Tanzania ifanye nini kuvuna faida za Huduma ya Afya kwa njia ya mtandao?

Tanzania ifanye nini kuvuna faida za Huduma ya Afya kwa njia ya mtandao?

wanzagitalewa

Senior Member
Joined
Jan 25, 2018
Posts
128
Reaction score
84
Katika miaka ya hivi karibuni, mapinduzi ya teknolojia za kidijitali yamekuwa mengi. Hii imezipa nchi nyingi faida bunifu za kupambana na changamoto mbalimbali.Mfano wa faida hizo ni huduma za afya kwa njia ya mtandao (m-health).

Kwa watoa huduma za afya wengi, m-health imeleta njia mpya za namna ya kutoa huduma ya afya kwa wahitaji. Kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya Deloitte, m-health ina tija kwa wote, wagonjwa na watoa huduma kwa wagonjwa. Mfano, mgonjwa anaweza kutumia mtandao kuperuzi dalili za ugonjwa na kushirikisha wengine ili kupata tiba stahiki.

Jinsi ambavyo ukuaji wa teknolojia na matumizi ya simu unaongezeka, idadi ya watu wanaotumia na kufaidika na m-health nayo itaendelea kuongezeka. Wataalamu wa sekta ya afya na teknolojia wanasema kwamba Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kufurahia matunda ya maendeleo haya ya kiteknolojia katika sekta ya afya.

Mfano, mgonjwa anayeweza kusoma vyema dalili za ugonjwa wake kwa njia ya mtandao anaondoa ulazima wa kwenda hospitali kwa baadhi ya matatizo. Katika eneo jingine, jumbe fupi za simu (SMS) zimesaidia kuwapa kina mama wanaonyonyesha taarifa sahihi kuhusu lishe kwa watoto wao.

Wakati tunafurahia teknolojia hizi na tija katika maisha yetu, ni vyema kukumbuka mchango mkubwa wa kampuni za mawasiliano ya simu ambazo zimetuwezesha kufikia maendeleo haya kwenye m-health. Mbali na kuweka miundombinu sahihi ya huduma hizi kukua, kampuni za simu pia zimeendelea kuwa bunifu kuwezesha wateja wake kupata huduma hizo.

Tigo Tanzania, mmoja ya kampuni kubwa za mawasiliano ya simu za mkononi nchini inawapa wateja wake, huduma hizi za m-health kama bima za afya na maisha. Huduma kama hizi zinaonesha namna gani kampuni hizi zinajiongeza na kwenda mbali zaidi kuhudumia wateja wake kwa ubunifu.

Tigo pia imewezesha usajili wa vizazi kipitia njia ya mtandao na hivyo kuwezesha upatikanaji wa haraka wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto. Hii ni hatua muhimu kwani cheti cha kuzaliwa ni nyaraka muhimu na ya awali kwa maisha ya binadamu yeyote ili kuweza kupata huduma zinazofuatia maishani kama afya, fedha, na kadhalika.

Tukiendelea kufurahia mchango huu wa kampuni za simu katika kuleta tija kwenye maisha yetu, tuendelee kuzijengea mazingira bora ya kufanya kazi hapa nchini Tanzania na kuziunga mkono ili ziendelee kufanya kazi bora zaidi.
 

Attachments

  • IMG-20201201-WA0002.jpg
    IMG-20201201-WA0002.jpg
    50.6 KB · Views: 20
Pale DIT kuna dish, lina telehealth moja babkubwa lakini aitumiki...imesheheni connection na madokta bigwa karibu wa India nzima wenye tahaluma mbalimbali za kitabibu,tungetumia mkonga wa taifa kulink madakitari wa Bugando na wakatibia wagonjwa Bukoba,shinyanga nk.wa Kcmc wakatibia watu waliopo Maji ya chai .specialist wa magonjwa ya kina mama alieopo Muhimbili akachunguza na kutoa tiba kwa mama alieopo mkuranga!

Pale Jakaya Kikwete heart institute wanatumia hii technologia kwa upasuaji wa moyo n.k. powered by TTCL.kulink na madokta bigwa wa matatizo ya moyo USA,India,China na Kwingineko,Pale wizara ya Afya kuna kitengo kabisa cha haya mavitu... changamoto ni nyingi kikubwa Siasa bado inaongoza kila kitu hapa Tanzania,ila utayari na baadhi ya mahitaji ya hii technology kutumika na kuleta tija katika huduma za afya Tanzania yapo tena ya hali ya juu tatizo ni siasa
 
in my dissertation a lot of things were suggested, 1. site ziwe Resourceful sio mnaweka mambo machache,yasiyoeleweka 2.Kuwe na presence of a proffessional anayeweza kutoa guidance in case of crisis au anayeweza ku direct wapi mtu aende au amuone nani,..yaani signposting to relevant 'proffessional'. User friendliness of the website etc etc.......it is hard to fight stigma;watu tumezoea kwenda hospitali tukiumwa,hii ni 'culture' yetu,hivyo wengi wanaotumia simu kutafuta matibabu wana DISATSSIFICATION. because of such beliefs..however internet penetration is getting higher,so it is anticipated sometime in the near future m-health will also be something normal...
 
Tiba Mtandao inatakiwa kuratibiwa kwa ukaribu na mamlaka zenye wataalamu wa tiba na afya ya binadamu wakishirikiana na wataalamu wa TEHAMA / Health Management Information System (HMIS) ili kuzuia 'uholela' wa kila mtu kwa vile anajua kutumia mtandao basi atoe ushauri au nasaha wakati wao siyo wataalamu wa tiba na afya ya binadamu.

Video hii inaonesha umuhimu wa tiba mtandao kushirikisha wataalamu wa tiba ya binadamu kama mradi huu :

Telemedicine project in Tanzania​


The video shows how the telemedicine project is working in Tanzania, run by ELCT (KKKT) and supported by IICD and Cordaid.

Language is Swahili with English subtitles
Source : IICD.org
 
Mtataka kodi hadi kwenye kinyesi, mnacheza na Kaka Beberu🐐🐐🐐🐐 bila kutumia akili, unamshika hadi mapwido, una wazimu wewe lazima akufyatue kiun
 
Health Management Information System (HMIS) in Tanzania
that reduces waiting time for patients and improves the overall efficiency of the clinic


IICD supports doctors and other health workers such as community workers in Africa and Latin America to use computers, mobile phones and other Information and Communication Technologies (ICT) to improve healthcare. This video tells the story of doctor Bon in Tanzania. This doctor works at a health clinic in Nyakato that is now using a Health Management Information System (HMIS) that reduces waiting time for patients and improves the overall efficiency of the clinic. The video also includes other examples and facts and figures about of IICD's effective work in 'ICT for health' in Africa
Source : IICD.org
 

The Business of Health - Telemedicine​


This week The Business of Health explores Telemedicine in South Africa and how it is changing the way healthcare will be delivered.
source : the Nielsen Network
 

Is Telemedicine The Future Of Health Care?​


The coronavirus pandemic has overwhelmed hospitals, physicians and the medical community. That's pushed telemedicine into the hands of providers and patients as the first response for primary care. Telemedicine isn't new to the medical community, however it hasn't been embraced due to insurance coverage, mindset and stigma. Here's how it works and what it means for the future of health care.
Source : CNBC
 
Mawazo Kama haya sio muhimu awamu hii labda uwashauri jinsi ya kuuwa upinzani utapata credit
 
Back
Top Bottom