TANROADS imesaini mkataba wa Ujenzi wa Daraja la Simiyu lenye urefu wa mita 150 na barabara za Maingiliano zenye urefu wa km 3 kwa kiwango cha lami

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia TANROADS imesaini mkataba wa Ujenzi wa Daraja la Simiyu lenye urefu wa mita 150 na barabara za Maingiliano zenye urefu wa km 3 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi bilioni 48.788.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya utiaji saini mkataba huo iliyofanyika leo tarehe 06 Julai 2023 Makao Makuu ya TANROADS Jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Mohamed Besta amesema Ujenzi wa mradi huo ni moja ya mikakati ya Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuboresha miundombinu ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji Nchini.

Amesema "daraja lilipo kwa sasa ni jembama na linakadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 70, lina urefu wa mita 140, ni daraja la chuma ambazo zimebebwa na nguzo za zege, kutokana na uwepo wa njia moja tu magari yanasubiriana ili kuvuka, daraja limezeeka na limekuwa likikarabatiwa mara kwa mara kwa kubadilisha chuma kila mwaka ili kuliwezesha kupitisha magari jambo ambalo limekuwa changamoto kwa usalama wa watumiaji na limekuwa likitumia gharama kubwa sana kwa matengenezo hivyo kuigharimu Serikali kiasi kikubwa cha fedha".

Ameeleza kwa kutambua umuhimu wa daraja hilo ambalo linaunganisha Jiji la Mwanza na sehemu za Mashariki na Kaskazini mwa Tanzania pamoja na Nchi Jirani za Kenya, Serikali imetenga fedha kwa ajili ya Ujenzi wa daraja jipya ili kupunguza gharama kubwa ya matengenezo, kuongeza usalama na ufanisi pamoja na kuondoa usumbufu kwa watumiaji ili kuchochea shughuli za kiuchumi.\n\n"Natoa shukrani za dhati kwa Serikali yetu kwa kutoa fedha za Ujenzi wa mradi huu, TANROADS itasimamia kikamilifu utekelezaji wake na kuhakikisha Mkandarasi anazingatia viwango vya kiufundi na mradi unakamilika kwa wakati, nitoe wito kwa Mkandarasi kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu ili kazi zikamilike ndani ya muda uliopangwa kwa viwango na gharama zinazokubalika'' amesisitiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta.

 
Kwahiyo unashauri vp shughuli za naendeleo zisifanyike?!!!!!
mkuu kwani tumeombwa ushauri!
barabara yenyewe maeneo wanapotaka kujenga daraja ni ya hovyo, wangeanza nayo kwanza hadi lamadi ikae sawa
na kurudi kuja mwanza pia
 
mkuu kwani tumeombwa ushauri!
barabara yenyewe maeneo wanapotaka kujenga daraja ni ya hovyo, wangeanza nayo kwanza hadi lamadi ikae sawa
na kurudi kuja mwanza pia
we inaonekana umekata hata tamaa ya kuishi. Sijawahi ona mtu wa hovyo km wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…