Tanzania imetoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi wa Burundi zaidi ya laki moja

Tanzania imetoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi wa Burundi zaidi ya laki moja

Kamyamya

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2012
Posts
560
Reaction score
572
Juzi jioni akiwa Tabora katika matukio muhimu kitaifa,rais alitoa tamko la kihistoria la kuwapa uraia wakimbizi 162000.

RAIS KIKWETE AWAPA URAIA WAKIMBIZI WA BURUNDI 162,156 MJINI TABORA LEO
unnamed%2B(16).jpg

Rais Jakaya Kikwete akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Loveness Ruhaga (kulia) aliyekuwa Mkimbizi kutoka nchini Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Tabora leo.

Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 na kuwatangazia kuwa sasa wamekuwa raia halali wa Tanzania hivyo wahakikishe wanafuata sheria zote za nchi na waepuke kufanya vurugu za aina yoyote kwani wakikiuka masharti hayo waweza kunyanganywa uraia huo.

Wakimbizi hao walioingia nchini tangu mwaka 1972 walionyesha furaha kwa kuimba na kucheza vyimbo mbalimbali. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.

unnamed%2B(17).jpg

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akimuonesha Rais Jakaya Kikwete (kulia) mchoro unaoonesha jinsi wakimbizi wa Burundi walivyoingia nchini wakati walipokuwa wanatoka nchini kwao mwaka 1972.

Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 waliokuwa raia wa Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Tabora leo. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.


unnamed%2B(18).jpg

Rais Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania, waliokuwa wakimbizi 162,156 kutoka nchini Burundi walioingia nchini tangu mwaka 1972. Tukio la utoaji wa vyeti hivyo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora mjini humo leo.

Raia Kikwete katika hotuba yake aliwataka raia hao wapya kuwa waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.

unnamed%2B(20).jpg

Msoma risala ambaye ni mwakilishi wa raia wapya 162,156 nchini ambao walikuwa wakimbizi kutoka nchini Burundi, Dafroza Baragwimba akiisoma risala yao mbele ya Rais Jakaya Kikwete (watatu kulia) wakati ya hafla ya utoaji wa vyeti kwa raia hao.

Rais Kikwete alitoa uraia kwa wakimbizi hao na kuwataka wawe waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.

unnamed%2B(21).jpg

Rais Jakaya Kikwete (wasita kushoto waliokaa), mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya raia wapya 162,156 wa Tanzania (nyuma waliosimama) baada ya kupewa vyeti vya uraia na Rais Kikwete katika hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini humo.

Picha zote na Felix Mwagara, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Chanzo: Michuzi
 
Tar.14,10,2014 Mh.rais ametoa tamko la kihistoria la kuwapa uraia wakimbizi 162000.waliotoka burundi tangu 1972.....!!??
 
Tar.14,10,2014 Mh.rais ametoa tamko la kihistoria la kuwapa uraia wakimbizi 162000.waliotoka burundi tangu 1972.....!!??

Kuna pros and con's,faida na hasara,tunaweza kuwatumia kama agents wetu katika nchi walizotoka kwa maana ya kupandikiza utawala tunaoutaka katika nchi zao,au wao wakawa mapandikizi kwetu kwa kufanya intelligence
 
Jamvini, huu uraia unaotolewa kwa kundi kuuuuubwa la watu una dhamira gani kama si kuandaa wapiga kura kwa ajili kupitisha katiba ya 666 pamoja na uchaguzi ujao? Ni mbinu ya "chama" maana kinajua kimeshapoteza imani yetu. Kinajua katiba yao tutaikataa. Na pia hofu ya uchaguzi 2015.
 
Nchi ya kwanza duniani kutoa uraia kwa watu wengi kwa mara moja. Tz noma sana yani watu 162,000 toka Burundi wamepewa tuu uraia, hivi wamelipia bei gani kwanza?

Nchini Tanzania hatimaye Serikali ya Tanzania hapo ilitoa vyeti vya uraia kwa waliokuwa wakimbizi wa zamani wa Burundi zaidi ya laki moja na elfu sitini na mbili ambao wamekuwa wakiishi kwa zaidi ya miaka arobaini kama wakimbizi,hatua inayoelezwa kuwa haijawahi kufanywa na nchi yoyote Duniani.

Sanjari na hatua hiyo Serikali ya Tanzania imesema hakutakuwa na mpango wa kuwahamisha kutoka katika makazi yao ambayo wamekuwa wakiishi kwa kipindi chote hicho na kwamba kwa sasa watakuwa huru kwenda kuishi popote kama raia wengine wa Tanzania ili mradi hawavunji sheria.

BBC
 
Jamvini, huu uraia unaotolewa kwa kundi kuuuuubwa la watu una dhamira gani kama si kuandaa wapiga kura kwa ajili kupitisha katiba ya 666 pamoja na uchaguzi ujao? Ni mbinu ya "chama" maana kinajua kimeshapoteza imani yetu. Kinajua katiba yao tutaikataa. Na pia hofu ya uchaguzi 2015.

Lazima wafanyiwe management nzuri,hawa wanyarwanda na warundi huwa hawasahau kwao na ni mabingwa was hujuma. Angalia kagame,kaishi Tanzania,kawa mkuu mkuu wa intelligence wa la Uganda lakini hatimaye karudi kwao!!!!!,baadhi waliishi Kongo tangu miaka ya hamsini,hawakuridhika,wakataka kuunda taifa jingine ndani ya Kongo,cha kufanya ni kuhakikisha hawakai eneo moja kama sasa, wasambazwe sehemu mbalimbali,hats kama kuna taifa linataka kuwatumia kwa hujuma mbalimbali zikiwamo za kijeshi lishindwe,wasikae mpakani karibu na nchi zao za asili kwa wingi mkubwa,na tatu TISS iwatumie baadhi kama maajenti na iwapeleke huko walikotoka,
 
Wale "Wasomali" wa kule Handeni walikuwa wangapi? Kama hii ni mara yenu ya kwanza kuona/kusikia kundi kubwa la wakimbizi wakipewa uraia basi bado Watanzania tuna safari ndefu ya kujifunza kufuatilia yanayotokea nchini.
 
....Nashangaa hawa watu wapwani wasiojua tabia ya hawa jamaa,hakika mmeliwa,warundi, wanyarwanda sio watu wa mchezo,mjiandae na uhalifu wa bunduki........inakuwaje unasema unawapa uraia watu ambao unasema walikuwa wanakaa hapa tanzania kwa miaka 42!....Nashangaa sana nchi hii ardhi hatuna,rasimalin ni ndongo lakini mnawazoa tu wapakistan,waarabu,wapalestine,kongo,kenya,rwanda,burundi......shauri lenu........maana ni ujinga tu,au kujipendekeza kwa wafadhili au mmeoa huko sasa mnahalalisha ili isionekane mmeoa TX,huko ofisi kuu kuna kasuku!
 
binadamu wote ni sawa na Afrika ni moja. Mwafrika ana haki ya kuishi popote pale atakapoona panamfaa ndani ya Afrika, wabaguzi pekee ndo wanalilia na kutukuza vimipaka hivi vilivyowekwa na wakoloni
 
Bora wapewe Tu watu tokea mwaka 72 enzi za mwalimu wapo nchini wameshakuwa wanyamwezi hao.
 
....Nashangaa hawa watu wapwani wasiojua tabia ya hawa jamaa,hakika mmeliwa,warundi, wanyarwanda sio watu wa mchezo,mjiandae na uhalifu wa bunduki........inakuwaje unasema unawapa uraia watu ambao unasema walikuwa wanakaa hapa tanzania kwa miaka 42!....Nashangaa sana nchi hii ardhi hatuna,rasimalin ni ndongo lakini mnawazoa tu wapakistan,waarabu,wapalestine,kongo,kenya,rwanda,burundi......shauri lenu........maana ni ujinga tu,au kujipendekeza kwa wafadhili au mmeoa huko sasa mnahalalisha ili isionekane mmeoa TX,huko ofisi kuu kuna kasuku!

Du nchi ya Tanzania ardhi hakuna, wewe utakuwa mgeni wa Tanzania.
 
This is a good gesture, Kenya should also do the same for the Makonde community from Mozambique who have been hereb for 60 years now. Somehow though the Mozambique government still want them back and may be this is what is causing the delay.
 
ktk dunia hii ya ubapari hakuna zaidi ya haki ya uraia.....maana yake ni kuwa Rais ameingiza vibaka kibao katka umaskini huu.....sijuin itakuwaje huko lakini hawa watu sasa wanaingia ktk jamii hii kufanya vurugu....kwani hamkumbuki mauji ya mbwa polisi na polisi binadamu kule mbezi si tuliambiwa ni warundi?........hatutaki wageni njaa hao
 
This is a good gesture, Kenya should also do the same for the Makonde community from Mozambique who have been hereb for 60 years now. Somehow though the Mozambique government still want them back and may be this is what is causing the delay.

And some somali and eritrea people residing at kenya for a long time
 
Wakimbizi hawa walikuwa Kambi gani?maana mtoa habari amerudia tu kuwa Rais ametoa vyeti vya uraia bila kutaja kambi ipi. Kuna Kambi hapo Tabora na hata Katavi. Kama ambavyo wengi wametia shaka ni kweli kwamba Warundi ni waovu. Nenda Kigoma kutokea Tabora, wamezagaa na ndiyo wanaofanya ujambazi kote huko. Huo ni
 
Kwa jicho langu la tatu naona muheshiwa ameongeza idadi ya majambazi wanaotumia silaha nchini kwetu, hawa hawa ndio watekaji wa mabasi ya abiria.
 
Mshirika wa muungano Zanzibar sidhani kama wanashuriwa juu ya suala muhimu kama hili.
 
Back
Top Bottom