Tanroads Tanga wanatumia rangi nyeupe hafifu zinazofutika muda mfupi kuchora alama kwenye lami

Tanroads Tanga wanatumia rangi nyeupe hafifu zinazofutika muda mfupi kuchora alama kwenye lami

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,273
Reaction score
13,567
Habari za leo?

Kuna watu/kampuni wamepewa kazi ya kuchora alama za barabarani katika highway ya Tanga mjini, Muheza, sina uhakika na huko kwingine.

Hawa watu wanachora alama za chini kwenye lami ikiwemo mstari wa katikati wa kugawa barabara (kushoto na kulia).

TATIZO: Wanatumia rangi nyeupe hafifu sana huenda ni chokaa ambayo kwa muda mfupi tu ndani ya siku chache inakuwa imeshafutika na haionekani tena.

Najua wamelipwa fedha za umma kufanya kazi hiyo na wao wanafanya uhuni na usanii.

Swali langu wasimamizi wao TANROADS na Wizara hawaoni huu uhuni? Au wametoa posho kwa mabosi ili wale pesa za umma kiulaini?

Leo wapo maeneo ya Saruji, Maweni wakielekea Kange na Tanga mjini.

Tafadhalini sana wahusika fuatilieni usanii wa hawa watu.
Asante.
 
Watu mada za maana kama hizi wako kimya wanapenda zile za kula Mbususu kimasihara nk.
Ngoja mwarabu wa DP World waje kuchukua bandari na wake zenu ndio akili zitachangamka.
 
Back
Top Bottom