Tanzania among weakest currencies in Africa

Ulichoandika ni sahihi
Ila kuna kupandisha thamani ya shilingi kwa kutoa zeros(fatilia), nchi kadhaa wamefanya
Na ndiyo maana nikatoa mfano Wa Zambia, msumbiji wamefanya hivyo, hiyo ndiyo hoja ya msingi kwanini na sisi tusifanye hivyo?
 
DOLLA ndo sarafu inayotafutwa zaidi duniani Mkuu, kwa mfano uloutoa mbona kuna nchi zimeizidi thamani DOLLA japo hazina Uchumi mkubwa....

Nadhani tunachanganya UCHUMI WA NCHI na THAMANI YA SARAFU ni vitu viwili tofauti japo vyaenda sambamba.
Supply and demand.., kuna supply ya dollar kiasi gani kulingana na utafutaji ?inaweza ikawa inatafutwa sana na supply yake ni kubwa nyingine inatafutwa kidogo na supply yake ndogo..., kama utafutaji ni watu kumi na supply ni 30 mwenye utafutaji wa watu wawili na supply ni moja atakuzidi...

Pia kumbuka kuwa na currency yenye nguvu kuna hasara zake bidhaa zako zinakuwa za gharama kuuza nje ndio maana China analaumiwa kwa ku-manipulate currency yake against the dollar ili iwe low hence cheaper products
 
Ulichoandika ni sahihi
Ila kuna kupandisha thamani ya shilingi kwa kutoa zeros(fatilia), nchi kadhaa wamefanya
Unachoongelea ni currency Revaluation..,(google upate maelezo zaidi) kwa kufanya hivyo pesa yako inakuwa na gharama kubwa kuliko ya nchi za nje.., sasa wewe wakati unabembeleza watu wanunue vitu vyako hawanunui alafu unaongeza gharama mara kumi unadhani watanunua ?

China wanamanipulate currency against the dollar (devalue) iwe na thamani ndogo ili watu wanunue zaidi (cheaper products) yaani mmarekani akienda china anapata bidhaa nyingi zaidi
 
Ulichoandika ni sahihi
Ila kuna kupandisha thamani ya shilingi kwa kutoa zeros(fatilia), nchi kadhaa wamefanya
Mfano ni Zambia na Botswana(kama sijakosea) lakini hii haitatui chochote ni njia ya muda mfupi kwa sababu baada ya miaka kadhaa mbele thamani ya salafu zao zitaendelea kushuka thamani kama kwaida.

Sababu Wanajaribu kupitia njia fupi na sio njia ndefu ambayo yanahusisha yafuatayo ambayo kwa kiasi kikubwa husababisha sarafu kushuka thamani.

1. bidhaa toka nje
Uagazaji wa bidhaa toka nje kwa kiasi kikubwa husababisha demand ya dola kuongezeka kwa sababu mabadilishano ya fedha kwa kiasi kikubwa ni dola ya marekani. Deficit ikiwa kubwa thamani ya sarafu itakuwa ndogo.

Ukija kwa nchi yetu anza kuangalia bidhaa tunazoagiza toka nje na zile tunazouza kwenda nje.

2. Mfumuko wa bei
Mfumuko wa bei inamaanisha pesa imeongezeka mtaani kuliko uzalishaji maana yake thamani ya sarafu itashuka tu ukishindwa kudhibiti mfumuko wa bei.

Zimbabwe kipindi cha Mugabe baada ya vikwazo uzalishaji ulikuwa chini, Ililalizimika serikali ichape mpaka noti ya dola ya zimbabwe bilioni moja.


sarafu za zamani za zimbambwe​
Japokuwa naona zimbabwe wamezuia uuzwaji wa sarafu za nje.
https://www.bbc.com/news/world-africa-48757080

Sababu zingine ambazo nchi zinapaswa kudili nazo zinazobabisha sarafu kushuka ama kupanda inahusisha

3. Uwiano wa bei za bidhaa tunazouza nje na zile tunazoagiza
4. Deni la Taifa.
5. Interest rates
6. Hali ya uchumi kwa wakati husika.

Kwa bahati mbaya au nzuri mambo kwa sasa yako tofauti.

Zamani import na export ilikuwa ni factor kubwa lakini sasa hivi forex inafanywa kwa mtindo wa speculation na kuna mabenki kama kumi yana influence hizi thamani za sarafu.


Ndio maana ukiwa unaangalia thamani ya shilingi vs USD unakuta inabadilika badilika hata baada ya dakika tano.

Hii inasababishwa na speculators, Na hawa speculators(mabenki, hedge funds, serikali mfano switzland 2010 ) huwa wanaangalia hizo factors 6 na zingine za kisiasa.

Sasa kama hizo kama hizo baadhi ya factors nilizoweka zikiwa nzuri demand ya currency itakuwa kubwa tu na wala nchi haitohitaji kupunguza sifuri.

Mtindo huu wanaofanya baadhi ya nchi wa kuzipa thamani ya juu sarafu zao sio rafiki na mchezo wa panya na paka.

Kwangu mimi nikiangalia uhalisia sioni ni namna ambayo sarafu ya tanzania inaweza pambana na dola ya marekani hata Rais awe nani na serikali iwe na chama gani.
 
Sawa mkuu, kula kongole,kwa mchango yenye tija, maana kuna watu wanaruka viduku kwenye nyuzi ambazo zimewazidi umri. Sisi mamuma Wa uchumi tunaitaji analysis kama hizi zenye kufikilisha.
 

Walikosea sana maana inflation ilikuwa ikiendelea bado
Ukitoa zeros akat kuna inflation ni kaz bure
 
Eti uondoe zero ili pesa ipande thamani.
Wazee uchumi ni taaluma sio suala la kukurupuka kama rahis wenu. Mtambue kwamba kuna Watu wanakaa darasani kusomea hayo mambo na sio jambo rahisi la kuongeza na kupunguza zeros.
 
Why dont yhe government apply elimination of zeros

Currently
1 usd =2300tsh

After eliminating zero
1usd =230tsh

Then our lowest will be 5tsh instead of 50tsh

And our highest currency will be 1000 instead of 10000tsh
Hii kitu aliniambia baba yangu jana nimemkumbuka mzee
 
Ina maana pesa yetu ikibadilishwa itakuwa juu sana kuliko iyo rand tafsiri ni kuwa 400Tsh mpaka 700Tsh ni rand chache na gharama nafuu sema tumeivuta pesa yetu inahitaji fixation irudi[/QUOTE]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…