Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mara, Eng. Vedastus Maribe, amemuomba Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, kusaidia kushinikiza Serikali kuu ili kuhakikisha barabara muhimu za mkoa huo zinajengwa kwa kiwango cha lami.
Maribe ameyasema hayo wakati wa ziara ya Wasira mkoani Mara, ambapo alitaka kufahamu maendeleo ya ujenzi wa barabara mbalimbali, ikiwemo barabara ya Mika-Kirongwe, ambayo ujenzi wake umekuwa ukifanyika kwa hatua ndogo ndogo.
Akijibu maombi hayo, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema atalifikisha suala hilo kwa mamlaka husika, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na Waziri wa Ujenzi ili kuhakikisha barabara hizo zinakamilika.
Amesema ujenzi wa barabara hizo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, ambayo inalenga kuboresha miundombinu ya usafiri na kukuza uchumi wa mkoa wa Mara.