Tanzania deports east African migrants

Tanzania deports east African migrants

Hayo ni maeneo ya Kilimanjaro ambayo yapo karibu na Kenya, hivyo kuna uwezekano mkubwa ukakuta Wakenya kuwa wengi zaidi ya watu wa mataifa mengine, na pia upande wa pili ndani ya Kenya utakuta kuna Watanzania wengi, ni kama vile ukienda Kigoma utategemea Warundi wawe wengi.

Japo pia nawashangaa ndugu zangu Wakenya wanaong'ang'ania kuishi kwenye nchi yenu hiyo, hii inafaa iwaingie kwamba ukienda kuishi kwenye nchi yenye chuki chuki na majungu, hakikisha stakabadhi zako zote zimekaa sawa
- Hakikisha umesajiliwa na ubalozi wa kwenu (hawa husaidia sana wakati unanyanyaswa)
- Hakikisha umepata vibali vyote, residential permit and work permit
- Hakikisha unaye wakili wako anayefahamu fika masuala ya uhamiaji

Naomba Wakenya tuendelee kuwa wakarimu kwa hawa watu wao waliojazana huku wakiwemo wale omba omba wao, tusilipize chuki kwa chuki.
Umesahau roho zenu mbaya zinazoambatana na ukatili.
 
Kila mtu ana kwao na kila mtu kama anaenda kwa mwenzie afate sheria za huko baasi....kama wewe umeruhusu wasiofata sheria hayo ni yako na yanakuhusu wewe na watu wako huko ila msitake tufanye mambo eti kisa kwa sababu na nyie mnafanya hapo mtangoja sana
 
Tumia ubongo kuandika, unafikiria kama tungekua wenye chuki kama nyie na tuwe na haja ya kuwafukuza hawa maelfu ya Watanzania kutoka Gikomba ingetuchukua zaidi ya siku moja? Hatungepoteza muda wa kuwachomea maduka, wanakusanywa tu mchana peupe na kuondolewa.
Lakini nchi yetu inatambua umuhimu wa kuwaachia wajasiria mali wachakarike, uwepo wa wageni wajasiria kutoka Somalia, Tanzania na kwengineko kunachangia pakubwa kwenye ukuaji.
Jirani yangu hapa Mtanzania amejenga apartments nzuri sana na tayari zimepata wapangaji, hivi ndio njia za kukuza uchumi, sio kuendeshwa kwa mihemko ya chuki.
Hata bongo kuna wakenya wengi wanafanya kaz wanakuja kununua mazao ulishawai sikia tumewaletea shida..????jaman jifunzen kufata utaratibuu tu tz hatuna shidaa na nyie
 
Hata bongo kuna wakenya wengi wanafanya kaz wanakuja kununua mazao ulishawai sikia tumewaletea shida..????jaman jifunzen kufata utaratibuu tu tz hatuna shidaa na nyie
Nakutanaga tu na wengi na wala hawana presha wanaendelea na shughuli zao shida hawa wengine wasiotaka kufata sheria
 
Ukatili upi huo unaozidi kuwala albino kama kitoweo na kuwachoma vifaranga kwa moto? Mungu anawaona.
Mbona mnang'ang'ania Tanzania sana kwani hamna kwenu? Ukitaka mkenya avae chupi kichwani mwambie marufuku kuingia Tanzania!!! Oh it gonna be WWIII
 
Mbona mnang'ang'ania Tanzania sana kwani hamna kwenu? Ukitaka mkenya avae chupi kichwani mwambie marufuku kuingia Tanzania!!! Oh it gonna be WWIII
Dah hii joke yako ni dry kama zile za MC Pilipili. Try again another day.
 
Achana nao akili zao hutazielewa. Watz wengi huwa wanajaribu ku'justify' upuuzi unaofanywa na serikali yao, kwa kusema kuw watz wenzao huwa wanadhulumiwa huku Kenya. Cha ajabu mtz yeyote ambaye amefika Kenya anajua uhalisia wa mambo. Wala time ya majungu ya kitoto na kulazimisha mambo madogo madogo yasiyoeleweka huwa hatuna. Kenya ingekuwa hivo tungekuwa tupo nyuma sana kimaendeleo na kifikra. Hapo ndipo napomkubali rais Uhuru Kenyatta, acha tu'concentrate' on the bigger picture kama wakenya. Hayo maswala madogo madogo tuwaachie vijana wadogo.
Kama wewe unavyo-justify Wasomali kurudishwa Somalia toka Daadab camp.
 
Haya mambo yakifanywa na Israel na Marekani watu watapiga kelele na mapovu yakutosha wakiongelea the so called ubaguzi.
 
Si kama mnavyowaitaga Israel na Marekani wabaguzi wakifanya haya yaliyofanywa na Tanzania.
Hakuna nchi yoyote duniani inayoruhusu watu kuishi bila document, hao huko Israel wamejisajili kama refugees, dunia inalalamika kwa sababu kuna haki za kimataifa za watu walioomba hifadhi kutokana na mizozo katika nchi walizotoka, hawa wakenya wakitaka kuishi bila proper documents wanaweza kujiandikisha kama wakimbizi wamekimbia njaa nchini mwao, tutawapokea na kuwapa chakula kama tunavyowahifadhi warundi na wakongo.
 
Back
Top Bottom