Hongera sana Tundu Antiphas Lissu,
Nakuona Tarehe 28/10/2020 ukienda kupiga kura kituoni, Naona watanzania wengi wakienda kukupigia kura siku hii.
Naona vituo vya kupigia kura vikiwa vimejaa, wananchi wakiwa na furaha wakisema Ni yeye.
Naona zoezi la kupiga kura likiwa limekamilika na maeneo mengi Tanzania wananchi wakiwa mita 200 kusubiri matokeo. Wengi wakiwa hawajali kama kuna mvua au jua wanachotaka ni kupata matokeo yao.
Naona maeneo mbalimbali ya Tanzania wananchi wakianza kushangilia kuwa unaongoza kwa kura nyingi dhidi ya Mpinzani wako Magufuli na naona watanzania wengi wakiwa na furaha huku wakipigwa na butwaa kwani hawaamini yanayotokea.
Naona kiongozi mkuu wa kikosi cha walinzi wa viongozi alifika nyumbani kwako na kukutaarifu kuwa Idara nyeti ya Taifa imeamua kukuwekea ulinzi na nyumba yako ikiwekewa ulinzi na kikosi maalumu cha kulinda viongozi. Hii ni kwa sababu idara imeona ni vyema na vizuri kukutambua rasmi kama amiri jeshi mkuu mtarajiwa.
Mwisho Naona vuguvugu la ushindi wako linawashinda Tume ya Uchaguzi maana Tanzania nzima ni furaha na maandamano ya watu kushangilia kuanguka kwa Magufuli na hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi inakutangaza kama mshindi wa kiti cha Uraisi.
Mungu naomba fanikisha na simamia hili kwa Jina la Yesu Kristo. Amen.