Tanzania hatujawahi kulala njaa kwa kukosa mkopo dhidi ya COVID-19, woga na tamaa ndiyo itakayotumaliza

IMF imeitega Tz Kwa kutaka kuipa mkopo wa kupambana na C - 19 na kuielekeza jinsi inapaswa ifanye ili ipewe huo mkopo

Ok, pale mwenye nacho anapotaka kumyang'anya zaidi mwenye kidogo, na Masikini

Mtu jasiri akitaka kurogwa na Mchawi huanza kwa kutishiwa tishiwa, mara sijui kesho hutaiona, mara sijui nitakufanya hiki na kile ili tu amwondolee ujasiri wake, amtie hofu na iwe vyepesi kwake kurogeka.

Maneno meeengi, na kikawaida, mtu hurogeka pindi anapokuwa amejawa na hofu ya kurogwa, hofu ya maisha ya itakuwaje sasa, mtu huyo ni rahisi saana kurogeka

Kukubali mkopo wa IMF na masharti yake, kisa tu tukabiriane na ugonjwa hewa wa Corona nchini, ni kumruhusu shetani mla watu kwamba, tuko tayari afanye atakavyo kufanya, kwani tnaona huko Kwa wenzetu mambo yalivyo, baada tu ya kutiwa hofu na wakakubali kupewa mikopo hii

Jambo la kujiuliza, Je, mpaka sasa, ni Kweli Tanzania tumeathirika mno kiasi cha kuhitaji msaada wa kifedha za masharti ambayo ndiyo yanayoambatana na maambukizi ya Corona kwa kasi kubwa?

Tanzania hatujawahi kufa njaa kwa sababu ya kutokukopa fedha za IMF ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Ila nina uhakika, endapo tukikubali kuingia huu mtego wa fedha hizo, Corona itasambaa kwa kasi ya ajabu!

Kwanza, tutakuwa tumefanya uongo Mbele za Mungu kusema, tumeathirika mno na tunahitaji msaada huo na wakati kila kitu Kinafanyika bila zingatio lolote!

Tanzania, Tumepewa nafasi nzuri Sana na Mwenyezi Mungu wa kujifunza kutoka mataifa mengine yaliyopokea misaada hiyo pamoja na kufuata masharti yake jinsi ambavyo watu wake walivyotabika, na bado tumeendelea kujifunza tena Kwa mataifa ambayo yaliyoanza kupokea chanjo,

Kwa hiyo Sisi kama nchi, tusiishie tu kupata somo kutoka Kwa mataifa mengine na somo Hilo lisitusaidie na kufanya tena kama walivyofanya wao. Itakuwa ni ujinga

Tunahitaji kufanya tofauti na wao

Mungu ibariki na kuilinda nchi yetu Tanzania
Kuna jamaa mmoja hivi alikuwa majukwaani anatuambia kuwa hataki mikopo ya corona lakini ajabu kuna siku wenye kutoa hiyo mikopo walitaka kujua pesa yao imetumikaje. Sasa kama ulitaka kumnanga Mama, tunaomba uanze na yule aliyechukua hiyo pesa kimya kimya huku majukwaani akituzuga kuwa hataki
 
Kwani mwenda zake hakuchukua pesa za watu kwaajili ya kujikinga na athari za koona? Au kisa yeye alizipiga kimya kimya Mama kaweka wazi?
 
Tungejifunza toka Kenya, walikimbilia kuchukua mikopo viongozi wao wakaifisadi huku deni la nchi likiongezeka.
heri mwaka 2025 ufike haraka tufanye uchaguzi wa rais.
 
Vipi lakini, hii mikopo imeleta tija sasa?
Unadhani tukikopa sasa itasaidia nini?
 
R.I.P Magufuli

Ulikataa lock down kwa watanzania licha ya chadema kukimbia bunge na kwenda kukaa lockdown kuogopa corona .
Ila kumbuka Mwendazake alichukua pesa kutoka EU kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona usiokuwepo
 
Tungejifunza toka Kenya, walikimbilia kuchukua mikopo viongozi wao wakaifisadi huku deni la nchi likiongezeka.
heri mwaka 2025 ufike haraka tufanye uchaguzi wa rais.
Uchaguzi hadi 2035,, kwasasa muacheni mama Ainyooshe nchi, na awanyooshe majambazi wa Lumumba
 
Umasikini ni kitu cha kupiga vita saana, Kilichofanywa na IMF ni kutupaka utamu mdomoni ili kuona kama tutaweza kuishinda tamaa ya chakula hicho

Lakini, ukweli wake ni kwamba, mikopo yote iliyotolewa Kwa kusudi la kupambana na Corona, ni kama ilikuja kusambaza Corona Kwa Kasi katika nchi husika
Huu siyo umasikini wa kipato, ni umasikini wa akili!

Huyu mama hata kuiga mazuri ya JPM hataki, anajiendea tu kama mpira
 
Hapo ni big No..watasema tujifungie,barakoa za nguo No,hakuna kunywa dawa zetu za asili.... Hizo fedha ziboreshe maeneo mengine hasa kilimo
 
Buana weee wasiache kitu eachukue waje waendeleze miradi kibap maji umeme afya tunazihitajiiii achana na kujidai donor country
 
Si tutakuwa tunafanya uwongo mkuu
 
Magufuli alipewa grant sio loan na EU alizichukua akafanyia vitu vya maana. Miradi ya kimkakati. Miundombinu.

Huo mkopo labda utatumika kununua COVID-19 vaccine. IMF siku zote wana masharti magumu sana na wanakueleleza utumie hizo pesa wapi na wanafuatilia.

Wakitaka watupe bure hizo vaccine and grants. Zitumike kuboresha miundombinu ya hospitali zetu, kwa kununua vifaa vinavyoweza kuokoa maisha ya wengi mashine za kupumulia, ct scan, lab, etc

😁😁Mkopo wa posho 🤪🤪.

Hongera mkuu,kweli huu mkopo kwanza sio wa lazima,wakitaka watupe msaada na sio mkopo
 
IMF imeitega Tz Kwa kutaka kuipa mkopo wa kupambana na C - 19 na kuielekeza jinsi inapaswa ifanye ili ipewe huo mkopo

Ok, pale mwenye nacho anapotaka kumyang'anya zaidi mwenye kidogo, na Masikini

Mtu jasiri akitaka kurogwa na Mchawi huanza kwa kutishiwa tishiwa, mara sijui kesho hutaiona, mara sijui nitakufanya hiki na kile ili tu amwondolee ujasiri wake, amtie hofu na iwe vyepesi kwake kurogeka.

Maneno meeengi, na kikawaida, mtu hurogeka pindi anapokuwa amejawa na hofu ya kurogwa, hofu ya maisha ya itakuwaje sasa, mtu huyo ni rahisi saana kurogeka

Kukubali mkopo wa IMF na masharti yake, kisa tu tukabiriane na ugonjwa hewa wa Corona nchini, ni kumruhusu shetani mla watu kwamba, tuko tayari afanye atakavyo kufanya, kwani tnaona huko Kwa wenzetu mambo yalivyo, baada tu ya kutiwa hofu na wakakubali kupewa mikopo hii

Jambo la kujiuliza, Je, mpaka sasa, ni Kweli Tanzania tumeathirika mno kiasi cha kuhitaji msaada wa kifedha za masharti ambayo ndiyo yanayoambatana na maambukizi ya Corona kwa kasi kubwa?

Tanzania hatujawahi kufa njaa kwa sababu ya kutokukopa fedha za IMF ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Ila nina uhakika, endapo tukikubali kuingia huu mtego wa fedha hizo, Corona itasambaa kwa kasi ya ajabu!

Kwanza, tutakuwa tumefanya uongo Mbele za Mungu kusema, tumeathirika mno na tunahitaji msaada huo na wakati kila kitu Kinafanyika bila zingatio lolote!

Tanzania, Tumepewa nafasi nzuri Sana na Mwenyezi Mungu wa kujifunza kutoka mataifa mengine yaliyopokea misaada hiyo pamoja na kufuata masharti yake jinsi ambavyo watu wake walivyotabika, na bado tumeendelea kujifunza tena Kwa mataifa ambayo yaliyoanza kupokea chanjo,

Kwa hiyo Sisi kama nchi, tusiishie tu kupata somo kutoka Kwa mataifa mengine na somo Hilo lisitusaidie na kufanya tena kama walivyofanya wao. Itakuwa ni ujinga

Tunahitaji kufanya tofauti na wao

Mungu ibariki na kuilinda nchi yetu Tanzania

Mkupo ni mzuri kama una riba nzuri ya chini sana na kuna sababu ya kuchukuwa pesa. Hivyo huwezi kuongelea mkopo mzuri au mbaya bila kujua riba. Kama mkopo ni muda mrefu mfano miaka 10 kwa riba 1% ni kwanini tusichukuwe badala ya kukopa ndani kwa riba ya 10% na kupunguza pesa kwenye mzunguko. Pesa ya miradi ya umeme, reli au upanuaji wa bandari tukipata kwa riba ya chini tuchukuwe
 
Kwani hadi unaitwa mkopo, mkopaji anaitwa kwenda kuchukua au anaomba tena kwa masharti magumu?

Danganyeni mamburula wenzenu.

Ukweli ni kuwa takwimu ni haki yetu. Kwa sisi kupewa takwimu kuna pia incentive ya mkopo.

Shida iko wapi hapo?

Au hofu ya uwepo wa mwendazake ingalipo?
Hii inaitwa, tawala mawazo yako! Unachokiamini kishike, Ila ukweli tusiukwepe, Hatujaathirika kiasi cha kuhitaji mikopo inayofuatana na covd ndani yakeu
Your head need to be examined
Kivipi, umeona nini kwake
 
Buana weee wasiache kitu eachukue waje waendeleze miradi kibap maji umeme afya tunazihitajiiii achana na kujidai donor country
Eee Bhana eeeh!!

Kwa hiyo waiongopee IMF ili waje kufanya tofauti na walichokiombea siyo?😛
 
Mkupo ni mzuri kama una riba nzuri ya chini sana na kuna sababu ya kuchukuwa pesa. Hivyo huwezi kuongelea mkopo mzuri au mbaya bila kujua riba. Kama mkopo ni muda mrefu mfano miaka 10 kwa riba 1% ni kwanini tusichukuwe badala ya kukopa ndani kwa riba ya 10% na kupunguza pesa kwenye mzunguko. Pesa ya miradi ya umeme, reli au upanuaji wa bandari tukipata kwa riba ya chini tuchukuwe
Mkuu, mkopo unaotolewa unaelekezwa ukafanye nini na eneo gani, ndio Maana nasema, umasikini ni kitu cha kupiga vita Kwa kila khali
 
Hii inaitwa, tawala mawazo yako! Unachokiamini kishike, Ila ukweli tusiukwepe, Hatujaathirika kiasi cha kuhitaji mikopo inayofuatana na covd ndani yakeu

Kivipi, umeona nini kwake

Kwani mkopo waja vipi yakhe si twakwenda wenyewe kuuomba?

IMG_20210610_140144_633.jpg

Kwani kuupata mkopo benki hata kwa mtu kazi ndogo?
 
Mkuu, mkopo unaotolewa unaelekezwa ukafanye nini na eneo gani, ndio Maana nasema, umasikini ni kitu cha kupiga vita Kwa kila khali

Nisiache kukupa nukuu hii ya leo tokea kwa waziri wa fedha bajeti ya serikali 2021/22. Kwenye red kuna husika:

IMG_20210610_181722_190.jpg

Tunahitaji zaidi mkopo kuliko wanaoutoa wanavyotaka kutupa sisi.

Hiyo ndiyo iliyo habari yenyewe.
 
Back
Top Bottom