Nimesoma moja ya post humu kwamba kwa mujibu wa CAG, Tanroads walikuwa na bakaa kwenye bajeti yao. Nimesikitika sana kwa kweli. Hali ilivyo mbaya sana tena sana kwenye jimbo la kibamba kwa barabara zilizopo chini ya Tanroads, alafu inapatikana hela ya kurudi serikalini? Hii si ni dharau kweli?
Kuna barabara mbovu sijawahi kuona, kutokea mpigi magoe to mbezi kupigia barabara ya msumi na ile ya mbezi high school hizi barabara hazitamaniki kabisa. Watu wanateseka sana kwa kukosa usafiri, dalala zimehamisha ruti zao.
Hivi kweli Tanroads hawapo humu JF? Kwamba hawatusikii wananchi tunavyopata shida? Au mpaka aishi huku mkubwa flani ndo mtajenga?
Ikifika muda wa kuweka hata kifusi hakiwekwi, kinachofanyika ni kuparua parua kwa juu, baada ya siku mbili mahandaki yanaanza upya.
Tanroads mnatutesa wananchi.