SoC04 Tanzania Ijayo ni Tanzania ambayo inaamini Binadamu wote ni sawa

SoC04 Tanzania Ijayo ni Tanzania ambayo inaamini Binadamu wote ni sawa

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 4, 2024
Posts
6
Reaction score
1
Tanzania Tuitakayo Miaka 25 Ijayo Ni Tanzania Ambayo Inaamini Binadamu Wote Ni Sawa Hakuna Aliye Bora Kuliko Mwenzie Kwasababu Ya Cheo, Jina, Mali Na Mengineyo.

Maana Kumekuwa Na Utaratibu Wa Mazoea Katika Hili Taifa Nikimaanisha Matabaka Ya Watu Fulani Ambao Wao Keki Ya Taifa Ni Kwaajili Ya Birthday Zao Tu Na Si Watu Wengine Hivyo Kuna Hali Yakulambana Viatu Na Miungu Watu Inatakiwa Mwananchi Wa Kawaida Ashiriki Moja Kwa Moja Kufanya Maamuzi Isiwe Tu Kwenye Hizi Chaguzi Zilizo Jaa Lawama Na Ulaghai Kwahiyo Haki Ya Watu Kuishi Izingatiwe Watu Wengi Wanapoteza Haki Zao Za Msingi Kwa Kuhofia Kupoteza Haki Yao Ya Kuishi Kwasababu Mazingira Yaliyopo Yanaminya Uhuru Wa Kujieleza Na Kukosoa Maovu Yanayoendelea Kwenye Serikali Kama Serikali Ni Watu Na Si Ni Mtu Basi Watu Hao Wasikilizwe Maoni Yao Na Yafanyiwe Kazi.

Ifike Wakati Nchi Isiwe Ya Kundi Fulani Maana Maamuzi Ya Kundi Fulani Yana Athiri Maisha Ya Watu Wengi Ambao Hawasikilizwi Na Wala Hawahusishwi Kwenye Maamuzi Ya Taifa Lao Isipokuwa Wakati Wa Uchaguzi , Hivyo Serikali Yapaswa Kuunda Programu Maalum Ambazo Zitatumika Kusikiliza Kero Na Maoni Ya Wananchi Maana Nao Wana Fikira Zao Ambazo Zinaweza Saidia Maendeleo Ya Taifa Hili , Tizama Wananchi Wengi Wana Mawazo Mazuri Tu Ila Kuyafikisha Wanashindwa kutokana Na Hofu Ya Kupoteza Haki Ya Kuishi Ama Kushikwa Na Kufungwa Vifungo Ambavyo Si Rafiki Hivyo Uwekwe Mfumo Wa Wazi Na Rafiki Wenye Kuzingatia Hali Zote Za Binadamu Wanaojua Kusoma Na Wasiojua Kusoma, Wanaojua Kuandika na Wasiojua Kuandika, Wanaojua Kutumia Teknolojia(Simu, Kompyuta) Na Wasiojua Kutumia Teknolojia Maana Kila Aliye Timamu Ana Wazo Na Maendeleo Huanzia Kwenye Wazo.

Na Maendeleo Yeyote Yanategemea Uzalendo Wa Kweli Hivyo Watu Wapewe Uhuru Wa Kukosoa Mienendo Ya Viongozi Wao Ili Kulinda Na Kuendeleza Tunu Za Nchi Hii Haya Mambo Ya Kusema Unanijua Mimi Ni Nani Yanatafuna Sana Roho Ya Taifa Hili Silaha Zilizopo Zitumike Kuilinda Nchi Na Maadui Siyo Kuwatishia Raia Wake Wasafi Na Watiifu

Ko Tujenge Nchi Kwa Uzalendo Na Si Kujenga Hoja.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom