Tanzania bado tuna tatizo la upangaji vipaumbele vyetu, baada ya Elimu, Afya na kilimo, ilipaswa ije nishati!. Ni aibu na hatari kupikia kuni na mkaa!

Wanasema baba ndio kichwa cha familia, familia isiyokuwa na uwelekeo wakimaendeleo baba ndio tatizo.

Pascal Mayalla wana ccm nyie ndio baba wa taifa hili nini shida kwenye hili la kilimo
Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu, ni kweli pale mwanzo Baba alikuwa tatizo, na baadhi ya akina sisi watoto, hilo tuliliona, hatuku kaa kimya kwa kunyamaza, tulipaaza sauti zetu kulisema




Huyu Baba wa sasa aliyepo, (japo kijinsia ni mwanamke), ili asifanye makosa kama ya Baba aliyemtangulia anahitaji kusaidiwa kuonyeshwa tatizo ni sisi Watanzania wenyewe kwenye Upangaji wa Vipaumbele Vyetu, baadhi ya sisi Watanzania wazalendo tumeisha libaini hili na tumejitolea kujitokeza kumsaidia kupitia sauti zetu (TV Program ya "Kwa Maslahi ya Taifa" ), au kupitia makala za magazetini "Kwa Maslahi ya Taifa" na huku kwenye mitandao ya Jamii ikiwemo JF, na mfano mzuri ni Makala yangu hii

Tanzania bado tuna tatizo la upangaji vipaumbele vyetu, baada ya Elimu, Afya na kilimo, ilipaswa ije nishati!. Ni aibu na hatari kupikia kuni na mkaa!

Makala hiyo iliandamana na kipindi cha TV kwenye ITV na TBC. Sasa kama Mzee Baba (Mama Babaa) na lile jicho lake (japo limeregea lakini linaona sana), litakuwa limeona, hata kama sio yeye mwenyewe in person, lakini lile jicho lake jingine by proxy linaloona kila mahali , kila kona hadi uvunguni, litakuwa limeona, hivyo Mimi kama raia mwema wa taifa langu, nitakuwa nimetimiza wajibu wangu kwa nchi yangu.

P.
 
Wanabodi,
Baada ya kijiuliza tatizo ni nini, ndipo nimekuja na conclusion yangu, sisi Tanzania tuna tatizo katika upangaji wa vipaumbele vyetu!.
Paskali
Hili tatizo la Upangaji wa Vipaumbele Vyetu, linaendelea kututafuna na kukata across the society yetu.

Jana ndio ilikuwa ufunguzi wa Bunge Live kupitia TBC 1. Baada ya Bunge kuanza, hardly 5 minutes, TBC wakahamia kwenye shughuli nyingine less important kuliko Bunge, lakini Kwa TBC, ikapewa umuhimu zaidi ya Bunge. Hivyo kwenye Upangaji wa Vipaumbele Vyetu nini ni muhimu zaidi kustahili Bunge live kuachwa na kutangazwa live nyingine.

Leo Bunge live, ilikuwa inasomwa budget ya Waziri Mkuu, huwezi amini Bunge live ilikatwa tena tukapelekwa live nyingine!.

Bado tunamatatizo katika upangaji wa Vipaumbele Vyetu, mtu akifanya booking ya live, kama ni muda wa Bunge live, then aambiwe huo ni muda wa Bunge Live. Hivyo afanye adjustment ya ratiba yake isiingiliane na Bunge live.

Kama Bunge linalipia hiyo Bunge live kwa TBC, then it's not fair kwa TBC kuikatisha na kurusha live nyingine.

Lakini kama TBC wanawarushia Bunge live bure, akitokea mteja anayelipa, then, they are right kuwakatisha.

Kama Bunge wanalipa, halafu anatokea mteja mwingine analipa, kitendo cha kulikatisha Bunge Live kwa ajili ya live nyingine,ni kushindwa kupanga Vipaumbele Vyetu, kati ya mihimili yote mitatu, ya Bunge, serikali na mahakama, Bunge ndio the most important kwasababu ndio Mhimili pekee wa wawakilishi wa wananchi wenye Katiba na ndio walipa kodi.

P
 
Anko nikitulia nitasikiliza makala yote.
 
Niliwahi kushauri, Rais Samia asaidiwe kwenye eneo la upangaji vipaumbele vyetu,
Kwenye uzi huu nilishauri kipaumbele No.1 Elimu, 2. Afya 3. Kilimo
Hiki ndicho Dr. Bashiru alichokisema, sijui kwanini watu wamjie juu wakati it is facts.
P
 
Niliwahi kushauri, Rais Samia asaidiwe kwenye eneo la upangaji vipaumbele vyetu,
Kwenye uzi huu nilishauri kipaumbele No.1 Elimu, 2. Afya 3. Kilimo
Hiki ndicho Dr. Bashiru alichokisema, sijui kwanini watu wamjie juu wakati it is facts.
P
Makada wa CCM hawajawahi kukubali kukosolewa kama alivyowahi kushauri hayati Julius Nyerere (1962 "Tujisahihishe".

Alipoondoka madarakani Nyerere aliendelea kuikosoa serikali ya rais Ally Hassan Mwinyi lakini aliheshimiwa hakuwahi kushambuliwa na vijana wa CCM kama ilivyo sasa mpaka Nyerere aliandika kitabu kingine " "Uongozi wetu na hatma ya Tanzania"

Nchi inatakiwa isimamiwe kujenga taifa la haki, heshima, huru, linalojitegemea ili kufikia maendeleo katika ngazi zote za kijamii.

Makada wa CCM kumshambulia Dr.Bashiru Ally ni sawa na kuwashambulia wapiga kura walioichagua serikali kuwasikiliza na kuwatatulia matatizo na changamoto wanazokumbana nazo kila siku ukizingatia hali ya uzalishaji chakula kwa wakulima wadogo wadogo ni duni, mvua hakuna, umeme hakuna, pembejeo ni za upendeleo na bei aghali sana kwanini msikosolewe?
 
Tatizo la upangaji vipaumbele vyetu, pia tuna tatizo kwenye manunuzi makubwa!, tuliona mambo kwenye Rada, kwenye ndege ya rais, kwenye Richmond, kwenye ndege za Atcl, kwenye mitambo ya JNHEP, na sasa kwenye mabehewa!, tumeletewa mabehewa chakavu, hata kwa macho tuu unayaona, viongozi wetu wanatuambia ni mapya kutoka kiwandani!, hii maana yake ni tumeuziwa mabehewa chakavu kwa bei ya mapya!.

Ziko nchi 4 zenye heshima kubwa duniani kwenye reli, 1. Ujerumani, 2. India, 3. China, 4. Afrika Kusini, ilikuwaje kuwaje kampuni ya Uturuki, iliyoanzishwa mwaka 2019, ikapewa tenda hii kubwa ya kununua mabehewa ya Tanzania?.
P
 
Zahma bin fedheha kubwa hii aisee. Yaani raia tunachezewa akili kisawa sawa. Sasa haya mambo lazima yafike hatima na mwisho wake maana si sawa hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…