Tanzania haimo kwenye nchi 50 zenye amani

Yaani waTz humu mnavosema hatupo top 50 utadhani tupo that far from top 50 wakati hapo sisi Tanzania ni ya 51 kwa dunia nzima, ni ya 8 Afrika ni ya 1 East and Central Africa.....Bado nchi nyingi zinatutegemea likija swala la Amani especially East and Central Africa.

Nchi ambazo kila siku tunahisi ndio nchi za kuzikimbilia kimsaada wa kijeshi na vitu kama hivyoo zenyewe hazina amani hiyo ambayo tunayo Watz..
 
Anayekupandiksha ndo anakushusha, kwa sasa hatutaki sifa za kinafiki tunapambana na hali yetu, viva serikali ya awamu ya tano. Orodha kitu gani watuweke na orodha ya nchi zenye flyover kuonyesha tumepiga hatua au zenye streamline.
kwahiyo lazima muuwe ili muwe na streamliner?
 
Uchumi wenyewe chini ya mzee baba hakuna cha kujivunia. Ni uchumi unaokuwa kwa gharama ya madeni makubwa chini ya sekta ya umma ambapo dunia nzima imeshatoka huko. Ni ulimbukeni utakaoigharimu sana taifa wakati huohuo amani haipo. Nakuambia tutagawana fito nchi hii baada ya muda mfupi tu wa jiwe kumaliza kipindi chake magogoni.
 
Siku hizi wanatengeneza takwimu feki,za kuiondoa Tanzania,bahati mbaya wanajisahau na wao wanajiondoa
Eti sierra leone ina amani kuliko Tanzania!
 

Hahahaha! Mkuu, tulipokuwa UDSM kuna jamaa alirudia mwaka kwa kukosa 1%. Alitakiwa apate 40% ili asirudie mwaka yeye akapata 39%. Lecturer akamwambia ametafuta sehemu ya kumpa hiyo 1% hakuipata!

Sie tunaongelea Tanzania haimo kwenye 50 bora wewe unasema imo kwenye 51!
 
Hakuna kitu kibaya kama kuondoa roho ya Amani tuliyokuwaga nayo watanzania miaka mitatu iliyopita.sasa hivi ni hofu hofu na mashaka tele kila uchwao dah.
 
Wewe ngumbalu kweli. Sasa ulitaka tuseme Tanzania imo wakati taarifa inasema haimo? Hayo mapenzi ya upofu mtajwa fanyiwa kitu mbaya siku moja
 
Marekani wamo?
 
Vipi kuhusu Marekani, Russia, China?
 
Tanzania kanchi kadogo sana kwa influence duniani, hakana impact yoyote. Wamekasahau tu.
Yaani mzungu katengeneza jedwali alafu kajaza nchi za ulaya alafu kuna watu wanapiga vigeregere humu.
ila pia marekani sijaiona.
 
Siioni Marekani. Siioni Kenya. Siioni Uganda. Siioni Uingereza. Siioni China.

Botswana pamoja na deni lao naona wamo.
Nani kakudanganya usa kuna amani? Daily kuna shootings
 
Mbona wanasemaga Tanzania ni nchi ya amani au maana yake ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…