaefahamu hatua zetu za kudhibiti coona
 
Afande Antony wa kituo cha Chalinze kakamatwa usiku akiwa anasafirisha magunia ya bange na gari binafsi
 
Yule kiboko yake "JIWE" katangaza nia ya kugombea kiti kikubwa kabisa hapa Tz.
 
Magufuli aligawa Tausi 25 kwa kila Rais mstaafu na Kwa Mama Maria Nyerere /
 
Yule mkuu Paraboa wa uswizi wana JF wamepeleleza na kugundua kuwa ni mgonga ulimbo wa manzese.
 
Marekani imekumbwa na maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa hivi karibuni kutokana na mauaji ya mtu mweusi .
 
Yanga imesaini mkataba na La liga kupitia GSM na Uzi wa Mia khalifa waendelea kuwa kwenye chati Jf kwa kuupiku Uzi wa kula tunda kimasihara .
 
Jamii forums wangekuwa na option ukiingiza tarehe unapata thread zote za hiyo tarehe. Hii ingesaidia hata mwaka 2050 member wa JF akitaka kufuatilia habari zilizochukua uzito wa juu mwaka 2020 anazipa bila wasiwasi. Hii itasaidia sana hata ukitokea uzushi labda tar 10-10-2020 eti rais Magufuli alitembea kwa miguu kutoka Lumumba hadi kwa Msuguli! Ili kubaini ukweli, unaingiza tarehe then unapata habari za mwaka huo wa 2020 katika tarehe na mwezi husika. Kuna member aliliongea hili kwa namna kama hii kama sio gudume basi chizi maarifa.
 
Back
Top Bottom