mossad007
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 1,165
- 852
Mbona kuna nchi zinafahamaika kwa majeshi zinaongoza duniani. Iweje intelligence agency tu ndo zisirankiwe? Wanazuoni niwaulize kwani ni lazima kila kitu kirankiwe kwa kuangalia quantitative data tu? Ina maana hatuwezi kujua kitu fulani ni cha ngapi kwa kuangalia qualitative data. Kama hatukuwahi kushambuliwa, na kama siri za usalama hazikuwahi kugunduliwa, na kama mbinu za majasusi ziligunduliwa mapema kabla madhara hayajatokea kwa nini tusijilinganishe na mataifa mengine na kujipa nafasi stahili? Mimi naweza kukubali kuwa huenda miaka hiyo intelligencia yetu ilikuwa ya tatu.
Nikuulize swali ndugu Mabaghee kutokana na maswali hayo hayo uliyouliza anayegundua siri za usalama wako anakuambia kua tumegundua siri za usalama wenu? unaposema siri za majasusi kugunduliwa mapema kabla madhara hayajatokea mna uhakika gan kua jasusi hajatoa siri yoyote kuhusu usalama wenu ( refer to Cohen ) na hayupo au hawatakuwepo wengine? anayesema TISS ilikua ya tatu atupe details za nini kiliwafikisha hapo na miaka gan sio maneno matupu na atupe top three tujue nani wa kwanza na nani wa tatu.. Jeshi ni tofauti na idara za ujasusi JWTZ ikinunua ndege za kivita Urusi, haitatangaza itafanya siri yake lakini mrusi atajua kila kitu kwasababu ndo kakuuzia, majasusi tunawazalisha wenyewe na kuwatuma wenywe kisiri hatuuziwi na mtu! Nakubali idara yetu ilipata heshima lakini hili la kua wa tatu nani kasema? hiyo CIA, FSB,Mossad na M16 ndizo taasisi zinazosifika lakini kila mtu ataichagua yake kwa vigezo vyake na huwez toa ranking yako kidunia ikatambulika na kua recorded kama zilivyodata za uchumi wa dunia kwamba tunajua anaanza Mmarekan anafuata China then Japan hili dunia nzima wanajua na wamelirecord. Kwenye intellijensia ni tofauti tutabaki kuhisi tu na ikishakua kila mmoja ana yake as the best bas hizo takwimu sio FORMAL bali ni INFORMAL!