Tanzania imezizima, dunia imetaharuki kwa kuwa Magufuli alifanya yale wanadamu waliyotarajia kama kiongozi. Je, yupo atakayeweza kuvaa viatu vyake?

Miaka mitatu iliyopita nilikutana na mzee mmoja, tukaketi chini akanipa soga.../

Alisema wangapi walikuwepo namba moja, leo wamebaki chini ni vioja... watu wamewasahau
Sio wote tutakao sahauliwa mkuu.Wengine tutakumbukwa kwa yale mazuri au hata mabaya tuliyowafanyia binadamu wenzetu.Wewe utakumbukwa kwa lipi?
 
Ukijikita kwenye propaganda unageuka kuwa mjinga kwa watu wenye uelewa. Wakati wa Nyerere tuliambiwa hatuwezi kupata rais kama Nyerere, leo hii mnatuambia hatuwezi kupata rais kama Magufuli! Hivi mbona mnatuchanganya, au nyie ndio mmechanganyikiwa?
Sijasema hatuwezi kupata mwingine mkuu yupo.Swali ni kwamba je tutampata?Huyu tulishampata.
 
Tofauti ya Jiwe na Marais waliomtangulia Ni:-
Kupeleka maendeleo kwa upendeleo nyumbani kwao,hata Kama hakukuwa na umuhimu wowote kwa Taifa
butiama x
Uzaramoni x
Lupaso x
Msoga x
CHATO ✓

Kodi za taifa zilitumika kujenga miundombinu toka Zama za
Mwalimu,
Mwinyi,
Mkapa,
kikwete,
Magufuli,
lakini yeye ndio anapewa sifa zaidi ya waliomtangulia.

Wafanyakazi hawajaongezwa mishahara tangu bwana huyu aingie madarakani,hi haijwahi fanywa na Maraisi waliomtangulia,nadhani inaweza kuwa rekodi ya dunia.

Wakulima,wamekiona Cha moto.
wakulima wa korosho wanaweza kuwa mashahidi.

wafanyabiashara wamefilisika,wamehamisha biashara zao,wamefunga na wengine kufa.

Wanafunzi wa elimu ya juu wamekiona Cha moto kuhusu Loan Board,waliomaliza vyuo wamekatwa mikopo zaidi ya makubaliano,
walioomba mikopo wamebaguliwa tofauti na awali,

Waliobomolewa nyumba bila malipo,

Wapinzani waliteswa,kufukuzwa bungenj,kutekwa kupigwa risasi na kukimbilia uhamishoni,

Mambo ni mengi mda ni mchache.
Sina haja ya kukujibu,Watanzania kwa uwingi wao na vitendo vyao wamekujibu.

Yote ulivyo orodheshwa hayana uhalisia wowote, yamechangiwa na chuki na husuda.
 
Sijasema hatuwezi kupata mwingine mkuu yupo.Swali ni kwamba je tutampata?Huyu tulishampata.

Yeye mwenyewe alijigeuza kuwa adui wa kupatikana kiongozi sahihi, kwahiyo hata akipatikana asiye sahihi, yeye ni sehemu ya hilo tatizo.
 
Sina haja ya kukujibu,Watanzania kwa uwingi wao na vitendo vyao wamekujibu.

Yote ulivyo orodheshwa hayana uhalisia wowote, yamechangiwa na chuki na husuda.

Hakuna kitu kibaya kama kukwepa ukweli, na hili sio tatizo lako tu, bali wote wanaomsifia Magufuli hawataki kusikia ukweli halisi kuhusu mapungufu na madhara ya utawala wake, bali wanataka tuimbiwe sifa tu ambazo hazina uwiano na ukweli uliopo.
 
Uzuri wa sisi wananchi hua tunachambua chenga na mchele.
Tunaangalia tu,JPM was a really hero.Mimi sijawahi Ina niseme tu kweli.
Na wengi tumemuunga mkono JPM na si chama baada ya kutushawishi.

Mama Samia suluhu tutampa moyo wetu baada ya kuona akifanya mazuri,hatutoi uaminifu wetu kwa mtu kizembe.

JPM ALITUCHOTA,SI WAKUBWA SI WADOGO,DINI ZOTE,KASKAZKNI KUSINI MASHARIKI MPAKA MAGHARIBI,NJE YA MIPAKA YA TZ,AFRICA NA WAPENDA HAKI NA MAENDELEO DUNIA NZIMA.

HAKIKA JPM WEWE NI GOOD LEADERSHIP NILOISOMA NA KUIIMBA KWENYE MADARASA YANGU YOTE,NA NILIHISI TU NI KWA AJILI YA KUJIBIA MITIHANI KUMBE NI KWELI HUTOKEA GOOD LEADERSHIP NA NCHI IKAJENGEKA.

bado nae delea kuamini TZ Ni TAJIRI NA TUMEONESHWA HASWA
 
Sina haja ya kukujibu,Watanzania kwa uwingi wao na vitendo vyao wamekujibu.

Yote ulivyo orodheshwa hayana uhalisia wowote, yamechangiwa na chuki na husuda.
Ukweli unatabia ya kujitenga na Uongo siku zote,naona wameanza kufunga vihadithi vyao eti oooh madictator hujijengeaga uaminifu kwa wananchi ili wapendwe.Wamesahau maneno yao kua JPM hakubaliki na watu na Sasa wamepigwa na butwaa,wamezoea siasa maji taka na Uongo Uongo mwingi,wakafanye kazi na wao basi na si kutegemea siasa kuendesha maisha yao
 
Ngoja nimwambie kitu
Ukishakufa utapewa kila aina ya sifa
Mfano Ruge kuna watu walikuwa hawamfahamu au kumuona, lakini siku amefariki watu tulijazana barabarani kwasababu vyombo vya habari vilimtangaza sana
Ni hivyo yaani
 
Magufuli alionyesha utofauti kama kiongozi tangu mwanzo wa safari yake ya uongozi na siasa.Katika ngazi zote za utendaji na kama Waziri,alitimiza wajibu wake katika kila eneo.Akawa kivutio kikubwa kwa wananchi na hata adui zake ndani na nje ya nchi.

Kwa siri adui zake walikiri umahiri wake katika utendaji,ingawa hadharani,walionyesha chuki dhidi yake.Magufuli hakuwa fisadi.Hata hivyo adui zake walijaribu kila walipoweza kumpaka matope,ili aonekane kwamba naye ni fisadi na ana tabia za hovyo kama wao.Ila ukweli utabaki kuwa Magufuli hakuwa fisadi,kinyume chake alichukia ufisadi wa aina yeyote.

Chuki dhidi ya Magufuli zilionekana hata ndani ya chama chake.Yeye kwa sababu ya utendaji wake uliotukuka, alikuwa hukumu tosha kwa viongozi wengine wababaishaji.Sitaficha ukweli kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2015,CCM ilikuwa njia panda,CCM ilikuwa inakaribia kuaga duru za kiasa za Tanzania.Kama chama, CCM ilijisahau,ikaweka maslahi ya wananchi pembeni na kukumbatia mafisadi wa aina zote na mabeberu.Mtizamo huu wa CCM ulifika kilele chake kwa kupitishwa Azimio Zanzibar, Azimio ambalo lilikumbatia ubepari na mafisadi moja kwa moja.

Hali ya wananchi kiuchumi iliendelea kuzorota,huku mafisadi na mabeberu wakiendelea kuneemeka.Tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho ikazidi kuongezeka,na vilio vya maskini vikasikika kila kona ya Tanzania.Ikawa dhahiri kwamba madiliko yalihitajika,tena kwa haraka,ili kubadili hali hiyo.Hata hivyo wanyonge hawakuwa na mtetezi na hali yao ikazidi kuwa mbaya.Uonevu wa kila aina ulionekana kila mahali,haki zikapotea.Mahakama badala ya kutoa haki kwa wananchi kikawa chombo cha kulinda mafisadi na na mabeberu,huku chombo hicho kikinyang'anya haki za wananchi.Jeshi la Polisi nalo likasimamia dhuluma,badala ya kusimamia haki na kulinda wananchi na mali zao.Badala yake wakalinda maovu kama uuzaji wa madawa ya kulevya na wizi.Polisi wakaogopwa badala ya kuwa kimbilio la wanyonge.Magereza yakajaa vibaka,na waliopaswa kuwepo magerezani wakawa mtaani wakistarehe, huku wakikebehi wananchi.

Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa uchaguzi Tanzania.Lakini kwa jinsi hali ya nchi ilivyokuwa,hapakuwa na shaka yeyote kwamba CCM ingepoteza uchaguzi ule na upinzani,specifically CHADEMA wangeingia Ikulu

Nilishasema hapo awali kwamba Magufuli alikuwa hukumu kwa viongozi wenzie kwa sababu ya umahiri wake katika utendaji.Niseme hapa pia kwamba wananchi walimkubali sana Magufuli,kwa sababu ya uaminifu wake na utendaji wake.Kwa bahati mbaya ndani ya CCM hapakuwa na kiongozi aliyekuwa na sifa zinazokubalika na wananchi,isipokuwa Magufuli,ingawa alikuwa hakubaliki sana ndani ya chama chake.Hii ikakilazimu chama kumchagua kupereusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa 2015.

Ni historia, sasa kwamba Magufuli alishinda katika uchaguzi ule.Baada ya ushindi wa kishindo na kusimikwa kuwa Rais,Magufuli alianza safari ya kuitengeza Tanzania mpya,safari ambayo sina shaka yeyote kwamba imemgharimu maisha yake.

Katika kuitengeneza Tanzania mpya,Magufuli alisimamia sera ya CCM kikamilifu,akaanzisha miradi mingi ambayo iliifanya Tanzania ipae kuichumi mara moja.Hii iliwezekana kwa kuwa kwanza yeye mwenyewe alikuwa mtendaji makini na mwaminifu.Hii ilimuwezesha kuunda serikali yenye watendaji waaminifu,makini na wenye weledi.Kwa hiyo kama nchi tukaweza kuongeza mapato kutoka Sh. Bil.800( tril.0.8) mpaka Tri.1.3! Fedha hii ikawa chachu ya maendeleo makubwa Tanzania kwa muda mfupi.

Niwakumbushe wasomaji wangu kwamba Magufuli ndiye aliyekuwa Rais wa kwanza kuwa na ujasiri wa kuwaambia Watanzania kwamba Tanzania ni tajiri.Wengine wote walijitahidi kuwa-aminisha Watanzania kwamba Tanzania ni nchi maskini.Hatua hii ilionyesha wazi kwamba Magufuli hakuwa na la kuficha na kwa hiyo alikuwa Rais na kiongozi mwaminifu.

Tabia yake ya uaminifu na kuwa a "no nonsense President," iliwafanya watendaji wote chini yake nao kutenda kwa umakini na uaminifu mkubwa.Matokeo yake Tanzania ikapata maendeleo kwa muda mfupi,akawa mfano ani na nje ya Tanzania.Magufuli akapata sifa kwa wananchi aliowaongoza,wakampenda na akapata sifa duniani kote.

Magufuli hayupo nasi tena,tunae Mama Samia Suluhu.Najua kwamba Magufuli sio Mama Samia,ila kama wananchi wa Tanzania,tunategemea utendaji uliotukuka kutoka kwa Mama Samia Suluhu na hata zaidi.Tunajua the road ahead is bumpy and rough,kwa kuwa mazingira aliyokuwa nayo Hayati Magufuli hayajabadilika na ina wezekana ni magumu zaidi.Hata hivyo tunategemea utumishi uliotukuka.

Ni lazima mmoja wetu afe kwa niaba ya wengi.Magufuli umekufa kwa niaba yetu,nenda kwa amani na kwa heri hero na jabali,kipenzi cha Watanzania,na sisi tuko njiani.Karibu Mama Samia Suluhu.
Maisha yanasonga,shughuli zinasonga,ibada zinaendelea na kula watu wanaendelea kula.
 
Ukweli unatabia ya kujitenga na Uongo siku zote,naona wameanza kufunga vihadithi vyao eti oooh madictator hujijengeaga uaminifu kwa wananchi ili wapendwe.Wamesahau maneno yao kua JPM hakubaliki na watu na Sasa wamepigwa na butwaa,wamezoea siasa maji taka na Uongo Uongo mwingi,wakafanye kazi na wao basi na si kutegemea siasa kuendesha maisha yao
Hata shetani ana wafwasi wake,sifa nyingi mmezipata kiburi kwisha amani iendelee.
 
Hii ni wishful thinking mkuu.Maeneo mengi Marais makini waliondoshwa wakaja viongozi bora liende.Mifano ipo mingi,sina haja ya kuitaja.

Shida sio kuwa kiongozi,shida ni kuwa kiongozi makini aliyejitoa kuwa mtetezi wa wananchi wa ngazi zote.Tuendelee kumuomba Mungu sana.

Dhana kwamba muda wake umeisha siikubali,Tanzania needed him.

Watu wasiojifahamu wana sauti kama wewe!! So unasema kwa kuwa JPM ametutoka basi ndio mwisho wa taifa la Tanzania???

Mnataja Mungu sana lakini ni kwa dhihaka. Sasa inaonekana unajua kuwa hakutakuwa na mtu mwingine!! Una uungu wowote wa kujua waTanzania wote wa sasa na wajao hawatatosha???
 
Zama zaje zimekwisha! Tunaendelea na na wengine!
 
Magufuli alionyesha utofauti kama kiongozi tangu mwanzo wa safari yake ya uongozi na siasa.Katika ngazi zote za utendaji na kama Waziri,alitimiza wajibu wake katika kila eneo.Akawa kivutio kikubwa kwa wananchi na hata adui zake ndani na nje ya nchi.

Kwa siri adui zake walikiri umahiri wake katika utendaji,ingawa hadharani,walionyesha chuki dhidi yake.Magufuli hakuwa fisadi.Hata hivyo adui zake walijaribu kila walipoweza kumpaka matope,ili aonekane kwamba naye ni fisadi na ana tabia za hovyo kama wao.Ila ukweli utabaki kuwa Magufuli hakuwa fisadi,kinyume chake alichukia ufisadi wa aina yeyote.

Chuki dhidi ya Magufuli zilionekana hata ndani ya chama chake.Yeye kwa sababu ya utendaji wake uliotukuka, alikuwa hukumu tosha kwa viongozi wengine wababaishaji.Sitaficha ukweli kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2015,CCM ilikuwa njia panda,CCM ilikuwa inakaribia kuaga duru za kiasa za Tanzania.Kama chama, CCM ilijisahau,ikaweka maslahi ya wananchi pembeni na kukumbatia mafisadi wa aina zote na mabeberu.Mtizamo huu wa CCM ulifika kilele chake kwa kupitishwa Azimio Zanzibar, Azimio ambalo lilikumbatia ubepari na mafisadi moja kwa moja.

Hali ya wananchi kiuchumi iliendelea kuzorota,huku mafisadi na mabeberu wakiendelea kuneemeka.Tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho ikazidi kuongezeka,na vilio vya maskini vikasikika kila kona ya Tanzania.Ikawa dhahiri kwamba madiliko yalihitajika,tena kwa haraka,ili kubadili hali hiyo.Hata hivyo wanyonge hawakuwa na mtetezi na hali yao ikazidi kuwa mbaya.Uonevu wa kila aina ulionekana kila mahali,haki zikapotea.Mahakama badala ya kutoa haki kwa wananchi kikawa chombo cha kulinda mafisadi na na mabeberu,huku chombo hicho kikinyang'anya haki za wananchi.Jeshi la Polisi nalo likasimamia dhuluma,badala ya kusimamia haki na kulinda wananchi na mali zao.Badala yake wakalinda maovu kama uuzaji wa madawa ya kulevya na wizi.Polisi wakaogopwa badala ya kuwa kimbilio la wanyonge.Magereza yakajaa vibaka,na waliopaswa kuwepo magerezani wakawa mtaani wakistarehe, huku wakikebehi wananchi.

Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa uchaguzi Tanzania.Lakini kwa jinsi hali ya nchi ilivyokuwa,hapakuwa na shaka yeyote kwamba CCM ingepoteza uchaguzi ule na upinzani,specifically CHADEMA wangeingia Ikulu

Nilishasema hapo awali kwamba Magufuli alikuwa hukumu kwa viongozi wenzie kwa sababu ya umahiri wake katika utendaji.Niseme hapa pia kwamba wananchi walimkubali sana Magufuli,kwa sababu ya uaminifu wake na utendaji wake.Kwa bahati mbaya ndani ya CCM hapakuwa na kiongozi aliyekuwa na sifa zinazokubalika na wananchi,isipokuwa Magufuli,ingawa alikuwa hakubaliki sana ndani ya chama chake.Hii ikakilazimu chama kumchagua kupereusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa 2015.

Ni historia, sasa kwamba Magufuli alishinda katika uchaguzi ule.Baada ya ushindi wa kishindo na kusimikwa kuwa Rais,Magufuli alianza safari ya kuitengeza Tanzania mpya,safari ambayo sina shaka yeyote kwamba imemgharimu maisha yake.

Katika kuitengeneza Tanzania mpya,Magufuli alisimamia sera ya CCM kikamilifu,akaanzisha miradi mingi ambayo iliifanya Tanzania ipae kuichumi mara moja.Hii iliwezekana kwa kuwa kwanza yeye mwenyewe alikuwa mtendaji makini na mwaminifu.Hii ilimuwezesha kuunda serikali yenye watendaji waaminifu,makini na wenye weledi.Kwa hiyo kama nchi tukaweza kuongeza mapato kutoka Sh. Bil.800( tril.0.8) mpaka Tri.1.3! Fedha hii ikawa chachu ya maendeleo makubwa Tanzania kwa muda mfupi.

Niwakumbushe wasomaji wangu kwamba Magufuli ndiye aliyekuwa Rais wa kwanza kuwa na ujasiri wa kuwaambia Watanzania kwamba Tanzania ni tajiri.Wengine wote walijitahidi kuwa-aminisha Watanzania kwamba Tanzania ni nchi maskini.Hatua hii ilionyesha wazi kwamba Magufuli hakuwa na la kuficha na kwa hiyo alikuwa Rais na kiongozi mwaminifu.

Tabia yake ya uaminifu na kuwa a "no nonsense President," iliwafanya watendaji wote chini yake nao kutenda kwa umakini na uaminifu mkubwa.Matokeo yake Tanzania ikapata maendeleo kwa muda mfupi,akawa mfano ani na nje ya Tanzania.Magufuli akapata sifa kwa wananchi aliowaongoza,wakampenda na akapata sifa duniani kote.

Magufuli hayupo nasi tena,tunae Mama Samia Suluhu.Najua kwamba Magufuli sio Mama Samia,ila kama wananchi wa Tanzania,tunategemea utendaji uliotukuka kutoka kwa Mama Samia Suluhu na hata zaidi.Tunajua the road ahead is bumpy and rough,kwa kuwa mazingira aliyokuwa nayo Hayati Magufuli hayajabadilika na ina wezekana ni magumu zaidi.Hata hivyo tunategemea utumishi uliotukuka.

Ni lazima mmoja wetu afe kwa niaba ya wengi.Magufuli umekufa kwa niaba yetu,nenda kwa amani na kwa heri hero na jabali,kipenzi cha Watanzania,na sisi tuko njiani.Karibu Mama Samia Suluhu.
Tupate tena muuaji, mtekaji, mtesaji na mwenye roho mbaya kama magu?
 
Watu wasiojifahamu wana sauti kama wewe!! So unasema kwa kuwa JPM ametutoka basi ndio mwisho wa taifa la Tanzania???

Mnataja Mungu sana lakini ni kwa dhihaka. Sasa inaonekana unajua kuwa hakutakuwa na mtu mwingine!! Una uungu wowote wa kujua waTanzania wote wa sasa na wajao hawatatosha???
Umeniwekea maneno mdomoni mwangu.Taifa Tanzania litaendelea ila inawezekana not in the manner we would like.Ndio maana nimesema tumuombe Mungu Rais ajaye aipende nchi yake
 
Tupate tena muuaji, mtekaji, mtesaji na mwenye roho mbaya kama magu?
Mawazo haya umepandikiziwa akilini mwako,na kwa kuwa na wewe hujiongezi umeyachukulia kwamba ni kweli.Hakuna nchi yeyote duniani ambayo utafanya vitendo vya ku-sabotage nchi halafu ukaangaliwa tu,none.Uhuru una mipaka.

Finally ogopa sana mtu ambaye the West wanampenda,wana maslahi naye na ni saboteur.Angalia quotes za Marehemu Samora Machel👇.They speak all.
 
Attachments

  • IMG-20210320-WA0005.jpg
    IMG-20210320-WA0005.jpg
    48.8 KB · Views: 1
JPM alikuwa ni mpango mzima wa Mungu wa Mbinguni. Ukiona mkalimani anazomewa kwenye mazishi kwa kupotosha katika kutafasiri jua ya jayo yanafurahisha kama kutakosekana umakini kwenye maamuzi ya msingi ya Taifa hili.

Huyu mtu amepanda mbegu ambayo hamna wa kuififisha kirahisi rahisi tu. Si kwa wananchi wa Tanzania bali leo nimegundua kumbe hata kwa watu wengi dunia.

Viongozi Marais waliohudhuria mazishi leo Dodoma utaona hutuba zao zinaonesha wamelazimika kuja maana hata wananchi wao wanamkubaki JPM.

Wanasiasa matapeli na misheni taoni wanaofikria Magufuli kaondoka ndio watapata nafasi za kuzimua dilizi zao wanajidanganya saanaa.
 
Mawazo haya umepandikiziwa akilini mwako,na kwa kuwa na wewe hujiongezi umeyachukulia kwamba ni kweli.Hakuna nchi yeyote duniani ambayo utafanya vitendo vya ku-sabotage nchi halafu ukaangaliwa tu,none.Uhuru una mipaka.

Finally ogopa sana mtu ambaye the West wanampenda,wana maslahi naye na ni saboteur.Angalia quotes za Marehemu Samora Machel👇.They speak all.
Huwezi kunishawishi nimkubali muuaji, sheria na mahakama zipo, kama mtu ametenda kosa mfikishe mahakamani. Hizo propaganda za kizamani kuhusu west zimepitwa na wakati. Nchi zetu hizi bila misaada yao hatuwezi kujiendesha. Ila Mungu ni mkubwa, muuaji naye anakufa
 
Back
Top Bottom