pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 10,913
- 13,876
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania mashabiki na wapenzi wote wa mpira Tanzania na Africa mashariki kwa ujumla.
Kama kuna sehemu tunafeli kama taifa ni sehemu ya wachambuzi wetu yaani asilimia kubwa hawana uelewa wa mchezo wa mpira wa miguu wao wanachambua kwa kuangalia upepo na sio uhalisia kwasababu zifuatazo:–
Walimkataa KIBU DENIS kwa kumdharau na kumkejeli mpaka wengine wakaenda mbali kuandika makala za kumponda Ila leo hii wanamuita mkandaji na kumsifia kuanzia national team mpaka kwenye club ya simba.
Wakaja wakahamia kwa AZIZ KI wakasema ni hasara na yanga inatakiwa iachane naye lakini mwisho wa siku alikuja kuwaziba midomo baada ya kuja kocha mpya na leo kila mtu anaona mchango wake yanga.
Wakati simba inamsajili AYOUB LAKRED kila mtu hakutarajia kwamba atakuwa mchezaji mzuri kwasababu alikaa nje mwaka mzima na alipoanza kukaa langoni kila mtu alikuwa na wasi wasi na hakuamini kiwango chake ila anachokifanya sasa hivi kila mtu anaona wachambuzi na mashabiki wamezibwa midomo.
Katika mechi ya SIMBA NA YANGA kila mchambuzi na shabiki alimpa sifa GAMOND baada ya team yake kuibuka na ushindi wa goli 5–1 lakini kinachoendelea sasa hivi kwa mashabiki na wachambuzi wameanza kumponda na kulalamika kutokana na mfumo wake na jinsi anavyochelewa kuusoma mchezo na kufanya maamuzi na wengine wakidai upepo wake umekata.
Baada ya simba kumleta kocha mpya alinza kumpa nafasi ONANA ambaye alionekana kutopata nafasi kwa kocha aliyepita na wachambuzi na mashabiki kuanza kulalamika na kudai ni mzigo ila alichokifanya kwenye mechi mbili baada ya kuja kocha mpya kila mtu ameona na ameanza kubadilka wachambuzi wamebaki midomo wazi hawana la kuongea.
Watanzania wengi ni bendera fuata upepo wanaendeshwa na matukio yaani hawaumizi kichwa wakimkataa mtu wanamkataa mazima bila kuweka akiba ya maneno.
Remember failure is a condition and not a person and acquired characteristics can't be inherited always remember this quote.
Usimkatie mtu tamaa as long as he/she is alive.
Alamsik.