Tanzania Bara iwekeze kwenye elimu kwanza.


Barubaru,
Nakubaliana kabisa na wewe. Bila elimu tunapoteza muda maana hakuna tutakachoweza kufanya na tunaanda bomu litakalolipuka baada ya muda mfupi. Ujinga ni balaa kubwa kwa nchi yeyote ile.
 

Kwa kweli umenichekesha sana. Siku zote tunaamini Mkataa kwao ni mtumwa.

Mimi naamini wazi ilmu ya Tz ipo juu sana kwani inamfundisha mwanafunzi mambo mengi sana ukilinganisha na western education. Tatizo ni mfumo unaotumika na kukosekana kwa vifaa bora na nyenzo bora za kufundishia. Na kwa hivi sasa huu udanganyifu na kukariri mitihani kunakofanywa na mamlaka zilizo na dhamana.

Kwa bahati mimi ni mmoja niliyesomea huko Bara kuanzia Mtendeni primary, Tambaza sec, Ilboru na UDSM. Zote nimesomea Tanzania lakin pia nimesomea Carleton University (Canada) na Sophia University ( Japan). Na ukisema mihadhara sio tu Oman au nchi za kiarabu lakin pia hata tanzania, Nigeria, USA, Uk Canada na kwingine kwingi tu. Hivi ninavyo ongea wiki mbili zijazo nitakuwa South Africa kwenye makongamano ya kitaaluma.

Nilichobaini kwako ni Dharau dhidi ya Mamlaka iliyopewa dhamana na nchi yako kisharia kusimamia suala la ilmu zote. Dharau hizo zimekufikisha kukata tamaa kimaisha na kuikatisha tamaa jamii yako. Nakumbuka last time nilikuja UDSM kwenye college ya Biashara nikawa naongea na mmoja wa sr lecturer ambaye alikuwa nyuma yangu nikiwa hapo. yeye aliniambia vijana siku hizi hawasomi kama enzi zetu ndio maana tunawashika sana. Nilifadhaika sana kwa hilo.

Nilimweleza kitu kimoja tu. Siku zote lecturer anapimwa kwa kiwango cha kufaulisha na sio kufelisha. kama wewe umewafundisha wanafunzi 40 na ulipotoa mtihani only 15 wakafaulu the rest wakafeli ujue kuwa haueleweki darasani hivyo huwezi kupandishwa cheo. Huo ni mfumo wa kisasa.

lakin kumbuka kuwa TCU ni taasisi iliyo makini na ipo na kufuata mitaala ya nchi za Madola. Ni chombo halali kisharia kilichowekwa na Serikali yako kupima ubora wa ilmu yenu na ndio maana ilmu yenu inakubalika katika nchi zote za madola.

sasa wewe kaa pembeni na kukejeli , pasi na shaka ndio wale wale wanaolalama bila kutoa suluhisho la problrms mlizonazo.

nakupa pole sana.

Lakinkumbuka Znz imewekeza sana na kuna vyuo vingine vitatu nafikiri baada miaka miwili vitakuwa njia moja kuongeza wasomi katika nchi hiyo ndogo yenye watu wasiopungua milioni moja na nusu. Je Bara mnajiweka vipi kwa hili la kuongeza wasomi ili muingia katika ushindani wa EAC.

 

kwa jinsi unavyopeteza muda kujitambuliasha kuwa umesoma na kuwaona wengine hawajui ni wazi kuwa.umeenda shule ila hujaelimika+ pride ndio kitu kinachokupoteza usijifunze na kuelewa mapya.

Hembu leta ushahidi wa kuthibitisha kwamba lazima ukisoma uelimike.Ndipo tuweke reference zetu sana.Yaani tufanya calibration.
 

Nafikiri ahali yangu unajichanganya.

Nilichobainisha hapo kwa stage ya juu. Kumbuka kuwa kuna watu ambao lazima wafanye hizo kazi za kuhakiki na ku short list wale walioweza kufaulu kwa vigezo vilivyowekwa. kama interviewer ni lazima apate CV hizo mapema ikiwa pamoja na uthibitisho wa Vyuo alivyosomea mwombaji kabla kuanza kumsahili.

haiwezekani kabisa kumsahili mtu kabla hajahakikiwa uhalali wa vyeti vyake kwani hilo linaweza kumwingiza pabaya yule interviwer pindi ikijulikana nae alishiriki kumwingiza kazini. Kama mtu ameajiriwa na vyeti feki basi hukma yake inaanzia kwa wote walioshiriki kumwajiri mtu huyo kuanzia utawala, interviwers etc.

lazima uwe makini kwa hilo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…