Mfano ni Zambia na Botswana(kama sijakosea) lakini hii haitatui chochote ni njia ya muda mfupi kwa sababu baada ya miaka kadhaa mbele thamani ya salafu zao zitaendelea kushuka thamani kama kwaida.
Sababu Wanajaribu kupitia njia fupi na sio njia ndefu ambayo yanahusisha yafuatayo ambayo kwa kiasi kikubwa husababisha sarafu kushuka thamani.
1. bidhaa toka nje
Uagazaji wa bidhaa toka nje kwa kiasi kikubwa husababisha demand ya dola kuongezeka kwa sababu mabadilishano ya fedha kwa kiasi kikubwa ni dola ya marekani. Deficit ikiwa kubwa thamani ya sarafu itakuwa ndogo.
Ukija kwa nchi yetu anza kuangalia bidhaa tunazoagiza toka nje na zile tunazouza kwenda nje.
2. Mfumuko wa bei
Mfumuko wa bei inamaanisha pesa imeongezeka mtaani kuliko uzalishaji maana yake thamani ya sarafu itashuka tu ukishindwa kudhibiti mfumuko wa bei.
Zimbabwe kipindi cha Mugabe baada ya vikwazo uzalishaji ulikuwa chini, Ililalizimika serikali ichape mpaka noti ya dola ya zimbabwe bilioni moja.
View attachment 1167209
sarafu za zamani za zimbambwe
Japokuwa naona zimbabwe wamezuia uuzwaji wa sarafu za nje.
https://www.bbc.com/news/world-africa-48757080
Sababu zingine ambazo nchi zinapaswa kudili nazo zinazobabisha sarafu kushuka ama kupanda inahusisha
3. Uwiano wa bei za bidhaa tunazouza nje na zile tunazoagiza
4. Deni la Taifa.
5. Interest rates
6. Hali ya uchumi kwa wakati husika.
Kwa bahati mbaya au nzuri mambo kwa sasa yako tofauti.
Zamani import na export ilikuwa ni factor kubwa lakini sasa hivi forex inafanywa kwa mtindo wa speculation na kuna mabenki kama kumi yana influence hizi thamani za sarafu.
View attachment 1167233
en.wikipedia.org
Ndio maana ukiwa unaangalia thamani ya shilingi vs USD unakuta inabadilika badilika hata baada ya dakika tano.
Hii inasababishwa na speculators, Na hawa speculators(mabenki, hedge funds, serikali mfano switzland 2010 ) huwa wanaangalia hizo factors 6 na zingine za kisiasa.
Sasa kama hizo kama hizo baadhi ya factors nilizoweka zikiwa nzuri demand ya currency itakuwa kubwa tu na wala nchi haitohitaji kupunguza sifuri.
Mtindo huu wanaofanya baadhi ya nchi wa kuzipa thamani ya juu sarafu zao sio rafiki na mchezo wa panya na paka.
Kwangu mimi nikiangalia uhalisia sioni ni namna ambayo sarafu ya tanzania inaweza pambana na dola ya marekani hata Rais awe nani na serikali iwe na chama gani.