Tanzania Heathcare personnel for success!!

Tanzania Heathcare personnel for success!!

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Wasalaamu kwa wanaJF wote!

Nimepata fursa ya kuhudhuria mkutano mkuu wa madaktari viongozi katika sekta afya jijini Dodoma ulioanza leo tarehe 20 mwezi agosti 2019.

Pamoja na ukweli kuwa madaktari sio watu wa kujikweza lakini ni vyema tukatambua kuwa ipo kazi iliyotukuka inayofanywa na Serikali katika sekta ya afya kupitia madaktari au niseme uongozi wa kiutawala eneo la madaktari viongozi.

Ndani ya miezi sita madaktari waliopata fursa ya kuwa viongozi wameweza kifanikisha mambo mazito na ya kuacha alama katika jamii!

madaktari hawa viongozi wameweza kufanikisha ukamilishwaji wa ujenzi wa wa hospitali za wilaya 67 hili sio jambo la kubezwa na credits zitawaendea wote haswa madaktari viongozi waliopo wizara ya Afya na Ofisi ya Rais Tamisemi dawati la Afya.This is signficant change and outcome! Mungu awape nini zaidi ya baraka?

Ninaiona future nzuri ya Tanzania yenye afya kupitia uongozi huu mzuri wa sekta ya afya unayojengwa na ofisi ya Rais Tamisemi na wizara ya afya.

Katika mafanikio haya makubwa katika sekta ya afya ambayo kwa namna fulani hayajatajwa sana ni muhimu kuwataja wanaume na wanawake wa kazi wanaoendelea kuyasimamia mabadiliko haya ya kihistoria katika sekta ya Afya.

Kwa fursa hii napenda kuwataja wachache ili jamii iwatambue katika mabadiliko chanya ya sekta ya afya !

1-Waziri wa Nchi Tawala za mikoa na Serikali za mitaa-Mh Jafo

2-Waziri wa Afya -Ummy Mwalimu

3-Makatibu wakuu wa wizara ya afya na Tamisemi haswa Dr Chaula

4-Naibu katibu mkuu Tamisemi anayedeal na afya..Dr Dorothy Gwajima

5-Mganga mkuu wa Serikali-Dr Bakari(mwalimu wangu)

6-Director of Health Services Dr Ntuli Kapologwe(very humble and understanding(

7-Waganga wakuu katika mikoa na Halmashauri zote.

8-Mkurugenzi wa MNH na JKCI

8-Watumishi wote wa Sekta ya Afya.

Hao niliowataja pamoja na Think Tanks wote katika tasnia ya afya.


..
 
Nakubali 100%
Na hongera sana kuwa mdau wa maswala ya Afya kwa muda mrefu....
La pili ni lengo la kila mwananchi kuwa na bima ya afya hasa wa vijijini...
Last time I checked only 6% had it...
Yes natambua effort za kuhakikisha kila mtoto mwenye umri Chini ya 18yo kupata bima ya afya kwa gharama nafuu.... lakini vip kuhusu umri wa kati na wazee? (Najua utasingizia wazee bure. .which isn't true)

Sasa issue inakuja, kujenga vituo vya afya pekeee haitoshi wakati wananchi wengi wa naomba msaada walipiwe bill hospitali au wanakimbia bill....!
Kwanini kusiwe na mpango wa kuhakikisha kaya maskini zinaweza kupata huduma pia kulingana na vipato vyao... (CHF is z mockery)
Shida moja kwa sisi waafrika tukishapata kidogo tunasahau kama wapo wanaoteseka kwa mamilioni. ..
JFYI : 80% of the humanity lives below $10/ day... kwahiyo umasikini sio excuse. ... lazima issue hizi zile addressed na policy makers ....
 
#/WagangaWakuuWaMikoaNaHalmashauri
 
JFYI : 80% of the humanity lives below $10/ day... kwahiyo umasikini sio excuse..

Salamu, is it below $10 or $1/day..? Dola 10 mbona kubwa mno, sitaki kuamini nipo kwenye hiyo 80%.... hebu niweke sawa hapo.
 
Hv mnaongelea nchi ipi jamani?labda ntaanza kubadili vituo vya afya niyaone hayo mafanikio..mxiewww
 
Hongera Dr Doroti Gwajima kwa kuwajibika ...msimamo wako kwenye kuijenga sekta ya afya isiyo tegemezi unatambulika
 
Asante JF kwa utunzaji wa kumbukumbu
 
Huyu mama mmemsifia,kichwa kimepata moto.
Ona sasa "field marshal" anavyohorojoa
 
Back
Top Bottom