KERO TANROADS fanyieni ukarabati Musoma Road imechoka sana hasa kipande cha Mwanza mpaka Nyashimo

KERO TANROADS fanyieni ukarabati Musoma Road imechoka sana hasa kipande cha Mwanza mpaka Nyashimo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2021
Posts
280
Reaction score
173
Barabara hii imechoka sana hasa kipande cha Mwanza mpaka Nyashimo, lakini cha kushangaza TANROADS wanaitazama tu kila kukicha, barabara imejaa mashimo kila sehemu; sio katikati, sio kulia wala kushoto, ni mashimo kila upande.

Kuna baadhi ya vipande (kabla na baada ya Daraja la Simiyu) inabidi magari yatumie upande mmoja tu wa barabara ili kukwepa mashimo. Hii ni hatari sana kwa usalama wa abiria na magari pia.

Musoma Road ni barabara muhimu sana inayounganisha mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani ya Kenya na kwa kiasi kikubwa inachangia katika uchumi. Sasa kwa nini mmeitelekeza namna hiyo?

NB: Picha hizi zimepigwa kutokea ndani ya gari na wakati gari ikitembea.
IMG_20250425_174020.jpg
IMG_20250425_173253.jpg
IMG_20250425_173239.jpg
IMG_20250425_173141.jpg
IMG_20250425_172952.jpg
IMG_20250425_172950.jpg
IMG_20250425_172948.jpg
IMG_20250425_172824.jpg
IMG_20250425_172822.jpg
 
Issue ya barabara Mwanza ni kipengele sana. Hili jiji linajengwa majengo tu lakini barababara kuu zipo hoi
 
Back
Top Bottom