SoC02 Tanzania haijachelewa kuufikia uchumi wa Viwanda

SoC02 Tanzania haijachelewa kuufikia uchumi wa Viwanda

Stories of Change - 2022 Competition

Chode kanju

Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
17
Reaction score
19
Tanzania Haijachelewa Kuufikia Uchumi wa Viwanda

Tanzania ya Viwanda ni sera iliyopewa kipaombele sana na Raisi wa awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli akiamini kupitia uwekezaji na maendeleo ya viwanda ndio njia pekee itakayoiwezesha Tanzania kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi yatakayo akisi ustawi wa jamii kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma zote muhimu kama elimu, maji, afya, nishati, usafiri kwa ubora wa hali ya juu lakini pia kwa gharama nafuu ambazo hata kwa mwananchi wa hali ya chini ataweza kuzimudu, lakini pia utakaowezesha kutatua tatizo sugu la ajira kwa watu wa hali zote wenye viwango tofauti vya elimu hasa Vijana.

Dhamira, sera na maono hayo ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2025, haikuishia tuu kwenye makaratasi lakini ndani ya kipindi cha uongozi wa awamu ya tano, Tanzania ilianza utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa (mega projects) kama mradi wa ujenzi wa Reli ya umeme (Standard Gauge Railway) pamoja na ule wa bwawala kufua umeme la Mwalimu Nyerere (Steglier’s Gorge Hydroelectric Power Station) ambayo kukamilika kweke itakuwa chachu kwa Tanzania kufikia ndoto yake ya kuwa nchi ya viwanda.

Mageuzi ya kiuchumi ni suala linalohitaji Dira, sera na mipango madhubuti ya kimkakati ya muda mrefu, si suala linaloweza kufanyika ndani ya miaka miwili, mitano.

Mageuzi ya uchumi hasa ule wa viwanda unahitajji ufanisi wa maeneo mengine ambayo pamoja na jitihada za serikali za kutunga sera na mipango ya kuhakikisha ufanisi wa maeneo hayo lakini hali bado hairidhirishi kwa kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kiushindani (competitive economy) barani Afrika lakini pia na duniani kwa ujumla. Maeneo mengi ambayo ni nyeti katika kuchajiza ukuaji wa kiuchumi bado yanahitaji nguvu ya ziada ya kiuwekezaji (massive investment) itakayo chajiza na kuhamasisha mageuzi ya viwanda
Sera yoyote ya kimaendeleo na ukuaji wa uchumi eidha iwe uchumi wa buluu (blue economy) au uchumi wa viwanda (industrial economy) inategemea sana ufanisi wa sekta za usafirishaji, nishati, rasilimali watu (human resources ) ambayo ni zao la mfumo wa elimu, lakini pia bila kusahau msaada wa kitaasisi (Institutional support).

Kwasababu Tanzania ya viwanda ni mpango wa muda mrefu, hivyo basi, na ni dhahiri kwamba hakuna serikali yoyote duniani ambayo haifurahii kuona maendeleo hasa ya kiuchumi ya nchi husika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nayo ina kila sababu ya kuchukua hatua za dhati na za makusudi za kisera pamoja na kuhakikisha utekelezwaji wa sera hizo Kuelekea uchumi wa viwanda. Tanzania yenye kila aina ya tunu (Natural Endowments), ni aibu kwa taifa hili lenye utajiri wa rasilimali za ina zote, miaka zaidi ya 60 tokea uhuru wa Tanganyika na zaidi ya miaka 55 tokea kuundwa kwa serikali ya muungano ya Tanzania, lakini bado Tanzania ni miongoni mwa nchi masikini duniani kwa kuwa na changamoto za miundombinu (inadequate infrastructures), elimu, afya, maji, nishati, na usafiri.

Kwenye hili pamoja na jitihada serikali ambazo inazichukua, lakini bado haiwezi kujivua kwenye mzigo wa lawama kwani maamuzi ya serikali (Political Decisions) hasa ya kisera, mipango pamoja na utekelezaji wa sera na mipango hiyo ndio huamua ufanisi na maendeleo ya maeneo mengine ya ambayo ndio chachu ya ukuaji na maendeleo ya uchumi pamoja na ustawi wa jamii.

Tukirudi kwenye uchumi wa Viwanda, serikali inahitaji muendelezo wa kisera na Dira (policy consistency) ya maendeleo ya nchi, kwani kama kila awamu itakuja na sera zake ambazo mara nyingi utekelezaji wake haukamiliki katika kipindi cha awamu husika, Tanzania miaka nenda rudi haitaweza piga hatua kiuchumi (significant economic movement). Katika kuhakikisha muendelezo wa kisera na dira ya maendeleo ya nchi, Tanzania inahitaji kufanya maboresho ya kitaasisi (institutional stability reforms), hii itasaidia hata kumuongoza Raisi yeyote atakaepewa jukumu na dhamana ya kuingoza Tanzania kuweza kuzisimamia vyema sera na Dira ya maendeleo katika kipindi chake cha uongozi.

Tanzania katika kuelekea mageuzi ya kiuchumi kwa kuwa nchi ya viwanda inahitaji uwekejazi mkubwa katika maeneo ya usafirishaji, nishati, kilimo na Elimu. Hii haina maana kwamba maeneo mengine yapuuzwe, ila kwa kiasi kikubwa uchumi wa viwanda inategemea sana afanisi na ubora wa maeneo hayo.

Kilimo ni sekta muhimu sana inayochochea maendeleo ya viwanda kwani husaidia upatikanaji wa malighafi (raw materials) lakini pia ni sekta muhimu inayotoa soko la bidhaa za viwandani kama mbolea, zana za kulimia na kumwagilia. Serikali katika bajeti yake ya mwaka 2022/2023 imeitengea wizara ya Kilimo kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 900 kutoka shilingi bilioni 294 kwenye bajeti ya mwaka 2021/2022, uamuzi huu ni wa kimkakati na wa kupongezwa sana kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwani ni hatua muhimu sana itakayoifanya sekta ya kilimo kubeba ile dhana ya kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania.

Sera na mipango ielekezwe katika kuvutia uwekezaji mkubwa wa ndani na wa nje(Domestic and Foreign Direct Investment) katika sekta ya kilimo hasa kwenye mazao ya biashara na ya kimkakati kama vile korosho, pamba, kahawa, katani chai, alizeti, na tumbaku, lakini pia kwa kwa kuwawezesha wakulima na wawekezaji kwa kuwapa ruzuku hasa katika mazao ya kimkakati ili kufikia kiwango cha kukidhi mahitaji ya ndani na pia kushiriki kikamilifu katika biashara ya kimataifa hasa bidhaa za viwandani ili kuongeza mnyororo wa thamani (chain of value) wa bidhaa. Uwekezaji wenye tija katika sekta ya kilimo utasaidia katika masuala ya ajira lakini pia katika kuhakikisha upatikanaji wa muda wote Wa bidhaa muhimu kama sukari, ngano na mafuta ya kupikia ambazo mara kwa mara zimekuwa zikipatikana kwa shida au kwa bei ambayo ya juu sana inayopelekea kuzorota kwa baadhi ya shughuli nyengine za uzalishaji hasa wa sekta binafsi.

Nishati nayo ni eneo la kimkakati linalochochea ukuaji wa sekta ya viwanda. Kuelekea uchumi wa viwanda, Tanzania inahitaji kuzalisha na kusambaza nishati kwa kiwango kikubwa. Tanzania yenye vyanzo vikubwa vya maji barani Afrika, gesi ambayo imegundulika katika mikoa ya kusini, lakini bado takwimu zinaonesha asilimia kubwa ya matumizi ya nishati inayotumika majumbani ni nishati ya kuni na mkaa. Serikali inahitaji kuweka nguvu za kutosha katika kufanikisha kukamilika kwa mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere Stegilier’s Gorge hydroelectric power station, kwani kukamilika kwa mradi huu, Tanzania itaweza kushiriki kikamilifu katika kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda.

Eneo la miundombinu ya usafirishaji pia nalo ni la muhimu na la kimkakati litakaloiwezesha Tanzania kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi kupitia uchumi wa viwanda. Kwenye eneo hili serikali ya Tanzania iangalie hasa katika usafiri wa majini na nchi kavu (Land and water transportation). Takwimuzinaonesha kuwa zaidi ya 80% ya biashara za kimataifa hufanyika kupitia usafiri wa majini (maritime transportation), lakini pia kwa jeografia ya Tanzania imeifanya kuwa lango(gate way) kwa kuzihudumia nchi nyengine jirani ambazo hazina bahari (Landlocked countries). Serikila inahitaji jitihada na mipango ya kimkakati katika eneo la bandari ukizingatia kwa ukanda mzima wa Afrika mashariki na kati hakuna nchi inayofanya vizuri sana katika eneo hilo. Upanuzi wa bandari ya Dar es salaam na Tanga lakini pia kufanya majadiliano ya kina na yenye tija juu ya mikataba ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ili kuhakikisha uwezekano wa utekelezaji wake. Kwa upande wa usafiri wa nchi kavu, serikali inahitaji kusimamia kikamilifu utakelezaji wa Reli ya umeme (Standarg Gauge Railway) ambayo itaiunganisha Tanzania na nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC, hii itachochoea ufanisi wa bandari za Tanzania lakini pia kutatua kero ya ajali, gharama na muda wa usafirishaji.

Eneo jengine ambalo linaweza kuisaidia ni ujenzi wa barabara kubwa (highways) zitakazo iunganisha Tanzania na nchi zote jirani pamoja ikizijumuisha nchi za kenya na msumbiji. Barabara zilizopo sasa zinakabiliwa na changomoto nyingi, lakini ujenzi wa barabara kubwa za angalau njia mbili au tatu za kwenda na kurudi itachochea sana maendeleo ya sekta nyengine hasa viwanda na kilimo.

Eneo la Elimu nalo ni la msingi na nyeti sana litakalo hakikisha utekelezaji wa sera ya uchumi wa viwanda. Tanzania kwa asilimia kubwa ina viwanda vinavyozalisha bidhaa za chakula na vinywaji (Food processing and Beverage industries), lakini uchumi wa viwanda ambao unatija ni ule ambao utahakikisha ujenzi wa viwanda vikubwa (heavy industries), utakao zalishabidhaa nyingi za kiushindani kama magari, simu, televisheni na kompyuta. Maendeleo ya viwanda hivyo vinahitaji tekinolojia ya kisasa inayotumika na nchi zilizoendelea.

Serikali ya Tanzania inaweza kuja na sera ya kielimu itakayohakikisha upatikanaji wa rasilimali watu (human resource). Kwa Kupitia mahusiano yake na mataifa makubwa kiuchumi kama Japani, Ujerumani na Uchina, Tanzania inaweza kuja na mkakati wa muda mrefu wa kuwapeleka vijana wa kutoshakatika nchi hizo watakao bobea katika fani zitakazo chochea maendeleo ya viwanda hasa katika maeneo ya uhandisi na uchumi.

Mbwana Kanju Salim (Quantitative Economist)
kanjuchode@gmail.com

0655510642
 
Upvote 3
Back
Top Bottom