Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi, Machi 29, 2025, jijini Dar es Salaam, Mhandisi Besta amesema mvua zinazoendelea ziliharibu sehemu ya tuta la muda, lakini TANROADS imechukua hatua za dharura kuhakikisha mawasiliano yanarejea haraka.
“Kama mnavyojionea, wananchi wanapita kwa miguu na vyombo vyepesi vinapita, lakini kwa sasa magari makubwa yanapaswa kusubiri mpaka kazi ya kurejesha barabara ikamilike,” alisema na kuongeza
Mhandisi Besta ameendelea kwa kusema kuwa, kwa sasa, wasafiri wanaoelekea Bonyokwa Center wanashauriwa kutumia barabara ya Kinyerezi inayopita Gereza la Segerea.
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imeuhakikishia umma wa Watanzania kuwa, imejipanga kurejesha mawasiliano haraka katika maeneo yote yatakayokumbwa na maafa kutokana na mvua zinazoendelea.
Mdau alitoa wito ujenzi wa Daraja hilo ~ Tujengewe kivuko imara, hili daraja Mtaa wa Kanga, Kinyerezi Mwisho mvua ikinyesha inakuwa hatari kwa wavukaji