Uko serious au unatania!! Hii hata Arusha, Mwanza, Iringa, Mbeya, Morogoro hipo. Najua ata Eldo na Kisumu huwezi kosa road kama hii. Nilijua nilicho kuuliza, Kigali ni pazuri ila kui compare na Dar ni kujitoa ufahamu. Mfano fly overs zinajengwa kutokana na mahitaji siyo mapambo, kwa Kigali ilivyo in the near future siioni ikiwa na fly over. Ila mpaka 2025 Dar itakua na fly over 7, hapa naongelea miradi ambayo michoro ipo tayari na pesa imeshatengwa mengine ujenzi ume anza. Hapo bado kuna junctions ambazo zipo center upembuzi umeanza wa kuziwekea Fly over kama Morocco, Magomeni na Mwenge. Mimi nimefika Nai na Kampala ukweli kabisa Dar na Nai ndiyo miji ambayo itachuana E.A, Kigali ni kadogo sana inaweza ikawa sawa na wilaya moja ya Dar kimwonekano mpaka mapato.