Drone Camera
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 14,041
- 13,907
Huo unafiki unaouongelea ndo ninaomaanisha mimi. Na hiyo ni tabia ya mtu binafsi si tabia ya watu wa taifa fulani na utaikuta kwa baadhi ya watu wa taifa lolote lile.Unafiki upo, ni kawaida ya binadamu na hakuna yeyote dunia hii ambaye hakosi unafiki wa kiana, sisi wote tunao, hakuna msafi, ila hapa nazungumza kwa niliyoyaona kwenu, yaani hamna kitu kinauma kama mtu aongee nawe kwa lugha mnayotumia huko kwenu yenye ukarimu sana kisha uje kumsikia maneno aliyokusema. Yaani unabaki ukijiuliza maswali mengi sana maana kwa muda wote hukuona dalili ya aina yoyote ya kwamba jamaa anakuchukia, au wana chuki baina yao.
Tafiti zimefanywa za kisayansi zinaonyesha Tanzania ipo ndani ya mataifa kumi ambayo wananchi wake hawana furaha duniani, kwa mtu ambaye hawajui Watz kiundani hatasadiki maana ni nchi ambayo haijawahi kuwa na vta vya ndani, lakini inawekwa pamoja na mataifa ambayo kwao ni mwendo wa mabomu kila siku.
Hiyo ya Tz kuwekwa hilo kundi ni kutokana na haya mambo yanayoandikwa na wanasiasa na waandishi wengine..,na sio kwamba hizo takwimu au list siku zote zinaakisi uhalisia,hapana... Lile tukio la Makonda na Pompeo liliifanya Dar ianze kumulikwa kama jiji hatari.
Lakini je kwa uzoefu wako wa Dar es salaam na miji mingine duniani,hivi unaweza kuiweka dar miongoni mwa majiji hatari kweli? Dar hii ambayo hata ukiwa na silaha huoni umuhimu wa kutembea nayo inaweza kuwa hatari kweli kuliko Johannesburg au Durban ninayoona silaha nje nje na petty crime zakutosha? Hivyo si kila muda hizo data zitareflect uhalisia.