TANROADS: Tumeanza kuwaondoa wanaofanya shughuli kiholela kwenye hifadhi za barabara

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Alinanuswe Kyamba, amesema kuwa wameanza zoezi la kuwaondoa watu wanaofanya shughuli zao kiholela katika hifadhi za barabara bila vibali, pamoja na wale wanaotekeleza shughuli zinazokiuka sheria.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2026, Mhandisi Kyamba amesema kuwa baadhi ya shughuli zinaruhusiwa kufanyika katika hifadhi za barabara, lakini ni lazima wahusika wawe na vibali vinavyolipiwa ada kwa mujibu wa sheria. Ameeleza kuwa vibali hivyo hutolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja na vinapaswa kuhuishwa kulingana na utaratibu uliowekwa.

Amesema kuwa katika baadhi ya maeneo ya hifadhi za barabara, watu wamekuwa wakiendesha gereji, kuweka vibanda vya kuuza chipsi na kufunga mabango bila kuwa na vibali vinavyohitajika.

Ikumbukwe kuwa kumekuwa na hoja kuhusu utaratibu wa utoaji wa vibali kwa watu wanaotaka kujenga au kuweka miundombinu mbalimbali katika hifadhi za barabara, hususan katika barabara ya Morogoro (Morogoro Road).

Soma https://www.jamiiforums.com/threads...i-luis-je-tumesahau-yaliyotokea-2017.2456367/
 
View attachment 3696687

mnataka vibaka wakomae mtaani au sio!!
 
Back
Top Bottom