Tani 68,902 za Bangi zilikamatwa Tanzania kuanzia Mwaka 2015 hadi 2020

Tani 68,902 za Bangi zilikamatwa Tanzania kuanzia Mwaka 2015 hadi 2020

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483
Tatizo la matumizi na biashara ya dawa za kulevya limeendelea kuiathiri nchi yetu. Bangi imeendelea kuwa ni dawa ya kulevya inayotumika zaidi na ikizalishwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara hususani katika mikoa ya Mara, Morogoro, Arusha, Tanga, Mbeya, Kagera, Ruvuma, Iringa na Njombe.

Bangi.png

Vilevile, Mirungi imeendelea kutumika na kuzalishwa hapa nchini hasa katika Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Same na kiasi kingine cha dawa hii kimekuwa kikiingizwa nchini kutoka nchi jirani ya Kenya.

Nchi yetu Tanzania imekuwa ni njia kuu ya kupitishia na kusambaza dawa za kulevya za viwandani hususan heroin na cocaine kwenda Ulaya, China, Afrika Magharibi na Afrika Kusini na kiasi kingine kubaki na kutumika hapa nchini.

Kiasi kikubwa cha Heroin inayoingizwa nchini hutokea nchi za Afghanistan, Pakistan na Iran wakati kiasi kikubwa cha cocaine hutoka nchi za Amerika ya Kusini hasa Colombia, Peru na Bolivia.

Tatizo la matumizi ya dawa za kulevya limeendelea kuathiri sekta mbalimbali za uzalishaji na hivyo kudhoofisha ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Matumizi hayo yamekuwa yakiathiri afya za watanzania hasa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa letu.

Kwakuwa Bangi za kulevya hasa bangi ndo imekuwa inatumika sana Tanzania, Kwa leo nitawaletea Takwimu za Bangi iliyokamatwa kuanzia Mwaka 2015 hadi mwaka 2020 kwa Tani.

Mwaka 2015 tani 22.01 za Bangi zilikamatwa 23 na idadi ya watuhumiwa waliokamatwa wakijihusisha na bangi ni 13,275

Takwimu zinaonesha kwamba kiasi cha bangi kilichokamatwa mwaka 2016 ni tani 68.23 na idadi ya watuhumiwa waliokamatwa wakijihusisha na bangi ni 17,889

Kwa Mwaka 2017 Kiasi cha tani 52.19 za bangi zilikamatwa na idadi ya watuhumiwa waliokamatwa wakijihusisha na bangi ni 11,528

Mwaka 2018 tani 23.61 za bangi zilikamatwa, pia watuhumiwa 9,744 waliohusishwa na biashara ya dawa hiyo mwaka 2018 Walikamatwa.

Biashara ya bangi iliendelea kufanyika kwa mwaka 2019 na kukamatwa kwa tani 21.16 za dawa hiyo, idadi ya watuhumiwa waliojihusisha na biashara ya bangi mwaka 2019 ilikuwa 8,865

Mwaka 2020 Kiasi cha tani 13.23 za bangi zilikamatwa na kuhusisha jumla ya watuhumiwa 7,601. Ni kiasi kidogo ukilinganisha na Miaka mingine kuanzia 2015.

mbili.jpg
moja.jpg

Mwenendo wa Kiasi cha Bangi kilichokamatwa nchini kati ya Mwaka 2015-2020
 
Kwa mujibu wa mtandao wa Statista, wanasema bei ya bangi gramu moja ni kuanzia dollar 14 hadi 8 katika miji mbalimbali Marekani (kwa wastani ni dollar 10 kwa gramu).

Screenshot_20220307-150607.png


Sasa kwa mzigo huo wa Tani 68,000 kwa miaka mitano ni pesa karibia Dola za Kimarekani 680,000,000,000 hivi. Just imagine.
 
Zihararishwe tu ili tutumie kwa uhuru

Free People in free Nation
 
Kwa mujibu wa mtandao wa Statista, wanasema bei ya bangi gramu moja ni kuanzia dollar 14 hadi 8 katika miji mbalimbali Marekani (kwa wastani ni dollar 10 kwa gramu).

View attachment 2142116

Sasa kwa mzigo huo wa Tani 68,000 kwa miaka mitano ni pesa karibia Dola za Kimarekani 680,000,000,000 hivi. Just imagine.
Hiyo uloandika ndo bei gani? Iseme kwa maneno.
 
Iacheni hiii mimea ni baraka kutoka kwa Mungu mnaita dawa za kulevya mimea(majani) aibu kwa viongozi mnapitisha sheria kali kisa mimea baraka alizotupa Mungu aibu nchi za Africa viongozi wengi akili zao zipo matakoni aibu.
 
Back
Top Bottom