Tanzania imefaulu kwenda AFCON ki aina aina tu. Kutokuwa na uhakika wa kufaulu mpaka baada ya mechi Cape Verde

Tanzania imefaulu kwenda AFCON ki aina aina tu. Kutokuwa na uhakika wa kufaulu mpaka baada ya mechi Cape Verde

Jbush Garigo

Member
Joined
Feb 24, 2019
Posts
33
Reaction score
22
Ni kweli Tanzania tumefanya vizuri kwenye mechi kati yetu na Uganda. Lakini mimi najiliza 'kwanini tusubiri bahari nasibu?' kwanini tuwe watu wa kucheza Kamari kila siku? Kwanini tuwe watu wa kuiombea tu Lesotho ishindwe au Cape Verde ishinde?
Inamaana tulianza vibaya. Kwanini tusiingie kwenye mechi ya mwisho na muhimu kama hii leo tukiwa na hakika kama Uganda? Tuna kasoro gani? Kwa mantiki hii mawazo yangu nadhani hatutafika mbali japo nina hamu sana tufuke japo hata nusu fainali ya AFCON. Ni muda muhafaka sasa wa Taifa Staa kutuhakikishia kwamba ni kweli hatuingia AFCON kwa cheti feki wala kwa bahati mbaya.
Fundisho tunalopata hapa ni kwamba the ealier is the better kama tungeanza vizuri wala tusingekuwa na pressure kubwa kiasi hiki mpaka kufikia hatua ya kugusa uchumi wa nchi kwa kunywa kwa nusu bei, huu ni mtazamo wangu tu lakini.
Kila mtu ni lazima afanye maandalizi ya mapema na sio kusubiri bahati ya mtende kuzaa mnazi kama yaliyotukuta Leo. Mchezo wa mpira ni lazima tuufanye kuwa ni sehemu ya maisha ya watanzania hapo tutafanikiwa zaidi. Mungu sio Athumani. Mungu atuongoze twende mbele zaidi.
 
Back
Top Bottom