Tanzania haina mufti !,

Tanzania haina mufti !,

Chifu mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2025
Posts
422
Reaction score
489
TANZANIA HAINA MUFTI !
TANZANIA HANA SHEKH MKUU!

Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia kiongozi mkuu wa taasisi ya kidini iitwayo Baraza kuu la waislamu wa Tanzania bara akitajwa kama mufti na sheikh mkuu wa Tanzania na mtazamo huu ni makosa makubwa sana na uamebeba maudhui ya upotoshaji kwa kumvika mtu cheo ambacho kiuhalisia hakipo na hakiwezekani kuwepo kwa sababu zifuatazo;

..... ..........
Sehemu ya mwisho.



NITOE MIFANO.

Ukisema jaji mkuu wa Tanzania tunaelewa kuwa unamzungumzia kiongozi anayewatumikia watanzania wote wa dini , madhehebu, makabila na vyama vyote vya kisiasa na kijamii katika sekta ya mahakama chini ya wizara ya katiba na sheria Tanzania nzima.
Ukisema mkuu wa mkoa wa Mwanza unamaanisha mtu anayemuwakilisha mh Rais katika mkoa wa Mwanza akiwa mtumishi wa watu wa dini, madhehebu, makabila na vyama vyote!.
Ukisema mwenyekiti wa CCM taifa, mkoa au wilaya tunajua unamzungumzia kiongozi wa chama maalumu cha siasa anayewaongoza wanachama wa chama hicho katika nafasi iliyotajwa na sio kiongozi wa watanzania wote.
Upande wa taasisi za kidini ni hivyo hivyo lazima itajwe taasisi hiyo na nafasi ya kila muhusika.
Nimetoa mifano ya taasisi za kikristo hapa Tanzania zinavyowatambulisha viongozi wake.
Ni BAKWATA PEKE YAKE ambayo viongozi wake utasikia MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA.
JE ni mtumishi wa watanzania wote kama ilivyo JAJI MKUU WA TANZANIA?!
Je Mufti wa Tanzania anafanya kazi chini ya wizara gani na kwa sheria gani?!
Ili kuweka mambo sawa kuna nukta zifuatazo .

A. Kwakuwa taasisi hii haina wala haitakiwi kuwa na ofisi Zanzibar kwa kuwa Tayari waislamu wa zanzibar wanayo taasisi inayosimamia mambo yao ya kidini chini ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar jina la taasisi hii yatakiwa liwe BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANGANYIKA
( au Tanzania bara)

B. Yatakiwa kiongozi wao mkuu ajulikane kama MUFTI NA SHEIKH MKUU WA BAKWATA na siyo mufti na sheikh mkuu wa Tanzania.

C. Viongozi wa bakwata mikoani, wilayani na ngazi ya kata wajulikane kama sheikh wa BAKWATA mkoa fulani au sheikh wa BAKWATA wilaya fulani au sheikh wa BAKWATA kata fulani kama vile kisiasa tunaposikia kwamfano mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha , mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Temeke.

Ukisema mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga watu watadhani labda unamkusudia mkuu wa mkoa au hawatoelewa unamzungumzia mtu mwenye majukumu ya aina gani!
Ukisema pia Askofu wa mkoa wa Shinyanga pia huwezi kueleweka unamkusudia mtu wa aina gani kwa sababu katika nafasi za utumishi serikalini hakuna nafasi ya askofu.
Na pia ukisema sheikh wa mkoa wa Shinyanga pia hueleweki kwa sababu serikali haina nafasi ya sheikh katika utumishi wake kwa uma.
Lakini ukisema mwenyekiti wa chadema mkoa wa Shinyanga unaeleweka vizuri kuwa unamkusudia kiongozi wa chama maalumu cha siasa kati ya vyama vingi katika mkoa huo.
Pia ukisema Askofu wa jimbo katoliki jimbo la Shinyanga unaeleweka pia kuwa unamkusudia kiongozi wa kanisa maalumu kati ya makanisa mengi katika nafasi ya jimbo katika mkoa huo.
Na ukisema Sheikh wa BAKWATA mkoa wa Shinyanga pia unaeleweka kuwa unamkusudia kiongozi wa taasisi maalumu ya kiislamu kati ya taasisi nyingi katika mkoa huo.

TANZANIA HAINA MUFTI , TANZANIA HAINA SHEIKH MKUU.

Mwisho.

Makala hii imeandikwa na mimi

Abuu Ibraahiym Sibomana.

Kwa yeyote mwenye nyongeza , ushauri au mawazo tafauti anaweza kuwasiliana nami kupitia namba zifuatazo.

+255 714 525 158.
+255 717 445 411
 
Back
Top Bottom