Tanzana ni nchi pekee duniani isiyojali elimu ya watu wake

Tanzana ni nchi pekee duniani isiyojali elimu ya watu wake

FIKRA HAI

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
231
Reaction score
79
Vyuo vya ualimu Tanzania vimefanywa sehemu ya Mkurugenzi wa elimu ya ualimu ndugu Bakari Issa kuvuna hela kinyume na taratibu na maadili ya kazi.
Aidha ndugu Bakari Issa amewateua wakuu wa vyuo kwa misingi ya kulipa fadhila hiyo.Kipindi cha kufanya mazoezi kwa vitendo kwa wanachuo wizara hutuma hela kupitia Mkurugenzi wake na hapo ndipo Mkurugenzi huamuru kurudishiwa fedha kiasi Fulani kwa mlango wa nyuma.Hivyo wakuu wa yvuo hulazimika kupunguza posho za wakufunzi wataokaenda kuwakagua.
Aidha baada ya kuzidisha hela mwaka Jana na kupanga kuwa itahusika na vifaa vya wanachuo wanaokwenda BTP,na kuonekana vifaa wanavyopewa haviendani kabisa na kiwango cha fedha kilichopa,ndipo wanafunzi walipo Dai kupewa hela badala ya vifaa.
Hapo ndipo Issa akaja na mpango kuwa vifaa hivyo Ni pamoja na na mahitaji ya vyuo katika ufundishaji.Ni kwanini hakutoa maelekezo kabla ya hapo?
Na tabia hii imepelekea wakuu wa vyuo wengi kujiona wao ndo kila kitu na kuanza kuwadharau wafanyakazi wake.
Mkuu mmoja wa Chuo alisikika akisema wakufunzi chuoni kwake wote ni ng'ombe eti kwa sababu hawana hela,engine wakinunua magari anawakejeli eti bati Tu hiyo.Watu hawajali ufundishaji badala yake Ni kuangalia maslahi Yao na tuna viongozi katika kila nyanja.
Kuna mgogoro unaoendelea pale Chuo cha ualimu songea yote yamesababishw na Bakari Issa,nauliza nani yupo nyuma ya huyu mtu?
 
Hapo nimekuelewa,
binafsi ni mmoja kati ya wale waliokuwa wanachuo wachuo x huo mwaka jana! kiukweli ndio mwaka ambao pesa ya btp iliongezeka kutoka elfu mbili hadi elfu nne na mia tano per day,
chakustaajabisha pesa yavifaa/zana uongozi uliamua kutununulia vifaa kama rula,manila,daftari na kalamu-
wengi tuliridhishwa na mwenendo huo ila wakati tupo btp tulijua kuwa wizarani zilitolewa pesa taslim 47,000 ambazo kila mwanafunzi alitakiwa apewe kama fedha ya maandalizi ya zana/uifaa vyaufundishaji lakini wachache wakafanya mchezo nawakapiga pesa kupitia mkuu wa chuo, hatukuwa na jinsi isipokuwa kuwa wapole na kumaliza salama kwani muda wa mtihani ulikuwa karibu mno,
Thanx God nimemaliza nakufaulu vizuri sana and now nasubiri ajira zao while working in private schools..
 
Back
Top Bottom