Tanzania imewahi kuwa na Rais shabiki wa Simba?

Tanzania imewahi kuwa na Rais shabiki wa Simba?

Dar es Salaam Young Africans ni club iliyoanzishwa kwa lengo la kukutana kujadili na kuweka mikakati ya kupata Uhuru wa Tanganyika.

Kwa hiyo Young Africans walitumia club hii ya mpira kama kichaka cha kuukwepa mkono wa mkoloni aliyekataza makusanyiko ya kisiasa na kuruhusu ya michezo.

Hao waanzilishi wa Yanga ndiyo waanzilishi wa TANU, ASP, na hatimaye CCM.

Kwa hiyo usishangae kwanini viongozi wengi ni Yanga. Sababu ni hiyo kwamba Yanga imeanzishwa na wana-CCM na wazalendo wapigania uhuru na ndiyo maana wanajiita WANANCHI.

Kwa upande wa Simba, ilianzishwa na wapinzani wa uhuru ambao waliungwa mkono na mkoloni yaani baada ya kuona wazalendo wanapanga mipango yao kupitia michezo basi na wao wakaanzisha Sandaland ambayo ndiyo Simba.

Ushahidi mwingine angalia rangi za bendera za Yanga na CCM zinafanana.
 
Tanzania imewahi kuwa na Rais shabiki wa Simba?

Nyerere - Yanga

Mwinyi - Yanga (hata kwenye mazishi wajukuu zake waliweka wazi)

Mkapa - ????

Kikwete - Yanga

Magufuli - Yanga (kuna siku alifurahi sana kuona Simba kafungwa, aliwapiga Simba kijembe "Kagera sugar wametoboa tundu la Simba" huku anacheka kiyanga anga

Samia - Yanga huyu, aliwaalika ikulu kwa kufika fainali kombe shirikisho, aliwapa ndege bure kwenda na kurudi, kununulia mashabiki tiket, nk. sherehe za uhuru wa Malawi alipendekeza Yanga waende nae huko japo kikosi kilijaa yanga toto
mkapa yanga,samia ni simba
 
KWA HIYO UBINGWA WA YANGA HAPA NCHINI NI WA KIMKAKATI PIA ILI UWE RAIS LAZIMA UWE SHABIKI WA YANGA KAMA VIPI HUU UZI UTOLEWA KWANI UNAGAWA WATU
 
Sawa ilikuaje mkawapokea jwaneng galaxy na kuwapa hifadhi pale kigamboni.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Timu ambayo hawajui klabu yao imeuzwa au imekopeshwa hawezi kutoa watu makini.

Wanashangaa tuu mtu anasema ametumia 51bn kununua club na hakuna taarifa kwa wanachama wa club.
Bwana mdogo Uto iliwahi kukodiwa na Manji enzi za rais Kikwete.
 
JF IMEVAMIWA NA MAZUZU.

AKIWA YANGA AU SIMBA INASAIDIA NINI????

INA FAIDA GANI??????

AU KUWA KWAO YANGA KUMESABABISHA WACHUKUE UBINGWA WA AFRICA?????.??.
 
Unafikiri na wenyewe hawana akili timamu mpaka wafikie hatua ya kushabikia timu ambayo kiongozi wake alidiriki kuwaambia hadharani mashabaki na wanachama wa timu kwamba ni mbumbumbu!

Yaani mbumbumbu maana yake ni empty head, kilaza, pomole, bongotole, kichwa maji, kichwa mninga, kichwa panzi, popoma, nk.
 
Tanzania imewahi kuwa na Rais shabiki wa Simba?

Nyerere - Yanga

Mwinyi - Yanga (hata kwenye mazishi wajukuu zake waliweka wazi)

Mkapa - ????

Kikwete - Yanga

Magufuli - Yanga (kuna siku alifurahi sana kuona Simba kafungwa, aliwapiga Simba kijembe "Kagera sugar wametoboa tundu la Simba" huku anacheka kiyanga anga

Samia - Yanga huyu, aliwaalika ikulu kwa kufika fainali kombe shirikisho, aliwapa ndege bure kwenda na kurudi, kununulia mashabiki tiket, nk. sherehe za uhuru wa Malawi alipendekeza Yanga waende nae huko japo kikosi kilijaa yanga toto
Siyo Mashabiki wa Yanga, ni walezi wa timu zote ila timu yoyote ikifanya vizuri anajumuika nayo. Samia alikwenda kufunga Wiki ya Simba
 
Muda uliotumia kuandika huu utumbo,si ungekuna nazi tu mzee.
 
Back
Top Bottom