DOKEZO TANROADS Engineering Consulting Unit (TECU) inahitaji reforms. Ufanisi wa kazi hakuna na Watendaji tunadai malimbikizo ya mpaka miezi 10

DOKEZO TANROADS Engineering Consulting Unit (TECU) inahitaji reforms. Ufanisi wa kazi hakuna na Watendaji tunadai malimbikizo ya mpaka miezi 10

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
TECU imekuwa kichaka cha mameneja wa Mikoa na baadhi ya watu kutoka TANROADS HQ kujinufaisha, wamekuwa wakiweka figisu miradi mingi isimamiwe na TECU ili waendelee kupata fedha bila kazi.

Private Consultants wanakosa kazi na TECU (ukiachana na walioajiriwa kwa mikataba) wale inhouse wanawekwa kwa kujuana. Pili, kunakuwa na conflict of interest maana mameneja wa Mikoa ndo MaPM so wanakuwa upande wa Employer wakati huo huo Consultant hivyo wanakuwa wanatumia vibaya rasilimali za miradi kwa matumizi yasiyokusudiwa.

Ili TECU ifanye kazi kwa ufanisi kwanza inatakiwa ijitegemee kama ilivyo REA na TANESCO na watu wote wanaoajiriwa na TECU waajiriwe from TECU HQ na siyo kwa mameneja wa Mikoa wa TANROADS. Hii itaboresha ufanisi na kuondoa malalamiko mfano malipo ya mishahara na allowance yawe yanalipwa kwa wakati mmoja na makato kwenye site/responsibility allowance (kimsingi hayapaswi kukatwa) yafanane maana sasa hivi kuna mikoa mingine hawakatwi mikoa mingine wanakatwa 10% mingine 20% na mingine 30%.

Tatizo la mikoa mingine kutolipwa kwa wakati ilihali mikoa mingine wanalipwa kwa wakati litaisha.

Changamoto za watumishi ziwe na single channel kwenye TECU HQ badala ya ilivyo sasa kila Mkoa wana maelekezo yao.

Chief Engineer wa TECU Eng. Lutengano Mwandambo kwa sasa yupo kama pambo tu maana hana responsibility yoyote kwa watumishi wa TECU na sijui kama anajua changamoto za wafanyakazi wa TECU maana mameneja wa TANROADS mikoa ndo wanaamua kila kitu kwenye miradi.

Wakati TECU inakuwa assigned kusimamia miradi iwe na mkataba plus budget maana hivi sasa wanapewa kusimamia na hakuna bajeti hivyo kila meneja wa mkoa anaanza kupambana namna gani apate fedha ya kulipa. Hii inatia hofu kwani mtu anakuwa anadai kwa zaidi ya miezi 10 na ni kazi ya mkataba hivyo kuna wasiwasi mkataba utaisha huku watu wanadai je, watalipwa je? Na wakati mwingine meneja anayekuwepo mwanzo akihamishwa akaja mwingine anaanza kusema madeni ya nyuma hayatambui.

Mameneja na MaPE kutoka HQ wanalipwa allowance za site kila mwezi hata wasipokuja kwa miezi lukuki hivyo kunakuwa na double payments na sijui Internal Auditors wa TANROADS wanafanya kazi gani!

TANROADS na TECU ni uozo mtupu.
 
Tanaroad imekufa hata pesa za kulipa Wakandarasi hawana
 
Back
Top Bottom