Tanzania imekuwa nchi ya kitoto toto! Hatuku makini kama zamani

Tanzania imekuwa nchi ya kitoto toto! Hatuku makini kama zamani

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Tanzania ya sasa sio ile ya zamani. Pamoja na ukuaji wa habari na teknologia kuna ongezeko kubwa la watoto na vijana wengi. Umri wa kati Tanzania ni miaka 19.

Tusishangae kuona wasanii wamejaa kwenye mikutano ni kwasababu yangu vijana wadogo. Kijana wa miaka 21 hawezi kujali katiba au kuelewa ni nini watu wazima ndiyo kazi yao. Hivyo msishangae kuona machawa ni wengi kuliko wahariri na wahandishi wa habari wenye maono. Kwa ujumla nchi yetu sio ile tena ya wanasiasa makini hasa ndani ya CCM maana ni rahisi kudanganya hawa madogo maana hawajaamka na kuelewa mambo vizuri bado.

Bahati mbaya wazalendo wa kweli wanaopenda nchi zaidi ya mslahi binafsi ni wachache sana. Hivyo wako tayari na danganya toto kwa manufaa ya chama na wao na sio Taifa. Vijana hawa wanajui umuhimu wa katiba, deni la taifa, uwekezaji na mikataba. Wanasiasa nao kwasababu wanaelewa hili na sio wazalendo tutawaona wasanii, machawa na Polisi kila mahali na sio mambo ya maendeleo. Wengi hapa vijana wanasifia na kubishana bila hata kujua wanabishana kwa lipi hasa. Yaani hata kama mambo ni kwa manufaa yao wanapinga!

Tunawakati mgumu sana kwa kizazi hiki maana wanasiasa wamegundua ujinga wa vijana unawasaidia wao
 
Back
Top Bottom