Tanzania iliyo bora: Tunahitaji sheria bora, inayosimamia na kuwajibisha

Tanzania iliyo bora: Tunahitaji sheria bora, inayosimamia na kuwajibisha

Tanzania one love

New Member
Joined
Mar 10, 2018
Posts
4
Reaction score
0
Ili kujenga taifa tulitakalo na kufikia ndoto za wengi, ni lazima tukabiliane na matatizo yaliyomo ndani ya nchi yetu kwa kuboresha na kusimamia sheria.

1. Uwajibikaji wa viongozi katika kusimamia rasilimali za umma pamoja na uongozi.

2. Kuundwe sheria, au kuwe na utekelezaji wa sheria, zinazowawajibisha viongozi bila kuwalinda kulingana na aina ya vyeo

3. Kuundwe mfumo bora wa wazi na wa haki wa upigaji kura, hii itasaidia wananchi kujitokeza kupiga kura bila hisia tatanishi au wasiwasi wa matokeo

4. Kuwepo na utekelezaji au iundwe sheria nyingine kali itakayoweza kuwawajibisha viongozi wala rushwa pamoja na kuzuia rushwa

5. Iundwe sheria itakayomruhusu raia yoyote kutoa maoni bila hofu na kumlinda

6. Iundwe sheria itakayozuia viongozi kuingia mikataba ya kigeni inayouza rasilimali zetu.

7. Mwisho ianzishwe kampeni na itolewe kampeni ya kuwaelimisha wananchi juu ya haki zao kisheria, zinazowalinda na zinazowawajibisha, hii itasaidia wananchi kuipenda serikali yao na kuwajibika kwa kiwango cha juu katika kila nyanja
 
Back
Top Bottom