Tanzania imepata ukuaji mdogo wa GDP ukilinganisha na Rwanda na Uganda kuanzia mwaka 2021

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Katika ripoti ya NBS inayoonesha masuala mbalimbali ya GDP kwa kipindi cha kuanzia April hadi Juni 2023, imeonesha ukuaji wa GDP wa Tanzania umeshuka ukilinganisha na Rwanda na Uganda.

Tanzania imefananishwa na Rwanda na Uganda kwa kuwa ndio nchi pekee katika Jumuiya ya Africa Mashariki waliotoa takwimu kuhusu ukuaji wa uchumi wao. Takwimu zinaonesha mwaka 2020, GDP ya Tanzania ilikuwa kubwa kuliko nchi hizo.

CountryEconomic Growth Q2 2023Economic Growth Q2 2022
Rwanda6.3%7.5%
Uganda6.8%5.6%
Tanzania5.2%4.7%



Taarifa hii inaonesha hata ukuaji wa uchumi uliporomoka kwa kiasi kikubwa tangu dunia kukumbwa na COVID-19 mwaka 2019 ambapo athari zake zilianza kuonekana 2020



Hata hivyo, hii sio excuse kwa kuwa kama uchumi uliweza kukua vizuri na kuwa juu ya wenzetu tunapaswa kujiuliza wapi pana shida hadi uchumi kuporomoka kwa kulinganisha na wengine.
 
Sasa Kuna shida gani broo ikiwa Rwanda na Uganda Wana Ukuaji mkubwa kushinda Tanzania?

Ingekuwa ni case kama uchumi Wetu ungekuwa unapungua badala yake unakua so hakuna tatizo.

Mwisho mwaka 2023 is olmost done tunaenda 2024 na Ukuaji utakuwa kama ifuatavyo 👇

View: https://twitter.com/IMFAfrica/status/1711801484457746840?t=hZkcrIliilM4itXO1ZeSVQ&s=19
 
Rwanda na Uganda zilitupita, lakini nina uhakika na sisi tuliipita Burundi na South Sudan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…