Tetesi: Tanzania hatarini kuondolewa AFCON 2025 baada ya kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)

Tetesi: Tanzania hatarini kuondolewa AFCON 2025 baada ya kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu,

Mwandishi wa habari za michezo wa Ghana, Micky Jr ameripoti kuwa, Tanzania inaweza kuondolewa kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco licha ya kufuzu, baada ya kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Pia, Soma:
1732199095979.png
Katika dakika ya 73 ya mechi yao ya kufuzu, Tanzania ilifanya mabadiliko na kumuingiza mchezaji aliyekuwa na jezi namba 26. Hata hivyo, kwenye orodha rasmi ya wachezaji iliyowasilishwa CAF kabla ya mechi, hakukuwa na mchezaji yeyote aliyekuwa ameambatanishwa na namba hiyo ya jezi.
1732199435492.png
Kwenye Media start list Ibrahim Mohamed Ame ambaye ndiye alivaa jezi namba 26 aliorodheshwa na namba 24, ambaye aliingia dakika ya 76 kuchukua nafasi ya Nahodha Mbwana Samatta.
Screenshot 2024-11-21 171132.png

1732198316859.png
 
Tanzania inaweza kuondolewa kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco licha ya kufuzu, baada ya kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Katika dakika ya 73 ya mechi yao ya kufuzu, Tanzania ilifanya mabadiliko na kumuingiza mchezaji aliyekuwa na jezi namba 26. Hata hivyo, kwenye orodha rasmi ya wachezaji iliyowasilishwa CAF kabla ya mechi, hakukuwa na mchezaji yeyote aliyekuwa ameambatanishwa na namba hiyo ya jezi.
Hiyo ni kazi ya nani TFF ama benchi la ufundi?
 
Na iwe hivyo(waenguliwe) ili walau wapate ile feeling iliyowakuta wagombea wa upinzani serekali za mtaa.

Yaani mtu amekosea kidogo tu kujaza fomu mkamuengua eti amekua disqualified.

Haya sasa na nyie mmeingiza namba 26(Disqualified *****)na hayupo kwenye list

MKUKI KWA NGURUWE
 
No26 alikuwa nani huyo
 
Back
Top Bottom