SoC02 Tanzania haipaswi kuendelea kuitwa nchi Maskini

Stories of Change - 2022 Competition

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
321
Reaction score
691
Kwa ujumla, umaskini ni ile hali ya kukosa mahitaji muhimu kama chakula, maji, makazi, huduma za afya, na elimu.I'm

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikishirikiana na Idara ya Kuondoa Umaskini ya Wizara ya Fedha na Mipango mwaka 2017 – 18 unaonyesha kuwa wastani wa matumizi ya kaya moja kwa mwezi kwa Tanzania Bara ni shilingi 416,927. Kiwango hiki cha matumizi ni kikubwa kwa maeneo ya mijini (TZS 534,619) kuliko maeneo ya vijijini (TZS 361,956). Pia, utafiti unaonyesha kwamba umaskini wa mahitaji ya msingi umepungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011-12 hadi asilimia 26.4 mwaka 2017-18. Vile vile, kiwango cha umaskini wa chakula kimepungua kutoka asilimia 9.7 mwaka 2011-12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017-18. Kwa maoni yangu, bado kiwango cha umaskini kinapungua kwa kasi ndogo, sana ukilinganisha na jitihada nyingi zinazofanywa.

Meneja Takwimu za Pato la Taifa Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Daniel Masolwa alinukuliwa na gazeti la Mtanzania la Novemba, 2016 akisema; licha ya taarifa za Benki ya Dunia (WB) kuonyesha kuwa pato la chini zaidi kwa mtu mmoja kwa mwaka linapaswa kuwa dola za Marekani 3,000, kwa hapa nchini pato hilo ni kati ya dola 900 na 1,000, hali inayotajwa kusababisha Watanzania wengi kulalamikia ugumu wa maisha.

Hata hivyo, jamii za vijijini Tanzania bara na visiwani (Zanziba) zimeathirika zaidi. Kwa mujibu wa taarifa ya UNICEF (2016), pengo hili, kati ya jamii za mijini na vijijini, ndio sababu muhimu inayopelekea umaskini wa mtoto katika maeneo ya vijijini, ambapo asilimia 48 wanakosa mahitaji ya msingi, ukilinganisha na asilimia 10 ya wenzao wanaoishi mijini.

Watoto kutoka katika moja ya Familia za vijijini Tanzania
Familia maskini Tz Aug.jpg

Picha kwa hisani ya ukurasa wa Facebook wa Tanzania Yetu

Watoto kutoka katika moja ya Familia za vijijini Tanzania
Familia maskini Tz Aug 2022 II.jpg

Picha kwa hisani ya ukurasa wa Facebook wa Tanzania Yetu

Rasilimali Tulizojaliwa
Rasilimali hizi ni pamoja na ardhi yenye rutuba, mvua za kutosha (ingawa kwa sasa mvua hazinyeshi kwa utaratibu uliozoeleka kutokana na mabadilio ya tabia nchi), na watu ambao ni wengi zaidi katika maeneo ya mashambani (vijijini); vijiji vingi vina rasilimali nyingi, kama madini mbalimbali yenye thamani kubwa, gesi asili, misitu ya asili, mito, mabwawa asili ya maji, maziwa na bahari.

Usadizi wa Kifedha kutoka Jumuiya ya Kimataifa
Nchi zilizoendelea pamoja na taasisi za fedha za kimatai fa zimekuwa zikitoa mabilioni ya dola za kimarekani kwa miongo mingi ili kusaidia mifumo ya serikali kusisimua uchumi na kuleta maendeleo, lakini bado jitihada hizi hazijaweza kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kiwango cha kuridhisha. Tumekuwa na mikakati mingi ya kukuza uchumi, ambayo imekuwa ikifadhiliwa na jumuiya za kimataifa (kama nilivyotaja hapo juu), nitataja michache kama ifuatavyo: MKUKUTA (Mkakati wa Kukuza uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania), MKURABITA (Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania), Maendeleo Endelevu ya Milenia [2016 – 2030] ( yameridhiwa kutoka Umoja wa Mataifa), na Kilimo Kwanza. Pamoja na mikakati yote hii, uchumi umeshindwa kuongeza vya kutosha kasi ya kuondoa umaskini.

Nini kifanyike?
Kilimo bado ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania, kutokana na ukweli kwamba zaidi ya asilimia 80 ya watu wake wapo mashambani na maisha yao kwa kiasi kikubwa yanategemea kilimo. Kilimo kiimarishwe kuanzia ngazi ya kaya, kiwe cha umwagiliaji, badala ya kuendelea kutegemea mvua.

Serikali ipeleke wataalamu kujifunza katika nchi za Asia, hasa India ambapo wamefanikiwa sana katika kilimo cha umwagiliaji kwa gharama nafuu. Nimebahatika kutembelea India, maeneo mbalimbali ya mashambani, nikajionea wakulima wa kawaida wakifanya kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia visima vya kawaida. Kilimo hiki (ambacho kinashirikisha watu wengi) kimeifanya India kujitosheleza kwa chakula na hata kuuza kiasi kikubwa nje ya nchi. Maeneo mengi nchini India ni kame, lakini wakulima wanavuna maji ya mvua chache zinazonyesha kila mwaka na kuyatumia katika kilimo wakati wa kiangazi. Tanzania tuna vyazo vingi sana vya maji vinavyowezesha upatikanaji wa maji ya kutosha kufanya kilimo cha umwagiliaji mwaka mzima katika wilaya karibu zote. Endapo taifa litaimarisha sekta ya kilimo, itachangia ukuaji wa sekta ya viwanda, na hivyo kufikia malengo ya nchi ya kupunguza umaskini kwa kila mwananchi kwa haraka.

Sambamba na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji, ni vyema wakulima (hasa wale wadogo) kuwezeshwa kutumia zana za kisasa. Nchini India, mkulima wa kawaida anayemiliki ekari tatu, analima kwa trekta, anapalilia kwa trekta, na anavuna kwa mashine (“Combine Harvester”).

Vyama vya ushirika viimarishwe, ili viweze kuhudumia vyema wanachama wake (hasa wakulima – kuuza mazao kwa bei nzuri, kupata zana na pembejeo za kilimo kwa wakati, nk)

Serikali iangalie upya utaratibu wa kutoza kodi kwa wawekezaji wa Tanzania, kuanzia ngazi ya chini. Naamini serikali inakosa mapato mengi sana, kutoka kwa wafanyabiashara wengi wadogowadogo ambao hawapo katika mfumo rasmi. Ukihitaji leseni ya biashara, hata kama ni ndogo kiasi gani, utalazimika kulipa kiasi kisichopungua elfu 90 shilingi za kitanzania kwa halmashauri ya wilaya/mji/manispaa/jiji, na shilingi 120,000 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, kabla ya kufanya biashara; jumla ikiwa ni zaidi ya shilingi laki mbili. Hiki ni kiasi kikubwa sana kwa mtu mwenye mtaji wa kiasi kisichozidi shilingi elfu 50. Hii ndio sababu inayofanya watu wengi kushindwa kupata leseni za biashara na kujikuta wanafanya biashara mitaani kwa muda mrefu (maarufu kama Machinga). Kumbe serikali ingeweza kutoa vibali hivi bure, na wafanyabiashara wakawa wanalipa mamlaka husika kila mwezi, kuendana na mapato yao. Hii ingenufaisha pande zote, serikali (ingepanua wigo wa kodi) na wafanyabiashara (wangekuwa wanafanya biashara rasmi ambazo zingewawezesha kutambuliwa na taasisi za fedha, na kukopesheka).

Serikali ifanye mdahalo wa kitaifa na wadau mbalimbali kuhusu namna Mtanzania anaweza kutumia rasilimali tulizonazo kujikwamua kiuchumi na kuchangia uchumi wa taifa kwa ujumla.

Serikali pamoja na wadau wengine, iangalie upya mitaala ya elimu, ili iweze kuandaa wahitimu wa ngazi mbalimbali kuweza kutumia rasilimali tulizonazo kukuza uchumi.

Hitimisho
Tuna rasilimali zote zinazohitajika kufanya mapinduzi ya kiuchumi, bila kuhitaji msaada mkubwa kutoka nje ya nchi.

Rejea
Gazeti la Mtazania (Novemba, 2016), Kipato cha Mtanzania kwa Mwaka ni Dola 900.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Tanzania (2022), Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya
Binafsi kwa Tanzania Bara wa Mwaka 2017-18.

Taarifa ya Unicef (Septemba, 2009), "Childhood Poverty in Tanzania: Deprivations and Disparities in Child Well-Being"
 
Upvote 13
Ni kweli tuna rasilimali za kutosha na tunaweza kujinasua na umaskini kama tukizitumia ipasavyo
Mwaka 2012, Juni, niliandika makala kuhusu umaskini nchini Tanzania, nikachapisha katika ukurasa wa "Wikipedia", Inasomeka "Poverty in Tanzania"; ina habari nyingi kuhusiana na dhana ya umaskini.
 
Mimi nikisema hili andiko ulio tuletea umecopy siyo lako na nilàmwaka 2014 nitakuwa nakosea. !!

Kwani hakuna ripoti za NBC, WB za mwaka 2022 ?, inamaana wewe ulilala mwaka 2012 ukaja ukaamikia 2022 bila kujua takwimu zimebadirika Kwani sasa hivi unajua tupo mwaka gani ?

Huwenda hata mwaka tuliopo ujui na Hili andiko siyo lako ukitaka nikuonyeshe ripoti za NBS na WB za mwaka 2022 ambazo post yako uliyo copy kutoka 2012 hazina ?
 
Ndo maana kuna rejea pale mwishoni, angekua ajaweka rejea ndo tungesema amefanya plagiarism (Kuibia).
 
Kwani hakuna ripoti za mwaka 2022 za NBC, unajua hili shindano mimi lazima nimpime mtu anacho ongea kwamba kime mgusa au amejiandikia tu kwa andiko hili ajakaa akaandika vitu ambavyo ametumia akili yake hila amecopy sehemu.
 
Mimi nikisema hili andiko ulio tuletea umecopy siyo lako na nilàmwaka 2014 nitakuwa nakosea. !!

Kwani hakuna ripoti za NBC, WB za mwaka 2022 ?, inamaana wewe ulilala mwaka 2012 ukaja ukaamikia 2022 bila kujua takwimu zimebadirika Kwani sasa hivi unajua tupo mwaka gani ?

Huwenda hata mwaka tuliopo ujui na Hili andiko siyo lako ukitaka nikuonyeshe ripoti za NBS na WB za mwaka 2022 ambazo post yako uliyo copy kutoka 2012 hazina ?
Ndio, umekosea! Soma makala kwa umakini, ndio utoe maoni yako, sijatoa takwimu za 2012 wala za 2014!
 
Kwani hakuna ripoti za mwaka 2022 za NBC, unajua hili shindano mimi lazima nimpime mtu anacho ongea kwamba kime mgusa au amejiandikia tu kwa andiko hili ajakaa akaandika vitu ambavyo ametumia akili yake hila amecopy sehemu.
Kama unazo takwimu za 2022, ni vyema uzitoe kwa faida ya wote, kwasababu hapa tunajenga na sii kubomoa.
 
Ni kweli tuna rasilimali za kutosha na tunaweza kujinasua na umaskini kama tukizitumia ipasavyo
Moja ya rasilimali muhimu ambayo inaweza kubadilisha kabisa uchumi wa Tanzania, ni gesi iliyogunduliwa kule Mtwara. Kama ikitumika vizuri, itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza petroli nje ya nchi; lakini pia itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya misitu kama chanzo kikuu cha nishati kwa baadhi ya viwanda na kaya nyingi nchini.
 
Na pia kwa kuongezea mazingira yetu yatakuwa safi na salama kama matumizi ya gesi yataongezeka.
 
Tunaweza kujikwamua kiuchumi endapo serikali na wadau wengine watagundua vipaji vilivyomo ndani (nchini) na kuvitumia. Wananchi wa kawaida wakipewa nafasi wanaweza kubadili uchumi wa nchi bila kutegemea wawekezaji kutoka nje. Wawekezaji wa nje wanaweza kuingia ubia na wazawa, ikiwa wazawa wamewezeshwa kumiliki rasilimali!
 
Kwa ujumla, umaskini ni ile hali ya kukosa mahitaji muhimu kama chakula, maji, makazi, huduma za afya, na elimu.I'm

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikishirikiana na Idara ya Kuondoa Umaskini ya Wizara ya Fedha na Mipango mwaka 2017 – 18 unaonyesha kuwa wastani wa matumizi ya kaya moja kwa mwezi kwa Tanzania Bara ni shilingi 416,927. Kiwango hiki cha matumizi ni kikubwa kwa maeneo ya mijini (TZS 534,619) kuliko maeneo ya vijijini (TZS 361,956). Pia, utafiti unaonyesha kwamba umaskini wa mahitaji ya msingi umepungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011-12 hadi asilimia 26.4 mwaka 2017-18. Vile vile, kiwango cha umaskini wa chakula kimepungua kutoka asilimia 9.7 mwaka 2011-12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017-18. Kwa maoni yangu, bado kiwango cha umaskini kinapungua kwa kasi ndogo, sana ukilinganisha na jitihada nyingi zinazofanywa.

Meneja Takwimu za Pato la Taifa Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Daniel Masolwa alinukuliwa na gazeti la Mtanzania la Novemba, 2016 akisema; licha ya taarifa za Benki ya Dunia (WB) kuonyesha kuwa pato la chini zaidi kwa mtu mmoja kwa mwaka linapaswa kuwa dola za Marekani 3,000, kwa hapa nchini pato hilo ni kati ya dola 900 na 1,000, hali inayotajwa kusababisha Watanzania wengi kulalamikia ugumu wa maisha.

Hata hivyo, jamii za vijijini Tanzania bara na visiwani (Zanziba) zimeathirika zaidi. Kwa mujibu wa taarifa ya UNICEF (2016), pengo hili, kati ya jamii za mijini na vijijini, ndio sababu muhimu inayopelekea umaskini wa mtoto katika maeneo ya vijijini, ambapo asilimia 48 wanakosa mahitaji ya msingi, ukilinganisha na asilimia 10 ya wenzao wanaoishi mijini.

Watoto kutoka katika moja ya Familia za vijijini Tanzania
View attachment 2324678
Picha kwa hisani ya ukurasa wa Facebook wa Tanzania Yetu

Watoto kutoka katika moja ya Familia za vijijini Tanzania
View attachment 2324679
Picha kwa hisani ya ukurasa wa Facebook wa Tanzania Yetu

Rasilimali Tulizojaliwa
Rasilimali hizi ni pamoja na ardhi yenye rutuba, mvua za kutosha (ingawa kwa sasa mvua hazinyeshi kwa utaratibu uliozoeleka kutokana na mabadilio ya tabia nchi), na watu ambao ni wengi zaidi katika maeneo ya mashambani (vijijini); vijiji vingi vina rasilimali nyingi, kama madini mbalimbali yenye thamani kubwa, gesi asili, misitu ya asili, mito, mabwawa asili ya maji, maziwa na bahari.

Usadizi wa Kifedha kutoka Jumuiya ya Kimataifa
Nchi zilizoendelea pamoja na taasisi za fedha za kimatai fa zimekuwa zikitoa mabilioni ya dola za kimarekani kwa miongo mingi ili kusaidia mifumo ya serikali kusisimua uchumi na kuleta maendeleo, lakini bado jitihada hizi hazijaweza kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kiwango cha kuridhisha. Tumekuwa na mikakati mingi ya kukuza uchumi, ambayo imekuwa ikifadhiliwa na jumuiya za kimataifa (kama nilivyotaja hapo juu), nitataja michache kama ifuatavyo: MKUKUTA (Mkakati wa Kukuza uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania), MKURABITA (Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania), Maendeleo Endelevu ya Milenia [2016 – 2030] ( yameridhiwa kutoka Umoja wa Mataifa), na Kilimo Kwanza. Pamoja na mikakati yote hii, uchumi umeshindwa kuongeza vya kutosha kasi ya kuondoa umaskini.

Nini kifanyike?
Kilimo bado ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania, kutokana na ukweli kwamba zaidi ya asilimia 80 ya watu wake wapo mashambani na maisha yao kwa kiasi kikubwa yanategemea kilimo. Kilimo kiimarishwe kuanzia ngazi ya kaya, kiwe cha umwagiliaji, badala ya kuendelea kutegemea mvua.

Serikali ipeleke wataalamu kujifunza katika nchi za Asia, hasa India ambapo wamefanikiwa sana katika kilimo cha umwagiliaji kwa gharama nafuu. Nimebahatika kutembelea India, maeneo mbalimbali ya mashambani, nikajionea wakulima wa kawaida wakifanya kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia visima vya kawaida. Kilimo hiki (ambacho kinashirikisha watu wengi) kimeifanya India kujitosheleza kwa chakula na hata kuuza kiasi kikubwa nje ya nchi. Maeneo mengi nchini India ni kame, lakini wakulima wanavuna maji ya mvua chache zinazonyesha kila mwaka na kuyatumia katika kilimo wakati wa kiangazi. Tanzania tuna vyazo vingi sana vya maji vinavyowezesha upatikanaji wa maji ya kutosha kufanya kilimo cha umwagiliaji mwaka mzima katika wilaya karibu zote. Endapo taifa litaimarisha sekta ya kilimo, itachangia ukuaji wa sekta ya viwanda, na hivyo kufikia malengo ya nchi ya kupunguza umaskini kwa kila mwananchi kwa haraka.

Sambamba na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji, ni vyema wakulima (hasa wale wadogo) kuwezeshwa kutumia zana za kisasa. Nchini India, mkulima wa kawaida anayemiliki ekari tatu, analima kwa trekta, anapalilia kwa trekta, na anavuna kwa mashine (“Combine Harvester”).

Vyama vya ushirika viimarishwe, ili viweze kuhudumia vyema wanachama wake (hasa wakulima – kuuza mazao kwa bei nzuri, kupata zana na pembejeo za kilimo kwa wakati, nk)

Serikali iangalie upya utaratibu wa kutoza kodi kwa wawekezaji wa Tanzania, kuanzia ngazi ya chini. Naamini serikali inakosa mapato mengi sana, kutoka kwa wafanyabiashara wengi wadogowadogo ambao hawapo katika mfumo rasmi. Ukihitaji leseni ya biashara, hata kama ni ndogo kiasi gani, utalazimika kulipa kiasi kisichopungua elfu 90 shilingi za kitanzania kwa halmashauri ya wilaya/mji/manispaa/jiji, na shilingi 120,000 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, kabla ya kufanya biashara; jumla ikiwa ni zaidi ya shilingi laki mbili. Hiki ni kiasi kikubwa sana kwa mtu mwenye mtaji wa kiasi kisichozidi shilingi elfu 50. Hii ndio sababu inayofanya watu wengi kushindwa kupata leseni za biashara na kujikuta wanafanya biashara mitaani kwa muda mrefu (maarufu kama Machinga). Kumbe serikali ingeweza kutoa vibali hivi bure, na wafanyabiashara wakawa wanalipa mamlaka husika kila mwezi, kuendana na mapato yao. Hii ingenufaisha pande zote, serikali (ingepanua wigo wa kodi) na wafanyabiashara (wangekuwa wanafanya biashara rasmi ambazo zingewawezesha kutambuliwa na taasisi za fedha, na kukopesheka).

Serikali ifanye mdahalo wa kitaifa na wadau mbalimbali kuhusu namna Mtanzania anaweza kutumia rasilimali tulizonazo kujikwamua kiuchumi na kuchangia uchumi wa taifa kwa ujumla.

Serikali pamoja na wadau wengine, iangalie upya mitaala ya elimu, ili iweze kuandaa wahitimu wa ngazi mbalimbali kuweza kutumia rasilimali tulizonazo kukuza uchumi.

Hitimisho
Tuna rasilimali zote zinazohitajika kufanya mapinduzi ya kiuchumi, bila kuhitaji msaada mkubwa kutoka nje ya nchi.

Rejea
Gazeti la Mtazania (Novemba, 2016), Kipato cha Mtanzania kwa Mwaka ni Dola 900.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Tanzania (2022), Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya
Binafsi kwa Tanzania Bara wa Mwaka 2017-18.

Taarifa ya Unicef (Septemba, 2009), "Childhood Poverty in Tanzania: Deprivations and Disparities in Child Well-Being"
Nimekupigia Kura Naomba na Mimi unipigie Kura kupitia SoC 2022 - Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa
 
Mojawapo ya vipaumbele vya Rais wa awamu ya kwanza, Hayati Mlm J. K Nyerere ilikuwa ni kupata wasomi wa kutosha, ili waweze kutumia .rasilimali zetu na kuondokana na umaskini! Lengo la kupata wasomi wa kutosha alilitimiza; lakini mpaka sasa, tunahangaika, na hatujaweza kuwatumia hawa wasomi kutumia rasilimali hizi na walau kupunguza umaskini!
 
Back
Top Bottom