Tani 40,050 za korosho zaenda nje

Tani 40,050 za korosho zaenda nje

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
1570083207081.png

SERIKALI imeridhishwa na uwezo wa viwanda vya ndani katika kuongeza thamani ya korosho ya Tanzania, huku mpaka sasa tani 40,050 zimeshapakiwa kwenye meli tayari kwenda nje ya nchi kupitia Bandari ya Mtwara. Aidha, hadi kufikia Septemba 23, mwaka huu, tani 607.75 za korosho zilibanguliwa na viwanda vidogo na kuwezesha wabanguaji wadogo 1,000 kupata ajira, huku tani 3,309.64 zilibanguliwa na viwanda vikubwa na kuwezesha kutoa ajira 2,511 ambapo waajiriwa wengi ni wanawake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa vyombo vya habari jana, ubanguaji wa korosho hizo ulifanywa na viwanda vya aina mbili yaani viwanda vidogo vinavyosimamiwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) pamoja na viwanda vikubwa.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Joseph Buchweishaija alisema ubanguaji huo unafanyika katika viwanda vilivyopo mikoa ya Mtwara na Lindi na usafirishaji wa korosho hizo nje ya nchi unaendelea Bandari ya Mtwara. Profesa Buchweishaija alisema hadi kufikia Septemba 23, mwaka huu, tani 607.75 za korosho zilibanguliwa na viwanda vidogo na kuwezesha wabanguaji wadogo 1,000 kupata ajira huku tani 3,309.64 zilibangu liwa na viwanda vikubwa na kuwezesha kutoa ajira 2,511 ambapo waajiriwa wengi ni wanawake.

Alisema katika kutekeleza mpango wa ubanguaji, serikali kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) iliingia mikataba na viwanda vikubwa na SIDO kwa niaba ya viwanda au wabanguaji wadogo ili kubangua korosho hizo. Alivitaja viwanda hivyo vidogo katika Mkoa wa Mtwara kuwa ni Siwa Food Products, Mama Vitu Super Cashewnut, Mikindani Food Processing, Akross Ltd - SIDO, Mtwara na Kitama Farmers-Tandahimba na kwa Mkoa wa Lindi ni Waigero Ltd, Wabanguaji Wadogo BUCO na Uwakoru, Ruangwa.

Alisema mpaka sasa viwanda vitano vilivyo chini ya usimamizi wa SIDO Mtwara, vimekamilisha ubanguaji wa korosho na viwanda viwili ambavyo ni Waigero na Uwakoru chini ya usimamizi wa SIDO Lindi, vinaendelea na uzalishaji na ubanguaji. Mbali na viwanda hivyo vidogo, viwanda vingine ni Amama Farmers, Perfect Cashew, Hawte Investment Ltd na Al-Andalus Ltd ambavyo vinaendelea na ubanguaji wa kati, wakati Kiwanda cha Micronix na Korosho Afrika vimemaliza ubanguaji wa korosho ghafi kama makubaliano ya mikataba yao na kwa sasa viwanda hivyo, vinaendelea kubangua korosho walizouziwa na serikali tani 1,000.

Kuhusu usafirishaji wa korosho kutoka kwenye maghala kwenda melini, alisema kazi hiyo inaendelea vizuri na mpaka sasa tani 40,050 zimeshapakiwa kwenye meli tayari kwenda nje ya nchi kupitia Bandari ya Mtwara. “Hivi sasa ninavyozungumza tayari meli mbili zimepakia korosho na kuondoka, meli ya tatu imeanza kupakiwa ambapo itabeba kontena 1,015 ambazo sawa na tani 23,328 na kazi hii itakamilika kwa siku mbili ikizingatiwa kuwa kuna meli zingine mbili zipo majini na zitatia nanga na kuanza kazi ya kupakia korosho kwenda nje ya nchi,” alisema.

Majaliwa atembelea bandari Mtwara Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea bandari ya Mtwara na ameshuhudia shehena ya korosho ziliyonunuliwa na Kampuni ya Tang Long zikipakiwa katika meli kubwa yenye jina la AS Christiana kwa ajili kusafirishwa kwenda nchini Vietnam. “Ni faraja kuona mzigo wa korosho ukiondoka na kutoa nafasi ya kuingiza mzigo mwingine mpya wa korosho utakaopatikana baada ya kuanza msimu mpya mwezi huu.

Na mnunuzi huyu ameahidi kununua tani 100,000 katika msimu wa mwaka huu,” alisema Majaliwa. Alitembelea Bandari ya Mtwara jana kwa ajili ya kujionea kazi ya usafirishaji wa korosho inavyofanyika na alisema ameridhishwa na kasi na utaratibu unaoendelea badarini hapo.

Alisema Kampuni ya Tang Long ya Vietnam licha ya kuahidi kununua korosho katika msimu wa mwaka huu, pia imeomba kupatiwa eneo kujenga kiwanda cha kubangua korosho na wapo tayari kuanza hata Desemba, 2019.

Waziri Mkuu alisema ujenzi wa viwanda vya kubangulia korosho nchini, utaongeza thamani na kuwezesha dunia nzima kutambua kuwa korosho hizo zimetoka Tanzania, kwa sababu kwenye vifungashio watakuwa wameandika, hivyo kuongeza soko.

Akizungumzia kuhusu msimu wa uuzaji wa korosho wa mwaka huu, Waziri Mkuu alisema kipaumbele cha kwanza watapewa wenye viwanda vya ndani na kisha tani zinazobaki zitauzwa kwa wanunuzi kutoka nje. “Wito wa Rais Dk. John Magufuli wa ujenzi wa viwanda unalenga katika kuongeza ajira kwa wananchi kwa kuwa viwanda vinaajiri watu wengi wenye kada tofauti. Wakuu wa mikoa endeleeni kurahisisha mazingira ya uwekezaji,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe alisema licha ya kampuni ya Tang Long kununua korosho nchini, pia imeomba ikodishwe kiwanda kimojawapo cha serikali ili waanze ubanguaji wa korosho.
 
Naomba kukiri na kutambua kazi kubwa ilofanywa na Wizara ya KILIMO na Wizara ya Biashara kufanikisha mauzo ya korosho na sasa, zinasafiri kwenda ughaibuni kubanguliwa, kusindikwa na kuuzwa kama final consumable products.

My reality check, sijasikia au kuona strategic plan ya nini tutafanya mbele ili kutimiza nia njema ya Rais ambayo inatakiwa kuakisi sehemu ya hotuba yake wakati wa SADC.

Kwa kifupi sana, ali-analyze vizuri kuwa, AFRICA tunazalisha raw materials ikiwemo korosho.
Tunapouza mazao ghafi tunapeleka ajira za viwanda nje badala ya kuwa na hizo kazi zikafanywa na vijana. Tunapouza ghafi tunapangiwa bei.

Natamani kusikia kauli ya kimkakati, ifikapo mwaka 20... Tanzania inatakiwa kuzalisha finished products za Korosho ili kazi, umeme wa viwanda, maji wka ajili ya viwanda, vifungashio iwe ni made in Tanzania.

Natumai, wakuu wa vitengo na wizara husika mta-escalate ili jambo hili litokee
 
Kwahiyo mmexport ajira ya watanzania na kuwapelekea mabeberu? Hivi hatuna wawekezaji wazalendo wakafungua kiwanda nchini?
 
Hii ni aibu kuendelea kuuza malighafi nje ya nchi badala ya kuzichakata nchini tukatengeneza ajili na kuuza bidhaa nje!
 
View attachment 1222324

SERIKALI imeridhishwa na uwezo wa viwanda vya ndani katika kuongeza thamani ya korosho ya Tanzania, huku mpaka sasa tani 40,050 zimeshapakiwa kwenye meli tayari kwenda nje ya nchi kupitia Bandari ya Mtwara. Aidha, hadi kufikia Septemba 23, mwaka huu, tani 607.75 za korosho zilibanguliwa na viwanda vidogo na kuwezesha wabanguaji wadogo 1,000 kupata ajira, huku tani 3,309.64 zilibanguliwa na viwanda vikubwa na kuwezesha kutoa ajira 2,511 ambapo waajiriwa wengi ni wanawake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa vyombo vya habari jana, ubanguaji wa korosho hizo ulifanywa na viwanda vya aina mbili yaani viwanda vidogo vinavyosimamiwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) pamoja na viwanda vikubwa.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Joseph Buchweishaija alisema ubanguaji huo unafanyika katika viwanda vilivyopo mikoa ya Mtwara na Lindi na usafirishaji wa korosho hizo nje ya nchi unaendelea Bandari ya Mtwara. Profesa Buchweishaija alisema hadi kufikia Septemba 23, mwaka huu, tani 607.75 za korosho zilibanguliwa na viwanda vidogo na kuwezesha wabanguaji wadogo 1,000 kupata ajira huku tani 3,309.64 zilibangu liwa na viwanda vikubwa na kuwezesha kutoa ajira 2,511 ambapo waajiriwa wengi ni wanawake.

Alisema katika kutekeleza mpango wa ubanguaji, serikali kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) iliingia mikataba na viwanda vikubwa na SIDO kwa niaba ya viwanda au wabanguaji wadogo ili kubangua korosho hizo. Alivitaja viwanda hivyo vidogo katika Mkoa wa Mtwara kuwa ni Siwa Food Products, Mama Vitu Super Cashewnut, Mikindani Food Processing, Akross Ltd - SIDO, Mtwara na Kitama Farmers-Tandahimba na kwa Mkoa wa Lindi ni Waigero Ltd, Wabanguaji Wadogo BUCO na Uwakoru, Ruangwa.

Alisema mpaka sasa viwanda vitano vilivyo chini ya usimamizi wa SIDO Mtwara, vimekamilisha ubanguaji wa korosho na viwanda viwili ambavyo ni Waigero na Uwakoru chini ya usimamizi wa SIDO Lindi, vinaendelea na uzalishaji na ubanguaji. Mbali na viwanda hivyo vidogo, viwanda vingine ni Amama Farmers, Perfect Cashew, Hawte Investment Ltd na Al-Andalus Ltd ambavyo vinaendelea na ubanguaji wa kati, wakati Kiwanda cha Micronix na Korosho Afrika vimemaliza ubanguaji wa korosho ghafi kama makubaliano ya mikataba yao na kwa sasa viwanda hivyo, vinaendelea kubangua korosho walizouziwa na serikali tani 1,000.

Kuhusu usafirishaji wa korosho kutoka kwenye maghala kwenda melini, alisema kazi hiyo inaendelea vizuri na mpaka sasa tani 40,050 zimeshapakiwa kwenye meli tayari kwenda nje ya nchi kupitia Bandari ya Mtwara. “Hivi sasa ninavyozungumza tayari meli mbili zimepakia korosho na kuondoka, meli ya tatu imeanza kupakiwa ambapo itabeba kontena 1,015 ambazo sawa na tani 23,328 na kazi hii itakamilika kwa siku mbili ikizingatiwa kuwa kuna meli zingine mbili zipo majini na zitatia nanga na kuanza kazi ya kupakia korosho kwenda nje ya nchi,” alisema.

Majaliwa atembelea bandari Mtwara Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea bandari ya Mtwara na ameshuhudia shehena ya korosho ziliyonunuliwa na Kampuni ya Tang Long zikipakiwa katika meli kubwa yenye jina la AS Christiana kwa ajili kusafirishwa kwenda nchini Vietnam. “Ni faraja kuona mzigo wa korosho ukiondoka na kutoa nafasi ya kuingiza mzigo mwingine mpya wa korosho utakaopatikana baada ya kuanza msimu mpya mwezi huu.

Na mnunuzi huyu ameahidi kununua tani 100,000 katika msimu wa mwaka huu,” alisema Majaliwa. Alitembelea Bandari ya Mtwara jana kwa ajili ya kujionea kazi ya usafirishaji wa korosho inavyofanyika na alisema ameridhishwa na kasi na utaratibu unaoendelea badarini hapo.

Alisema Kampuni ya Tang Long ya Vietnam licha ya kuahidi kununua korosho katika msimu wa mwaka huu, pia imeomba kupatiwa eneo kujenga kiwanda cha kubangua korosho na wapo tayari kuanza hata Desemba, 2019.

Waziri Mkuu alisema ujenzi wa viwanda vya kubangulia korosho nchini, utaongeza thamani na kuwezesha dunia nzima kutambua kuwa korosho hizo zimetoka Tanzania, kwa sababu kwenye vifungashio watakuwa wameandika, hivyo kuongeza soko.

Akizungumzia kuhusu msimu wa uuzaji wa korosho wa mwaka huu, Waziri Mkuu alisema kipaumbele cha kwanza watapewa wenye viwanda vya ndani na kisha tani zinazobaki zitauzwa kwa wanunuzi kutoka nje. “Wito wa Rais Dk. John Magufuli wa ujenzi wa viwanda unalenga katika kuongeza ajira kwa wananchi kwa kuwa viwanda vinaajiri watu wengi wenye kada tofauti. Wakuu wa mikoa endeleeni kurahisisha mazingira ya uwekezaji,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe alisema licha ya kampuni ya Tang Long kununua korosho nchini, pia imeomba ikodishwe kiwanda kimojawapo cha serikali ili waanze ubanguaji wa korosho.
Tatizo Jiwe hakomi kukurupuka. Kaharibu saana hii Issue.
Alikuwa anakataza kwenda Nje haya anaruhusu kwanini sasa? Kiongozi gani hana hata Tafakuri juu ya Maamzi yake?
 
Tani ngapi zilizooza hadi sasa?bado bilioni ngapi ambazo zinadaiwa na wakulima wa korosho?
Tuanzie hapo kwanza[emoji2211]
 
Doa la korosho halisafishiki nyie mazumbukuku....
 
Kwahiyo mmexport ajira ya watanzania na kuwapelekea mabeberu? Hivi hatuna wawekezaji wazalendo wakafungua kiwanda nchini?
Inasikitisha sana, maana wengi wanasubiri JPM awaelekeze nini cha kufanya. Sio sawa kumtwisha Rais kila kitu.
Wizara ya Biashara, Uwekezaji na Fedha walitakiwa kuja na strategic industrial solution ambayo inatakiwa ifanyike ili in the next 2 years tuwe na viwanda hapa.
Hao Vietnamise wanaonunua, wameanza ubanguaji kwenye mid '80.

Before execution, in-depth thinking matters. Guys hii nchi ni yetu na watu wa public sector, kuweni na open mind ya ku-embrace brains za Watanzania walio nje ya public ili tu-maximize mauzya korosho na sio korosho ghafi
 
Tatizo Jiwe hakomi kukurupuka. Kaharibu saana hii Issue.
Alikuwa anakataza kwenda Nje haya anaruhusu kwanini sasa? Kiongozi gani hana hata Tafakuri juu ya Maamzi yake?
Kiongozi lazima awe decisive kutetea watu wake.
Bora alikuja na initiative ya kununua korosho wa sh.3,300 badala ya 1500 ambayo walitaka kununua waranguzi.
So far, wanunuzi wamepatikana kwenda kuzibangua bila mkulima kupunjwa.
Japo ni lazima twende kwenye kuzalisha end product hapa kwa kuongeza ajira, kupanua tax base na ku=maximize forex earnings.
 
Hii ni aibu kuendelea kuuza malighafi nje ya nchi badala ya kuzichakata nchini tukatengeneza ajili na kuuza bidhaa nje!
Sure, ila nchi nyingi za africa hatuna uwezo wa kuproduce high quality manufactured goods ambazo zinauwezo wa kushindana katika soko la dunia. Ndio maana tuna export sana malighafi kuliko bidhaa za kiwandani ndio maana tunahitaji uchumi wa viwanda ili kuproduce high quality manufactured goods.
 
Hiyo ya katika kati mbona ina sura ya mzee mkuu?
Screenshot_2019-10-03-14-59-35.jpeg
 
za mwaka jana mlizosema tuzigawane kwa lazima zipo wapi?
 
Sure, ila nchi nyingi za africa hatuna uwezo wa kuproduce high quality manufactured goods ambazo zinauwezo wa kushindana katika soko la dunia. Ndio maana tuna export sana malighafi kuliko bidhaa za kiwandani ndio maana tunahitaji uchumi wa viwanda ili kuproduce high quality manufactured goods.
Sio kwamba hatuna uwezo. Ila hatujaamua kutafuta huo uwezo ambao ni technology inayouzwa ili kutoa ubora unaokidhi viwango vya walaji sokoni.

Pale EPZA Dar; kuna plant inatengeneza jeans za kukidhi soko la USA. Plant ile ni machinery/technology ambayo inauzwa kutoa final product for USA market.

Hery Ford alisema if you think you can or you can't - you're right.

The good bread for changes/transformation DNA yake ni depth/shallow thinking pattern.
 
Tunawapongeza wizara ya biashara na viwanda kwa kazi iyo mlioifanya japo tumesafitisha raw material kwenda nje badala ya finished product ambazo zingekuwa na tija kwa uchumi wetu, lkn mwanzo mgumu,
Kongolee
 
Kwa maoni yangu kuna viti vya msingi sana kuangalia kwa nini tunasafirisha malighafi.

Nitaanza kwa kutoa mfano rahisi sana kwa kitu tunachotumia wote kila siku.

Natumai wote au wengi wetu tunakula kuku wa kukaanga aina ya broiler na viazi vya kukaaanga almaarufu chipsy, hata hivyo ukiangalia bidhaa hizo hizo kuna kampuni mbili tuu kubea duniani zinazoongoza kwa mauzo ya kuku na chipsi duniani yaan MACDONALDS na KFC, kwanini

Katika biashara yoyote kuna kitu kinaitwa brand, hii ndo msingi wa kumuwezesha mteja kuwa na imani ya bidhaa anayoinunua kwani ana uhakika na mahali ilipotokea na historia ya brand husika.

Tambueni kwamba, nchi inayoongiza kwa kununua korosho ghafi duniani ni ındia, lakini pia ındia sio walaji wa mwisho wa korosho na mazao mengi tuu tunayosafirish nje, makampuni mengi yenye brand kubwa yamewekeza ındia ikiwa ni kama hub ya kusindika mazao haya kwa ajili ya final consumers duniani pote, binafsi nimewahi kula korosho zilizokuwa processed india na nilizikuta kwenye ndege ya Kenya Airways ladha yake ni tofauti kabisaaa.

Hivyo Supermarkets nyingi duniani zinatambua aina ya brands ambazo pia ni maarufu kutoka India, china, Vietnum nk.

Sasa swali, mazingira ya sasa ya kubangua korosho ikiwa ni pamoja na packaging ni rafiki?

Kuna suala jingine pia la muendelezo wa mazao, kumbukeni Tanzania sio nchi pekee inayozalisha Korosho, msimu wa Korosho Tanzania ni mfupi mno, bodi zinazosimamia mazao pia zipo tofauti tofauti mfano bodi inayosimamia Korosho ni Tofauti na inayosimamia Ufuta, pamoja na mazao mengine, kinachotokea ni kwamba mwekezaji anatakiwa afungue kiwanda halafu kifanye kazi miezi 3hadi 4 korosho hakuna.

Ukiangalia viwanda vinavyosindika mazao Nchi nilizotaja hapo juu, vina option ya kusindika mazao yote na hivyo kuwa na mzunguko wa mazao mwaka mzima.

Hivyo Wizara zinazosimamia Kilimo na Wizara zinazosimamia viwanda na biashara lazima zirudi kwenye drawing table kama tuna nia ya kufanya mazao haya yawe yenye tija.
 
Umetoa mfano mzuri sana wa KFC na Macdonald;
What we could kwenye Korosho ni franchise brand kubwa kama hizi hapa

Amazon product ASIN B0077ROISE
Amazon product ASIN B015VOTNLG

Wao wanatupa specifications za kubangua; kuzi-roast, kiwango cha chumvi au sukuri.
Na brand packaging ubora wake kama za huko kwao.
Zikienda sokoni tunauza na wao wanavita commission.
This is the rule of the game and every one wins.
We get more forex, we create jobs, we increase tax base.

I wish waziri Bashungwa apigane kwenye kufanikisha mambo haya yatokee
 
Back
Top Bottom