Halafu nilisikia eti wanasifia kuwa tz ndio nchi ya kwanza kutoa uraia kwa idadi kubwa kwa wakimbizi. Yaani ndio yaleyale yakupenda sifa kuwa tunasifika kwa UPOLE, UKARIMU.
1. Hawa ambao Kikwete aliwapa uraia ni Kabila la Watusi pekee yao au ni Wahutu pekee au?
2. Kwa nini Kikwete aliwapa uraia hawa watu mbadala ya kuwarudisha kwako?
3. Je yanayotokea DRC Congo ya kundi dogo la Watusi badala ya kutanguliza utaifa wao wanatanguliza Utusi (ukabila)
Wanataka madaraka makubwa kuliko wenye Congo yao, je huko mbeleni hawatakuja kulalamika kuwa na wao kwa kuwa ni kundi dogo wanabaguliwa kwenye uongozi Tz?
4. Bahima wanajiona kuwa nchi za maziwa makuu ni mali yao wana ndoto ya kutawala kote, kwa nini Kikwete kuwaamini hawa watu?