Tanzania hatuna wachambuzi

Tanzania hatuna wachambuzi

Football analysis ni course kama course nyingine tatizo Kibongobongo watu wanaichukulia poa..

Nikishakuwa na bando langu, Smartphone na kujua baadhi ya istilahi mfano Low block, double pivot, Pressing, formation n.k basi naweza kujiita mchambuzi

SMH!
 
Habari za jioni wakuu,
Ikiwa umepita mda mchache toka kuanza kwa kikao kikubwa cha soka barani Africa ila kinachoendelea mitandaoni kinasikitisha sana.

Katika tasnia zilizovamiwa Tanzania ukiitoa ile ya Bongo movie basi inafuata tasnia ya michezo tena imejaa vilaza kweli hakuna anayesimamia ukweli wao wanaangalia interest zao na upepo unavuma kuelekea wapi kwasababu zifuatazo:–

Siku za karibuni CAF ilitoa orodha ya vilabu vitakavyoshiriki katika mashindano hayo na hatua zitakazo anzia huku AZAM FC ikiibua maswali mengi kwa hatua itakayoanzia,
kwani hawaanzii hatua ya awali kama team nyingine za Tanzania ila hakuna mchambuzi aliyefuatilia au kufafanua kwa nini wao wenyewe hawajui kama sisi na hakuna anayefuatilia zaidi ya kila mtu kuongea la kwake wao ndio walitakiwa watupe ufafanuzi ila hawajui kitu maajabu haya.

Arusha kuna tukio kubwa linafanyika linalokutanisha wawakilishi wa CAF kutoka sehemu mbali mbali badala ya wachambuzi wetu kutumia fursa hii adhimu kwa interview za watu mashuhuri na kujua undani wa mkutano huo kwa kutupa updates na ufafanuzi wa yanayojiri wao wamekuja na hoja mpya kabisa wakihoji kwa nini yanga hajaalikwa kwenye ghafla hyo kweli mmekosa vya kuzungumza na kuchambua ndio maana karia alisema mrudi shule.

Ukiangalia kuanzia WASAFI FM, CLOUDS FM na E–FM unapata picha tuna wachambuzi wa aina gani wao ni kujadili upuuzi wa simba kuhusu jeneza na mzungu na yanga kumruhusu haji manara kuwa MC ni kweli ni masuala ya mpira na yametokea kwenye vilabu vya mpira ila vinapewa airtime kubwa kuliko main content inayotakiwa wakija kuchambua soka la kimataifa ndo utatamani uzime redio hawana wanachokijua zaidi ya matokeo na takwimu tu.

Hivi ukweli mtu unafikia hatua ya kufanya kazi kampuni kubwa kama clouds fm au AZAM MEDIA halafu lugha gongano yaani haipandi muangalie yule Gift macha pale AZAM juzi wakati akiwahoji makocha baada ya mechi utatamani uzime TV,
sawa hujui basi wanashindwa hata kujiongeza kwa rasi simba maana kazi zao zinawakutanisha watu tofauti tofauti kutoka nchi nyingi wanao ongea lugha mbali mbali si vibaya wachambuzi wetu wajifunze kifaransa na English hilo sio la kuwaambia ni lazima ndo maana baada ya mechi wachambuzi wetu wanakimbia kufanya interview na wageni wanakimbilia kwa wenyeji.

Aibu kubwa hii kuna jamaa anaitwa Patrick nyembera pale AZAM ndo kituko kabisa clouds sitaki hata kuongea maana lwambano na priva baada ya good morning na how are you kinachofuata baada ya hapo ni aibu shafii dauda ndo wale wale.

Wachambuzi wetu wanapaswa wabadilike dunia inaenda kasi sana na technology inabadilika hizi simba na yanga zisiwafanye nyinyi ni kina roy Keane na Thierry Henry kwenye uchambuzi wakati kubadilisha article ya kiingereza tu kwenda kwenye kiswahili wengi wao ni mtihani wanatakiwa wajiongeze kwenye eneo hilo bahasha siziwalemaze akili wakati ni empty kichwani.

NB: Bila kupitisha sheria ngumu hili eneo linaenda kuwa bomu hawa wanasheria wahasibu na afisa ugavi pamoja na walimu warudi kwenye fani zao mpira una wenyewe au warudi shule wakasome.
Kwangu mchambuzi wangu makini ni Tembele Ally mwana wa Mayai.
 
Dah.mwanangu umeongea kitu ambacho kila siku naona tabu hawa waandishi wakiwahoji wageni ni aibu tupu.mpaka aibu naona mimi ninae angalia tv kumuona mtangazaji kabisa anahoji kwa lugha za kuunga unga hawajui kama wanatutia aibu watanzania .tena kuna hizi youtube channel ndio hamna kitu kabisa .yule mtangazaji wa baraka mpenja ndio hamnazo ana swali lake moja hilo hilo la kiingireza anamuuliza kila mtu.Aiseee ni aibu.na kule yule mtangazaji wa shafih dauda mweusi hivi aiseee ni hovyo alafu sijui wenyewe hawajion
 
Tatizo ni kwamba watu bright na wenye uelewa mkubwa hawapati nafasi za kuonesha uwezo wao. Badala yake watu wajanja wajanja na wasio na uwezi ndio wanapata hizo fursa. Sasa mwishowe kama taifa tunaonekana watu wa ovyo kwasababu wachache wasio na weledi wala uwezo ndio wamepata fursa.
 
Back
Top Bottom