Tanzania: 110 Foreign Nationals Given Tanzania Citizenship

Tanzania: 110 Foreign Nationals Given Tanzania Citizenship

Sifa ya kwanza kupata uraia wa nchi yeyote kwanza ni lazima ujue kusoma,kuongea na kuandika Lugha ya nchi unayotaka uraia kwa ufasaha pili ukubali kuingia kwenye utamaduni wa nchi hyo tatu ukubali kushirikiana na jamii utakayoikuta ikiwamo kushiriki ktk mambo yote ya kijamii na kitaifa
Lakini mm naona kwa nchi maskini za kiafrika watu wananunua uraia si kuomba uraia kwani kunatofauti ya kununua na kuomba uraia

huwezi kuupata uraia wa Germany,Japan,Denmark na nchi zote za Dunia ya kwanza na ya pili bila kujua Lugha ya hzo nchi lakini Tanganyika unakuta muhindi raia wa Tanzania hajui hata kuongea tu kiswahili sasa unajiuliza huyu aliomba uraia au alinunua uraia

Kweli kabisa, kuna siku nlienda kununua sim kwenye duka la muhindi kule posta, sasa kesho yake nlirudi na ile simu sababu kuna kitu kilikuwa hakiko sawa kwenye ile simu, nafika pale nkamkuta akiwa na wafanyakazi wengine [waswahili] ile naanza kumwelezea kilichonileta kwa Kiswahili, mara ghafla akang'aka "i don't know swahili talk to this one" huku akiwakaribisha wateja wengine ambao walikuwa ni wahindi wamefikia na wao kununua bidhaa, tena akaniambia nisogee pembeni na BOX langu maana aliona kama natia kiwingu.

Hapo nikapata kuwaelewa hawa watu ni wanamna gani maana sio mara ya kwanza kukutana na dharau za wahindi
 
Back
Top Bottom