Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Ni jambo la kushangaza sana eti tozo tulizobakiziwa ni kwa sababu ya ujenzi wa miradi ya kimkakati! Kwamba miradi hii inayokaridiriwa kugharimu zaidi ya trilion 30 yote inapaswa kukamilishwa kwa fedha za tozo.
Mwigulu anapaswa kuambiwa kuwa Tanzania ipo milele haifi leo wala kesho hivyo ujenzi wake utaendelea milele. Walijenga wahenga wetu na sisi tunaendelea pale walipoishia na wanaokuja wataendeleza pale tutakapoishia.
Hata ndani ya familia kama hawana rasilimali za kutosha maendeleo huenda kwa hatua, watajenga nyumba, baadaye watanunua gari nk. Hawatekelezi vyote wanavyohitaji kwa pamoja kwa kujinyima mahitaji ya msingi kama chakula, mavazi, elimu kwa watoto, matibabu nk.
Kwa hiyo Mwigulu aelezwe hata Rome haikujengwa kwa siku moja, hali kadhalika kwa Tanzania Nyerere alifanya sehemu yake, Mwinyi pia, wakafuata Mkapa, Kikwete na hatimaye Magufuli. Samia pia atafanya yake.
Tusiumizane bila sababu ya msingi. Mwigulu yeye haoni shida kwa sababu ni mnufaika wa tozo. Mwigulu hapati uchungu wo wote kwa sababu analamba asali, anakula kwa urefu wa kamba aliyofungwa na Samia! Mwigulu akumbushwe kuwa wengine tozo zinagharimu mlo wa siku! Mwanafunzi wa chuo akitoa laki moja gharama ya tozo ni mlo wa siku moja!