Tangu ulipoondoka mambo yamebadirika, miluzi imeongezeka

Tangu ulipoondoka mambo yamebadirika, miluzi imeongezeka

Ningependa kuona watu kama Prof.Lumumba au Prof.Kabud wakiandika kitabu cha maisha ya Magufuli, hakika kitakuwa ni moja ya vitabu bora na chenye historia muhimu sana.

Prof. Lumumba na Prof. Kabudi ni moja ya wauumini wazuri wa sera za Magufuli hivyo wanaweza kuandika kitu kwa urithi wa Tanzania ya kesho.
Nadhani Lumumba atakiandika na kitauza sana
 
Haya ndiyo mazuri ambayo "anti- Maghufulism" hawatoweza kuyafuta kwenye nuru ya ulimwengu na walimwengu, miaka kenda kenda kenda elfu mia na ushee atakapozaliwa mrithi wake.
 
Mimi nitakuwa wa mwisho kumsaliti Magufuli.

Nilijua Magufuli amefariki basi waliomchukia wataanza maisha mapya bila Magufuli, ila cha ajabu waliohai wanahofu na Magufuli na Falsafa ya Magufuli kuliko hata alivokuwa hai...

Bila shaka hofu ya Hawa watu imetokana na namna watu walivojitokeza kumzika. Magufuli na Umagufuli utaishi miaka na miaka, na Utawala wa Magufuli ndio Standard ya viongozi wajao.

Umagufuli utaishi milele
 
MAGUFULISM

Hii ni aina mpya ya Falsafa iliyoanzishwa katika Karne ya 21 haswa mwaka 2021 kutokana na falsafa za aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli aliyeishi kati ya 1959-2021. Katika Falsafa ya Magufulism tutaangazia mitizamo ya mwanafalsafa huyu katika nyanja za Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii, Kidini, Kiutamaduni, Kielimu na Kisayansi. Falsafa hii imeandikwa na kubuniwa na mwanazuoni katika Elimu ya Saikolojia ya Watoto na mbobezi katika Historia kwa Ujumla.

MAGUFULIST

Hawa ni watu wote wanaoamini , wanaoishi na kuenenda katika falsafa ya Magufulism. Magufulist siku zote wanaamini kuwa maendeleo ya Taifa ama mtu binafsi yanatokana na kulinda raslimali tulizo nazo kwa nguvu zote na Kufanya kazi kwa uadilifu bila kutegemea misaada kutoka nje.

Hapa chini tutaichanganua falsafa ya MAGUFULISM katika nyanja mbalimbali ambapo tutaangalia Dr. John Pombe Magufuli alikuwa na mitizamo na falsafa gani kuhusu mambo mbalimbali:

MAGUFULI NA UCHUMI:

Dr. John Pombe Joseph Magufuli aliamini uchumi imara hutengenezwa kwa kutumia raslimali zilizotuzunguka kwa uaminfu na uadilifu. Dr, Magufuli aliamini pia kuwa endapo kila mmoja akitimiza wajibu wake wa kufanya kazi kwa bidii na kulipa Kodi kwa uaminifu basi uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla ungeimalika sana. Dr. Magufuli alipinga uwekezaji wenye masharti ya Unyonyaji kutoka kwa mataifa ya Nje hususani katika Sekta ya Madini, Bandari nk.

MAGUFULI NA SIASA:

Katika upande wa Siasa Dr. Magufuli aliamini katika uwepo wa Vyama vya siasa vyenye mlengo wa kuleta ushindani wa hoja na sio vyama vinavyotumiwa na mataifa ya Kigeni kutaka kuvuruga amani na mshikamano wa Taifa. Dr Magufuli alividhibiti kwa nguvu kubwa vyama vilivyokuwa vikitumiwa na mataifa ya Kigeni kupenyeza agenda za mataifa ya kigeni. Katika Upande mwingine Dr. Magufuli aliamini kuwa Maendeleo hayana chama. Katika kuonyesha kuwa maendeleo hayana chama , Dr. Magufuli aliwateua viongozi wengi wa Vyama vya Upinzani katika nyadhifa tofauti tofauti katika Serikali yake.

MAGUFULI NA JAMII

Dr. John Pombe Magufuli aliamini katika ustawi wa jamii na kupinga aina zote za unyanyasaji toka kwa watu wenye madaraka na matajiri. Katika kipindi chake cha uongozi ndipo jina "WANYONGE" lilipata umaarufu. Wananchi walipoona Msafara wa Dr. Magufuli waliukimbilia na kuona mtetezi wao amefika, naye Dr. Magufuli aliwapa nafasi ya Kuwasikiliza.

*MAGUFULI NA DINI"

Dr. Magufuli aliamini kuwa tunamuamini Mungu mmoja hivyo alihimiza usawa, upendo na mshikamano kati ya watu wa madhehebu yote. Alichangisha fedha za Kujenga Misikiti katika makanisa mbalimbali, na pia pesa za kujenga Makanisa kutoka misikiti mbalimbali. Dr. John Pombe Magufuli aliamini kuwa hakuna jambo linaloshindikana mbele za Mungu. Hata katika kipindi ambacho Dunia ilikuwa ikihangaika na janga la Corona Dr Magufuli alichukua msimamo tofauti na mataifa mengine, aliwahimiza watanzania kumuomba Mungu maana yeye hashindwi na jambo lolote lile.

MAGUFULI NA MAHUSIANO YA KIMATAIFA

Dr John Pombe Magufuli aliamini katika ushirikiano usio na chembe za unyonyaji kati ya Taifa lake na mataifa ya Kigeni. Dr Magufuli allikuwa tayari kusitisha uhusiano na Taifa lolote ama taasisi yoyote yenye lengo la kufanya unyonyaji kwa Taifa lake. Kwa Lugha rahisi Dr Magufuli hakuwa muumini wa Kujipendekeza kwa Taifa tajiri ama Taasisi za Kimataifa kwani aliona kuwa watu wote ni sawa hivyo hakuna sababu ya kuwanyenyekea wanyonyaji kutoka katika mataifa ya Kigeni.

MAGUFULI NA RUSHWA/UFISADI

Dr. Magufuli alichukia Rushwa na Ufisadi kwa dhati ya moyo wake. Alikuwa tayari kuvunja urafiki na mtu yeyote aliyetetea ama kufanya vitendo vya rushwa. Katika Kipindi chake cha Uongozi neno "KUTUMBUA MAJIPU" lilimaanisha kuondoa viongozi wote wasio waadilifu na kuwachukulia hatua.

Hii ni sehemu ndogo kati ya Historia ndefu na ya kusisimua kuhusu Kiongozi na mwana falsafa huyu aliyeishi katika Karne ya 21.
Magufulism=Nazism=Fascism hizo zote lazima zipigwe vita maana ni falsafa za kishenzi zinastahili kutumika motoni tu kule kwa shetani

Nashauri hata jina Magufuli liwe na maana ya mtu muovu kabisa.

Serikali itunge sheria mtu yoyoye anayetetea au anaye-promote mambo ya magufuli au kukutwa na symbol yoyote ya magufuli afungwe au apigwe fine kama inavyofanyika kwa wafuasi wa manazi wa Hitler
 
Ahsante,Mkuu. Nakupongeza kwa iliyoyaandika.
Hapa nimejifunza misamiati mitatu sasa.
Magufulism, Magufulist na Magufulification.
Viva Magufuli.
 
Magufulism=Nazism=Fascism hizo zote lazima zipigwe vita maana ni falsafa za kishenzi zinastahili kutumika motoni tu kule kwa shetani

Nashauri hata jina Magufuli liwe na maana ya mtu muovu kabisa.

Serikali itunge sheria mtu yoyoye anayetetea au anaye-promote mambo ya magufuli au kukutwa na symbol yoyote ya magufuli afungwe au apigwe fine kama inavyofanyika kwa wafuasi wa manazi wa Hitler
Hahaha, Unaota...
 
Mimi nitakuwa wa mwisho kumsaliti Magufuli.

Nilijua Magufuli amefariki basi waliomchukia wataanza maisha mapya bila Magufuli, ila cha ajabu waliohai wanahofu na Magufuli na Falsafa ya Magufuli kuliko hata alivokuwa hai...

Bila shaka hofu ya Hawa watu imetokana na namna watu walivojitokeza kumzika. Magufuli na Umagufuli utaishi miaka na miaka, na Utawala wa Magufuli ndio Standard ya viongozi wajao.

Umagufuli utaishi milele
Ndugu yangu, Umagufuli umeota mioyoni mwa watu. Si rahisi kuupoteza Umagufuli hata kidogo.
 
Magufulism=Nazism=Fascism hizo zote lazima zipigwe vita maana ni falsafa za kishenzi zinastahili kutumika motoni tu kule kwa shetani

Nashauri hata jina Magufuli liwe na maana ya mtu muovu kabisa.

Serikali itunge sheria mtu yoyoye anayetetea au anaye-promote mambo ya magufuli au kukutwa na symbol yoyote ya magufuli afungwe au apigwe fine kama inavyofanyika kwa wafuasi wa manazi wa Hitler
Kwa nini Mnamuogopa Magufuli wakati amekwisha fariki.

Magufuli alikufa mwili tu, ila ataaishi Milele
 
Magufulism=Nazism=Fascism hizo zote lazima zipigwe vita maana ni falsafa za kishenzi zinastahili kutumika motoni tu kule kwa shetani

Nashauri hata jina Magufuli liwe na maana ya mtu muovu kabisa.

Serikali itunge sheria mtu yoyoye anayetetea au anaye-promote mambo ya magufuli au kukutwa na symbol yoyote ya magufuli afungwe au apigwe fine kama inavyofanyika kwa wafuasi wa manazi wa Hitler
sasa hii ndio itakua title ya project yako mkuu, nenda ukazicompere.
 
Back
Top Bottom