Tanzania iliwaza vyema, umeme mkubwa uliopita sokoni umeua watu 26 Kongo

Tanzania iliwaza vyema, umeme mkubwa uliopita sokoni umeua watu 26 Kongo

Zipo njia kubwa na ndogo
Bagamoyo road pande zote mbili kuna njia kubwa za umeme.... HIGH VOLTAGE NI ILE SASA..... Achana na ule unaoenda Zanzibar hapana.... angalia umeme uliopo pembezoni mwa barabara zile nyaya 6 za juu kabisa... SASA NJOO TEGETA NA BUNJU UNIAMBIE KAMA UKIKATIKA WAYA WATSKUFA WATU WANGAPI?Anzia tu tegeta nenda boko malizia na pale bunju B..... HAPO SASA NJOO USEME NINI KITATOKEA.
 
unama
Nenda Mbagala Zakhiem na kituo kipya cha daladala kipo ukiachilia mbali soko. Kwahiyo wewe kazi yako kusifu usilolijua!
Unamaanisha kituo cha daladala kipo chini ya Grid ya TAIFA (high Voltage?)? kama sio unafiki weka ushahidi hapa wa picha
Kwa wale waliosomea Physikia wanaelewa kuwa madhara ya grid (umeme mkubwa) sio lazima waya ukatike. Hata kutumia muda mwingi chini ya zile nyaya sio salama...japo ni somo refu
 
Masoko ya Tanzania wapate somo kwa tukio hilo , hasa karume, boma, Mabibo , temeke nk
 
Nchini Tanzania hairuhusiwi kujenga au kufanya shughuli chini ya miundombinu ya umeme inayobeba umeme mkubwa(High voltage). Wachache wanaelewa lengo, wengine wakijaribu kuishi chini ya njia hizo na mara kadhaa tumeshuhudia bomoa bomoa. Pia TANESCO wakijenga njia mpya wako radhi kulipa fidia wahusika waondoke.

Nchini Kongo, hali imekuwa tofauti kwenye soko lililopo mjini Kishasa ambapo waya unaobeba umeme mkubwa umedondoka na kugusua baadhi ya nyumba na soko hilo, watu 26 wakifariki.

Chama cha wahandisi nchini Kongo kwenye taarifa yake, wamesema ajali hiyo ambayo iliweza kuepukika ni matokeo ya kutoheshimu mipango miji chini ya njia kubwa za umeme.

Shirika la umeme nchini Kongo limesema ajali hiyo ilitokea radi ilipopiga wakati wa mvua na upepo mkali Jumatano asubuhi na kutoa pole kwa familia zilizoathirika.

Video iliyosambaa inawaonyesha marehemu miili yao ikiwa imelala sehemu ikiwa kwenye maji yatokanayo na mvua. Waziri mkuu amesema soko hilo lilishapangwa kuhamishwa kwenye baraza la mawaziri kilichofanyika Jan 7, sababu ya wakati huo ikiwa ni soko kutengeneza foleni barabara inayounganisha Kinshasa na mji wa Matadi.
Mtoa mada huenda hujafanya uchuguzi kabla,ukisema shughuli za binadamu unajua mipaka yake?? Anyway nguzo za umeme(high volteg) kuna mda zinakross barabara kuu chukuli basi la abilia 50 likiguswa na waya kama sokoni huko kongo ilivotokea kudondokewa waya itakuwaje?? Hatuombi itokee ingawa ndo ivo
 
Back
Top Bottom